< Yohana 7 >

1 Baada ya mambo haya, Yesu alikwenda sehemu mbalimbali za Galilaya. Hakutaka kwenda Uyahudi kwa sababu Wayahudi huko walitaka kumuua.
post haec ambulabat Iesus in Galilaeam non enim volebat in Iudaeam ambulare quia quaerebant eum Iudaei interficere
2 Sikukuu ya Vibanda ya Wayahudi ilikuwa imekaribia.
erat autem in proximo dies festus Iudaeorum scenopegia
3 Hivyo ndugu zake Yesu wakamwambia, “Ondoka hapa uende Uyahudi ili wanafunzi Wako wapate kuona miujiza unayofanya.
dixerunt autem ad eum fratres eius transi hinc et vade in Iudaeam ut et discipuli tui videant opera tua quae facis
4 Mtu anayetaka kujulikana hafanyi mambo yake kwa siri. Kama unafanya mambo haya, jionyeshe kwa ulimwengu.”
nemo quippe in occulto quid facit et quaerit ipse in palam esse si haec facis manifesta te ipsum mundo
5 Hata ndugu zake mwenyewe hawakumwamini.
neque enim fratres eius credebant in eum
6 Yesu akawaambia, “Wakati wangu bado haujawadia, lakini wakati wenu upo siku zote.
dicit ergo eis Iesus tempus meum nondum advenit tempus autem vestrum semper est paratum
7 Ulimwengu hauwezi kuwachukia ninyi, lakini unanichukia mimi kwa sababu ninawashuhudia kwamba matendo yao ni maovu.
non potest mundus odisse vos me autem odit quia ego testimonium perhibeo de illo quia opera eius mala sunt
8 Ninyi nendeni kwenye Sikukuu, lakini mimi sitahudhuria Sikukuu hii kwa sababu wakati wangu haujawadia.”
vos ascendite ad diem festum hunc ego non ascendo ad diem festum istum quia meum tempus nondum impletum est
9 Akiisha kusema hayo, akabaki Galilaya.
haec cum dixisset ipse mansit in Galilaea
10 Lakini ndugu zake walipokwisha kuondoka kwenda kwenye Sikukuu, yeye pia alikwenda lakini kwa siri.
ut autem ascenderunt fratres eius tunc et ipse ascendit ad diem festum non manifeste sed quasi in occulto
11 Wayahudi walikuwa wakimtafuta huko kwenye Sikukuu na kuulizana, “Yuko wapi huyu mtu?”
Iudaei ergo quaerebant eum in die festo et dicebant ubi est ille
12 Kulikuwa na minongʼono iliyoenea kumhusu Yesu katika umati wa watu, wakati wengine wakisema, “Ni mtu mwema.” Wengine walikuwa wakisema, “La, yeye anawadanganya watu.”
et murmur multus de eo erat in turba; quidam enim dicebant quia bonus est alii autem dicebant non sed seducit turbas
13 Lakini hakuna mtu yeyote aliyemsema waziwazi kumhusu kwa sababu ya kuwaogopa Wayahudi.
nemo tamen palam loquebatur de illo propter metum Iudaeorum
14 Ilipokaribia katikati ya Sikukuu, Yesu alipanda kwenda Hekaluni na kuanza kufundisha.
iam autem die festo mediante ascendit Iesus in templum et docebat
15 Wayahudi wakastaajabia mafundisho yake wakasema, “Mtu huyu amepataje kujua mambo haya bila kufundishwa?”
et mirabantur Iudaei dicentes quomodo hic litteras scit cum non didicerit
16 Ndipo Yesu akawajibu, “Mafundisho yangu si yangu mwenyewe, bali yanatoka kwake yeye aliyenituma.
respondit eis Iesus et dixit mea doctrina non est mea sed eius qui misit me
17 Mtu yeyote akipenda kufanya mapenzi ya Mungu, atajua kama mafundisho yangu yanatoka kwa Mungu au ninasema kwa ajili yangu mwenyewe.
si quis voluerit voluntatem eius facere cognoscet de doctrina utrum ex Deo sit an ego a me ipso loquar
18 Wale wanenao kwa ajili yao wenyewe hufanya hivyo kwa kutaka utukufu wao wenyewe. Lakini yeye atafutaye utukufu wa yule aliyemtuma ni wa kweli, wala hakuna uongo ndani yake.
qui a semet ipso loquitur gloriam propriam quaerit qui autem quaerit gloriam eius qui misit illum hic verax est et iniustitia in illo non est
19 Je, Mose hakuwapa ninyi sheria? Lakini hakuna hata mmoja wenu anayeishika hiyo sheria. Kwa nini mnataka kuniua?”
nonne Moses dedit vobis legem et nemo ex vobis facit legem
20 Ule umati wa watu ukamjibu, “Wewe una pepo mchafu! Ni nani anayetaka kukuua?”
quid me quaeritis interficere respondit turba et dixit daemonium habes quis te quaerit interficere
21 Yesu akawajibu, “Nimefanya muujiza mmoja na nyote mkastaajabu.
respondit Iesus et dixit eis unum opus feci et omnes miramini
22 Lakini kwa kuwa Mose aliwaamuru tohara (ingawa kwa kweli haikutoka kwa Mose bali kwa baba zenu wakuu), mnamtahiri mtoto hata siku ya Sabato.
propterea Moses dedit vobis circumcisionem non quia ex Mose est sed ex patribus et in sabbato circumciditis hominem
23 Ikiwa mtoto aweza kutahiriwa siku ya Sabato kusudi sheria ya Mose isivunjwe, kwa nini mnanikasirikia kwa kumponya mtu mwili wake wote siku ya Sabato?
si circumcisionem accipit homo in sabbato ut non solvatur lex Mosi mihi indignamini quia totum hominem sanum feci in sabbato
24 Acheni kuhukumu mambo kwa jinsi mnavyoona tu, bali hukumuni kwa haki.”
nolite iudicare secundum faciem sed iustum iudicium iudicate
25 Ndipo baadhi ya watu wa Yerusalemu wakawa wanasema, “Tazameni, huyu si yule mtu wanayetaka kumuua?
dicebant ergo quidam ex Hierosolymis nonne hic est quem quaerunt interficere
26 Mbona yuko hapa anazungumza hadharani na wala hawamwambii neno lolote? Je, inawezekana viongozi wanafahamu kuwa huyu ndiye Kristo?
et ecce palam loquitur et nihil ei dicunt numquid vere cognoverunt principes quia hic est Christus
27 Tunafahamu huyu mtu anakotoka, lakini Kristo atakapokuja, hakuna yeyote atakayejua atokako.”
sed hunc scimus unde sit Christus autem cum venerit nemo scit unde sit
28 Ndipo Yesu, akaendelea kufundisha Hekaluni, akisema, “Ninyi mnanifahamu na kujua nitokako. Mimi sikuja kwa ajili yangu mwenyewe, bali yeye aliyenituma ni wa kweli na ninyi hammjui.
clamabat ergo docens in templo Iesus et dicens et me scitis et unde sim scitis et a me ipso non veni sed est verus qui misit me quem vos non scitis
29 Mimi namjua kwa kuwa nimetoka kwake, naye ndiye alinituma.”
ego scio eum quia ab ipso sum et ipse me misit
30 Ndipo wakatafuta kumkamata, lakini hakuna mtu yeyote aliyethubutu kumshika kwa sababu saa yake ilikuwa bado haijawadia.
quaerebant ergo eum adprehendere et nemo misit in illum manus quia nondum venerat hora eius
31 Nao watu wengi wakamwamini, wakasema, “Je, Kristo atakapokuja, atafanya miujiza mikuu zaidi kuliko aliyoifanya mtu huyu?”
de turba autem multi crediderunt in eum et dicebant Christus cum venerit numquid plura signa faciet quam quae hic facit
32 Mafarisayo wakasikia watu wakinongʼona mambo kama hayo kuhusu Yesu, ndipo wao pamoja na viongozi wa makuhani wakatuma walinzi wa Hekalu waende kumkamata.
audierunt Pharisaei turbam murmurantem de illo haec et miserunt principes et Pharisaei ministros ut adprehenderent eum
33 Yesu akasema, “Mimi bado niko pamoja nanyi kwa kitambo kidogo, kisha nitarudi kwake yeye aliyenituma.
dixit ergo Iesus adhuc modicum tempus vobiscum sum et vado ad eum qui misit me
34 Mtanitafuta lakini hamtaniona, nami niliko ninyi hamwezi kuja.”
quaeretis me et non invenietis et ubi sum ego vos non potestis venire
35 Wayahudi wakaulizana wao kwa wao, “Huyu mtu anataka kwenda wapi ambako hatuwezi kumfuata? Je, anataka kwenda kwa Wayunani ambako baadhi ya watu wetu wametawanyikia, akawafundishe Wayunani?
dixerunt ergo Iudaei ad se ipsos quo hic iturus est quia non inveniemus eum numquid in dispersionem gentium iturus est et docturus gentes
36 Yeye ana maana gani anaposema, ‘Mtanitafuta lakini hamtaniona,’ na, ‘nami niliko ninyi hamwezi kuja’?”
quis est hic sermo quem dixit quaeretis me et non invenietis et ubi sum ego non potestis venire
37 Siku ile ya mwisho ya Sikukuu, siku ile kuu, wakati Yesu akiwa amesimama huko, akapaza sauti yake akasema, “Kama mtu yeyote anaona kiu na aje kwangu anywe.
in novissimo autem die magno festivitatis stabat Iesus et clamabat dicens si quis sitit veniat ad me et bibat
38 Yeyote aniaminiye mimi, kama Maandiko yasemavyo, vijito vya maji ya uzima vitatiririka ndani mwake.”
qui credit in me sicut dixit scriptura flumina de ventre eius fluent aquae vivae
39 Yesu aliposema haya alimaanisha Roho Mtakatifu ambaye wote waliomwamini wangempokea, kwani mpaka wakati huo, Roho alikuwa hajatolewa, kwa kuwa Yesu alikuwa bado hajatukuzwa.
hoc autem dixit de Spiritu quem accepturi erant credentes in eum non enim erat Spiritus quia Iesus nondum fuerat glorificatus
40 Waliposikia maneno hayo, baadhi ya watu miongoni mwa ule umati wakasema, “Hakika huyu ndiye yule Nabii.”
ex illa ergo turba cum audissent hos sermones eius dicebant hic est vere propheta
41 Wengine wakasema, “Huyu ndiye Kristo!” Lakini wengine wakauliza, “Je, Kristo kwao ni Galilaya?
alii dicebant hic est Christus quidam autem dicebant numquid a Galilaea Christus venit
42 Je, Maandiko hayasemi kwamba Kristo atakuja kutoka jamaa ya Daudi na kutoka Bethlehemu, mji alioishi Daudi?”
nonne scriptura dicit quia ex semine David et Bethleem castello ubi erat David venit Christus
43 Kwa hiyo watu wakagawanyika kwa ajili ya Yesu.
dissensio itaque facta est in turba propter eum
44 Baadhi yao walitaka kumkamata, lakini hakuna aliyethubutu kumgusa.
quidam autem ex ipsis volebant adprehendere eum sed nemo misit super illum manus
45 Hatimaye wale walinzi wa Hekalu wakarudi kwa viongozi wa makuhani na Mafarisayo waliokuwa wamewatuma ili kumkamata Yesu, wakaulizwa, “Mbona hamkumkamata?”
venerunt ergo ministri ad pontifices et Pharisaeos et dixerunt eis illi quare non adduxistis eum
46 Wale walinzi wakajibu, “Kamwe hajanena mtu yeyote kama yeye anenavyo.”
responderunt ministri numquam sic locutus est homo sicut hic homo
47 Mafarisayo wakajibu, “Je, nanyi pia mmedanganyika?
responderunt ergo eis Pharisaei numquid et vos seducti estis
48 Je, kuna kiongozi yeyote au mmoja wa Mafarisayo ambaye amemwamini?
numquid aliquis ex principibus credidit in eum aut ex Pharisaeis
49 Lakini huu umati wa watu wasiojua Sheria ya Mose, wamelaaniwa.”
sed turba haec quae non novit legem maledicti sunt
50 Ndipo Nikodemo, yule aliyekuwa amemwendea Yesu siku moja usiku, ambaye alikuwa mmoja wao akauliza,
dicit Nicodemus ad eos ille qui venit ad eum nocte qui unus erat ex ipsis
51 “Je, sheria zetu zinaturuhusu kumhukumu mtu kabla ya kumsikiliza na kufahamu alilotenda?”
numquid lex nostra iudicat hominem nisi audierit ab ipso prius et cognoverit quid faciat
52 Wakamjibu, “Je, wewe pia unatoka Galilaya? Chunguza nawe utaona kwamba hakuna nabii atokae Galilaya!” [
responderunt et dixerunt ei numquid et tu Galilaeus es scrutare et vide quia propheta a Galilaea non surgit
53 Kisha wakaondoka, kila mtu akarudi nyumbani kwake.
et reversi sunt unusquisque in domum suam

< Yohana 7 >