< Yona 4 >
1 Lakini Yona alichukizwa sana akakasirika.
Lakini hili lilimchukiza Yona naye akakasirika.
2 Akamwomba Bwana, “Ee Bwana, hili si lile nililolisema nilipokuwa ningali nyumbani? Hii ndiyo sababu niliharikisha kukimbilia Tarshishi. Nikifahamu kuwa wewe ni Mungu mwenye neema na huruma, si mwepesi wa hasira na umejaa upendo, ni Mungu ambaye hughairi katika kupeleka maafa.
Basi Yona akamwomba Bwana akasema, “Ee, Bwana, hiya sio yale niliyosema wakati niliporudi katika nchi yangu? Ndiyo maana nilifanya haraka na kujaribu kukimbia Tarshishi-kwa sababu nilijua kuwa wewe ni Mungu mwenye neema, mwenye huruma, si meingi wa hasira, mwingi kwa uaminifu, na hughairi maafa.
3 Sasa, Ee Bwana, niondolee uhai wangu, kwa kuwa ni afadhali mimi nife kuliko kuishi.”
Kwa hiyo sasa, Bwana, nakuomba, uniondoe uhai wangu, kwa maana ni bora kwangu kufa kuliko kuishi.”
4 Lakini Bwana akamjibu, “Je unayo haki yoyote kukasirika?”
Bwana akasema, Je, ni vema kwamba umekasirika?”
5 Yona akatoka nje akaketi mahali upande wa mashariki wa mji. Hapo akajitengenezea kibanda, akaketi kwenye kivuli chake na kungojea ni nini kitakachotokea katika mji.
Kisha Yona akaondoka mjini akaketi upande wa mashariki wa jiji. Huko alifanya makao na akaketi chini yake katika kivuli ili aweze kuona mji utakuwaje.
6 Ndipo Bwana, Mungu akaweka tayari mzabibu na kuufanya uote, kumpa Yona kivuli kilichomfunika kichwa ili kuondoa taabu yake, naye Yona akafurahi sana kwa ajili ya ule mzabibu.
Bwana Mungu aliandaa mmea na kuukuza juu ya Yona ili uwe kivuli juu ya kichwa chake ili kupunguza dhiki yake. Yona alikuwa na furaha kubwa kwa sababu ya mmea.
7 Lakini kesho yake asubuhi na mapema Mungu akaamuru buu, autafune mzabibu huo nao ukanyauka.
Lakini Mungu aliandaa mdudu kulipopambazuka asubuhi iliyofuata. Alishambulia mmea na mmea ukapooza.
8 Wakati jua lilipochomoza, Mungu akautuma upepo wa hari wa mashariki, nalo jua likawaka juu ya kichwa cha Yona mpaka akazimia. Akatamani kufa, naye akasema, “Ni afadhali mimi nife kuliko kuishi.”
Ikawa wakati jua lilipochomoza asubuhi, Mungu aliandaa upepo mkali wa mashariki. Pia, jua lilipiga kichwa cha Yona na akaanguka. Kisha Yona alitamani kufa. Akajiambia, “Ni bora kwangu kufa kuliko kuishi.”
9 Lakini Mungu alimwambia Yona, “Je, unayo haki kukasirika kuhusu mzabibu huo?” Akasema, “Ndiyo, ninayo haki. Nimekasirika kiasi cha kufa.”
Kisha Mungu akamwambia Yona, “Je, ni vema wewe kuwa na hasira juu ya mmea?” Yona akasema, Ni vyema kuwa nimekasirika hata kufa.
10 Lakini Bwana akamwambia, “Wewe unakasirika kwa ajili ya mzabibu huu, nawe hukuusababisha kuota wala kuutunza. Uliota usiku mmoja, nao ukafa usiku mmoja.
Bwana akasema, Umeuhurumia mmea, ambao haukuufanyia kazi wala haukukua. Uliomea katika usiku na kufa usiku.
11 Lakini Ninawi ina zaidi ya watu 120,000 ambao hawawezi kupambanua kulia au kushoto, pamoja na ngʼombe wengi. Je, hainipasi kufikiri juu ya mji ule mkubwa?”
Kwa hiyo mimi, haikunipassa kuuhurumia Ninawi, mji mkuu, ambalo kuna watu zaidi ya mia na ishirini elfu ambao hawajui tofauti kati ya mkono wao wa kulia na mkono wao wa kushoto, na pia ng'ombe wengi?