< Yohana 6 >
1 Baada ya haya, Yesu alikwenda ngʼambo ya Bahari ya Galilaya, ambayo pia huitwa Bahari ya Tiberia.
After these things Jesus went over the sea of Galilee, which is [the sea] of Tiberias.
2 Umati mkubwa wa watu uliendelea kumfuata, kwa sababu waliona ishara nyingi za miujiza alizofanya kwa wagonjwa.
And a great multitude followed him, because they saw his miracles which he performed on them that were diseased.
3 Kisha Yesu akapanda mlimani akaketi huko pamoja na wanafunzi wake.
And Jesus went upon a mountain, and there he sat with his disciples.
4 Pasaka ya Wayahudi ilikuwa imekaribia.
And the passover, a feast of the Jews, was nigh.
5 Yesu alipotazama na kuuona ule umati mkubwa wa watu ukimjia, akamwambia Filipo, “Tutanunua wapi mikate ili watu hawa wale?”
When Jesus then lifted up [his] eyes, and saw a great company come to him, he saith to Philip, Whence shall we buy bread that these may eat?
6 Aliuliza swali hili kumpima, kwa maana alishajua la kufanya.
(And this he said to prove him: for he himself knew what he would do.)
7 Filipo akamjibu, “Hata fedha kiasi cha dinari mia mbili, hazitoshi kununua mikate ya kuwapa watu hawa ili kila mtu apate kidogo.”
Philip answered him, Two hundred penny-worth of bread is not sufficient for them, that every one of them make take a little:
8 Mmoja wa wanafunzi wake aitwaye Andrea, ndugu yake Simoni Petro, akamwambia,
One of his disciples, Andrew, Simon Peter's brother, saith to him,
9 “Hapa kuna mvulana mmoja mwenye mikate mitano ya shayiri na samaki wawili wadogo. Lakini hivi vitatosha nini kwa umati huu wote?”
There is a lad here, who hath five barley-loaves, and two small fishes: but what are they among so many?
10 Yesu akasema, “Waketisheni watu chini.” Palikuwa na majani mengi katika eneo lile, nao watu wakaketi. Palikuwa na wanaume wapatao 5,000.
And Jesus said, Make the men sit down. (Now there was much grass in the place.) So the men sat down in number about five thousand.
11 Ndipo Yesu akachukua ile mikate, akamshukuru Mungu na kuwagawia wale watu waliokuwa wameketi. Akafanya vivyo hivyo na wale samaki. Kila mtu akapata kadiri alivyotaka.
And Jesus took the loaves; and when he had given thanks, he distributed to the disciples, and the disciples to them that were set down; and likewise of the fishes, as much as they would.
12 Watu wote walipokwisha kula na kushiba, akawaambia wanafunzi wake, “Kusanyeni vipande vilivyobaki vya ile mikate, kisipotee chochote.”
When they were satisfied, he said to his disciples, Gather the fragments that remain, that nothing may be lost.
13 Hivyo wakavikusanya, wakajaza vikapu kumi na viwili kwa vipande vya ile mikate mitano ya shayiri na samaki wale wawili wadogo vilivyobakishwa na waliokula.
Therefore they gathered [them], and filled twelve baskets with the fragments of the five barley-loaves, which remained over and above to them that had eaten.
14 Baada ya watu kuona muujiza ule Yesu aliofanya, walianza kusema, “Hakika huyu ndiye Nabii ajaye ulimwenguni!”
Then those men, when they had seen the miracle that Jesus performed, said, This is truly that prophet that should come into the world.
15 Yesu akijua kwamba walitaka kuja kumfanya awe mfalme wao, kwa nguvu, akajitenga nao akaenda milimani peke yake.
When Jesus therefore perceived that they would come and take him by force, to make him a king, he departed again to a mountain himself alone.
16 Ilipofika jioni, wanafunzi wake waliteremka kwenda baharini.
And when evening had [now] come, his disciples went down to the sea,
17 Wakaingia kwenye mashua, wakaanza kuvuka bahari kwenda Kapernaumu. Wakati huu kulikuwa tayari giza na Yesu alikuwa hajajumuika nao.
And entered into a boat, and went over the sea towards Capernaum. And it was now dark, and Jesus had not come to them.
18 Bahari ikachafuka kwa sababu upepo mkali ulikuwa unavuma.
And the sea arose by reason of a great wind that blew.
19 Wanafunzi walipokuwa wamekwenda mwendo wa karibu maili tatu au nne, walimwona Yesu akitembea juu ya maji akikaribia mashua, nao wakaogopa sana.
So when they had rowed about five and twenty or thirty furlongs, they see Jesus walking on the sea, and drawing nigh to the boat: and they were afraid.
20 Lakini Yesu akawaambia, “Ni mimi. Msiogope.”
But he saith to them, It is I; be not afraid.
21 Ndipo wakamkaribisha kwa furaha ndani ya mashua, na mara wakafika ufuoni walikokuwa wakienda.
Then they willingly received him into the boat: and immediately the boat was at the land whither they were going.
22 Siku iliyofuata, wale watu waliokuwa wamebaki ngʼambo waliona kwamba palikuwepo na mashua moja tu na kwamba Yesu hakuwa ameondoka pamoja na wanafunzi wake, ila walikuwa wameondoka peke yao.
The day following, when the people who stood on the other side of the sea saw that there was no other boat there, save that one into which his disciples had entered, and that Jesus went not with his disciples into the boat, but [that] his disciples had gone away alone;
23 Lakini zikaja mashua nyingine kutoka Tiberia zikafika karibu na mahali pale walipokula mikate baada ya Bwana kumshukuru Mungu.
(Yet there came other boats from Tiberias nigh to the place where they ate bread, after the Lord had given thanks: )
24 Mara wale watu wakatambua kwamba Yesu hakuwepo hapo, wala wanafunzi wake. Wakaingia kwenye mashua hizo, wakaenda Kapernaumu ili kumtafuta Yesu.
When the people therefore saw that Jesus was not there, neither his disciples, they also took boats, and came to Capernaum, seeking for Jesus.
25 Walipomkuta Yesu ngʼambo ya bahari wakamuuliza, “Rabi, umefika lini huku?”
And when they had found him on the other side of the sea, they said to him, Rabbi, when camest thou hither?
26 Yesu akawajibu, “Amin, amin nawaambia, ninyi hamnitafuti kwa kuwa mliona ishara na miujiza, bali kwa sababu mlikula ile mikate mkashiba.
Jesus answered them and said, Verily, verily, I say to you, Ye seek me, not because ye saw the miracles, but because ye ate of the loaves, and were satisfied.
27 Msishughulikie chakula kiharibikacho, bali chakula kidumucho hata uzima wa milele, ambacho Mwana wa Adamu atawapa. Yeye ndiye ambaye Mungu Baba amemtia muhuri.” (aiōnios )
Labor not for the food which perisheth, but for that food which endureth to everlasting life, which the Son of man will give to you: for him hath God the Father sealed. (aiōnios )
28 Ndipo wakamuuliza, “Tufanye nini ili tupate kuitenda kazi ya Mungu?”
Then said they to him, What shall we do, that we may work the works of God?
29 Yesu akawajibu, “Kazi ya Mungu ndiyo hii: Mwaminini yeye aliyetumwa naye.”
Jesus answered and said to them, This is the work of God, that ye believe on him whom he hath sent.
30 Hivyo wakamuuliza, “Utafanya ishara gani ya muujiza, ili tuione tukuamini? Utafanya jambo gani?
They said therefore to him, What sign showest thou then, that we may see, and believe thee? what dost thou work?
31 Baba zetu walikula mana jangwani, kama ilivyoandikwa, ‘Aliwapa mikate kutoka mbinguni ili wale.’”
Our fathers ate manna in the desert; as it is written, He gave them bread from heaven to eat.
32 Yesu akawaambia, “Amin, amin nawaambia, si Mose aliyewapa mikate kutoka mbinguni, bali Baba yangu ndiye anawapa mkate wa kweli kutoka mbinguni.
Then Jesus said to them, Verily, verily, I say to you, Moses gave you not that bread from heaven; but my Father giveth you the true bread from heaven.
33 Kwa maana mkate wa Mungu ni yule ashukaye kutoka mbinguni na kuupa ulimwengu uzima.”
For the bread of God is he who cometh down from heaven, and giveth life to the world.
34 Wakamwambia, “Bwana, kuanzia sasa tupatie huo mkate siku zote.”
Then said they to him, Lord, evermore give us this bread.
35 Yesu akawaambia, “Mimi ndimi mkate wa uzima. Yeye ajaye kwangu, hataona njaa kamwe na yeye aniaminiye, hataona kiu kamwe.
And Jesus said to them, I am the bread of life: he that cometh to me, shall never hunger; and he that believeth on me, shall never thirst.
36 Lakini kama nilivyowaambia, mmeniona lakini bado hamwamini.
But I said to you, That ye also have seen me, and believe not.
37 Wale wote anipao Baba watakuja kwangu na yeyote ajaye kwangu, sitamfukuzia nje kamwe.
All that the Father giveth me, shall come to me; and him that cometh to me, I will in no wise reject.
38 Kwa kuwa nimeshuka kutoka mbinguni si ili kufanya mapenzi yangu, bali mapenzi yake yeye aliyenituma.
For I came down from heaven, not to do my own will, but the will of him that sent me.
39 Haya ndiyo mapenzi yake yeye aliyenituma, kwamba, nisimpoteze hata mmoja wa wale alionipa, bali niwafufue siku ya mwisho.
And this is the Father's will who hath sent me, that of all which he hath given me, I should lose nothing, but should raise it up again at the last day.
40 Kwa maana mapenzi ya Baba yangu ni kwamba kila mmoja amtazamaye, Mwana na kumwamini awe na uzima wa milele, nami nitawafufua siku ya mwisho.” (aiōnios )
And this is the will of him that sent me, that every one who seeth the Son, and believeth on him, may have everlasting life: and I will raise him up at the last day. (aiōnios )
41 Wayahudi wakaanza kunungʼunika kwa kuwa alisema, “Mimi ndimi mkate ulioshuka kutoka mbinguni.”
The Jews then murmured at him, because he said, I am the bread which came down from heaven.
42 Wakasema, “Huyu si Yesu, mwana wa Yosefu, ambaye baba yake na mama yake tunawajua? Anawezaje basi sasa kusema, ‘Nimeshuka kutoka mbinguni’?”
And they said, Is not this Jesus the son of Joseph, whose father and mother we know? how is it then that he saith, I came down from heaven?
43 Hivyo Yesu akawaambia, “Acheni kunungʼunikiana ninyi kwa ninyi.
Jesus therefore answered and said to them, Murmur not among yourselves.
44 Hakuna mtu awezaye kuja kwangu kama asipovutwa na Baba aliyenituma, nami nitamfufua siku ya mwisho.
No man can come to me, except the Father who hath sent me draw him: and I will raise him up at the last day.
45 Imeandikwa katika Manabii, ‘Wote watafundishwa na Mungu.’ Yeyote amsikilizaye Baba na kujifunza kutoka kwake, huyo huja kwangu.
It is written in the prophets, And they shall be all taught from God. Every man therefore that hath heard, and hath learned from the Father, cometh to me.
46 Hakuna mtu yeyote aliyemwona Baba isipokuwa yeye atokaye kwa Mungu, yeye ndiye peke yake aliyemwona Baba.
Not that any man hath seen the Father, save he who is from God, he hath seen the Father.
47 Amin, amin nawaambia, yeye anayeamini anao uzima wa milele. (aiōnios )
Verily, verily, I say to you, He that believeth on me hath everlasting life. (aiōnios )
48 Mimi ni mkate wa uzima.
I am that bread of life.
49 Baba zenu walikula mana jangwani, lakini wakafa.
Your fathers ate manna in the wilderness, and are dead.
50 Lakini hapa kuna mkate utokao mbinguni, ambao mtu yeyote akiula, hatakufa.
This is the bread which cometh down from heaven, that a man may eat of it, and not die.
51 Mimi ni mkate wa uzima ule uliotoka mbinguni. Mtu yeyote akiula mkate huu, ataishi milele. Mkate huu ni mwili wangu, ambao nitautoa kwa ajili ya uzima wa ulimwengu.” (aiōn )
I am the living bread which came down from heaven: if any man shall eat of this bread, he shall live for ever: and the bread that I will give is my flesh, which I will give for the life of the world. (aiōn )
52 Ndipo Wayahudi wakaanza kuhojiana vikali wao kwa wao wakisema, “Mtu huyu awezaje kutupatia mwili wake tuule?”
The Jews therefore contended among themselves, saying, How can this man give us [his] flesh to eat?
53 Hivyo Yesu akawaambia, “Amin, amin nawaambia, msipoula mwili wa Mwana wa Adamu na kuinywa damu yake, hamna uzima ndani yenu.
Then Jesus said to them, Verily, verily, I say to you, Except ye eat the flesh of the Son of man, and drink his blood, ye have no life in you.
54 Mtu yeyote aulaye mwili wangu na kunywa damu yangu, anao uzima wa milele. Nami nitamfufua siku ya mwisho. (aiōnios )
Whoever eateth my flesh, and drinketh my blood, hath eternal life; and I will raise him up at the last day. (aiōnios )
55 Kwa maana mwili wangu ni chakula cha kweli na damu yangu ni kinywaji cha kweli.
For my flesh is food indeed, and my blood is drink indeed.
56 Yeyote alaye mwili wangu na kunywa damu yangu, atakaa ndani yangu nami nitakaa ndani yake.
He that eateth my flesh, and drinketh my blood, dwelleth in me, and I in him.
57 Kama vile Baba aliye hai alivyonituma mimi, na kama nami ninavyoishi kwa sababu ya Baba, hivyo anilaye mimi ataishi kwa sababu yangu.
As the living Father hath sent me, and I live by the Father: so he that eateth me, even he shall live by me.
58 Huu ndio mkate ushukao kutoka mbinguni, si kama ule mkate baba zenu waliokula nao wakafa. Lakini yeye aulaye mkate huu ataishi milele.” (aiōn )
This is that bread which came down from heaven: not as your fathers ate manna, and are dead: he that eateth of this bread shall live for ever. (aiōn )
59 Yesu alisema maneno haya alipokuwa akifundisha katika sinagogi huko Kapernaumu.
These things he said in the synagogue, as he taught in Capernaum.
60 Wengi wa wafuasi wake waliposikia jambo hili wakasema, “Mafundisho haya ni magumu. Ni nani awezaye kuyapokea?”
Many therefore of his disciples, when they had heard [this], said, This is a hard saying; who can hear it?
61 Yesu alipojua kwamba wafuasi wake wananungʼunika kuhusu mafundisho yake, akawaambia, “Je, jambo hili limewaudhi?
When Jesus knew in himself that his disciples murmured at it, he said to them, Doth this offend you?
62 Ingekuwaje basi kama mngemwona Mwana wa Adamu akipaa kwenda zake huko alipokuwa kwanza?
[What] if ye shall see the Son of man ascend up where he was before?
63 Roho ndiye atiaye uzima, mwili haufai kitu. Maneno haya niliyowaambia ni Roho tena ni uzima.
It is the spirit that reviveth; the flesh profiteth nothing: the words that I speak to you, [they] are spirit, and [they] are life.
64 Lakini baadhi yenu hamwamini.” Kwa maana Yesu alifahamu tangu mwanzo wale ambao hawangemwamini miongoni mwao na yule ambaye angemsaliti.
But there are some of you that believe not. For Jesus knew from the beginning who they were that believed not, and who he was that would betray him.
65 Akaendelea kusema, “Hii ndiyo sababu niliwaambia kwamba hakuna mtu awezaye kuja kwangu isipokuwa amejaliwa na Baba yangu.”
And he said, Therefore I said to you, that no man can come to me, except it were given to him by my Father.
66 Tangu wakati huo wafuasi wake wengi wakarejea nyuma wakaacha kumfuata.
From that [time] many of his disciples went back, and walked no more with him.
67 Hivyo Yesu akawauliza wale wanafunzi wake kumi na wawili, “Je, ninyi pia mnataka kuondoka?”
Then said Jesus to the twelve, Will ye also go away?
68 Simoni Petro akamjibu, “Bwana, tuondoke twende kwa nani? Wewe unayo maneno ya uzima wa milele. (aiōnios )
Then Simon Peter answered him, Lord, to whom shall we go? thou hast the words of eternal life. (aiōnios )
69 Tunaamini na kujua kuwa wewe ndiwe Aliye Mtakatifu wa Mungu.”
And we believe, and are sure that thou art that Christ, the Son of the living God.
70 Ndipo Yesu akajibu, “Je, sikuwachagua ninyi kumi na wawili? Lakini mmoja wenu ni ibilisi.”
Jesus answered them, Have not I chosen you twelve, and one of you is a devil?
71 (Hapa alikuwa anasema juu ya Yuda, mwana wa Simoni Iskariote. Ingawa alikuwa mmoja wa wale kumi na wawili, ndiye ambaye baadaye angemsaliti Yesu.)
He spoke of Judas Iscariot [the son] of Simon: for it was he that was to betray him, being one of the twelve.