< Yohana 21 >

1 Baada ya haya Yesu akawatokea tena wanafunzi wake kando ya Bahari ya Tiberia. Yeye alijionyesha kwao hivi:
Baada ya makowe ago Yesu atikuidhihirisha kae kwa anapunzi bake mu'Bahari ya Tiberia; ayee nga aidhihirisha mwene:
2 Simoni Petro, Tomaso aitwaye Didimasi, yaani Pacha, Nathanaeli wa Kana ya Galilaya, wana wa Zebedayo na wanafunzi wengine wawili walikuwa pamoja.
Simoni Petro abile pamope ni Thomaso ywakemelwa Didimas, Nathanieli kana ya Galilaya, bana ba Zebedayo ni anapunzi wenge abele ba Yesu.
3 Simoni Petro akawaambia wenzake, “Mimi naenda kuvua samaki.” Nao wakamwambia, “Tutakwenda pamoja nawe.” Wakatoka, wakaingia ndani ya mashua, lakini usiku ule hawakupata chochote.
Simoni Petro kaabakiya, “Nenga niyenda kuvua omba.” Nabo kabammakiya, “Twenga, lae twayenda ni wenga.” Kabayenda ni kujingya mu'ngalaba, lakini kilo chee boti bapatike kwaa chochote,
4 Mara baada ya kupambazuka, Yesu akasimama ufuoni, lakini wanafunzi hawakumtambua kwamba alikuwa Yesu.
Bwamba paakite, Yesu ayemite ufukweni, nabo anapunzi batangite kwaa kuwa abile Yesu.
5 Yesu akawaambia, “Wanangu, je, mna samaki wowote?” Wakamjibu, “La.”
Boka po Yesu kaabakiya”Ainja, mwabile ni chochote chakulya?” Ni bembe kanyangwa, “Hapana.”
6 Akawaambia, “Shusheni nyavu upande wa kuume wa mashua yenu nanyi mtapata samaki.” Wakashusha nyavu na tazama wakapata samaki wengi mno hata wakashindwa kuvutia zile nyavu zilizojaa samaki ndani ya mashua.
Kaabakiya, “Muuluye wavu upande wa kummalyo wa ngalaba, ni mwenga mwalowa pata kiasi.' Kwa eyo kabauluya wavu ni bembe aweza kwaa kulivuta kae kwa kuwa yabile ni omba wanyansima.
7 Yule mwanafunzi aliyependwa na Yesu akamwambia Petro, “Huyu ni Bwana!” Simoni Petro aliposikia haya, akajifunga nguo yake kwa kuwa alikuwa uchi, naye akajitosa baharini.
Bai yolo mwanapunzi ywabile ampendile Yesu kammakiya Petro, “Ni Ngwana.” Ni ywembe Simoni Petro paayowine kuwa ni Ngwana, kaitaba nganju yake(maana abile awala kwaa inoite), Boka po kaitosa mubahari.
8 Wale wanafunzi wengine wakaja kwa ile mashua huku wakikokota ule wavu uliyojaa samaki, maana hawakuwa mbali na nchi kavu, ilikuwa yapata dhiraa 200
Balo anapunzi bake baisa mu'ngalaba (mana babile kwaa kutalu ni pwani, yapata mita mia jimo boka ufukweni), ni bembe babile bakivuta nyavu zabile zitopii omba.
9 Walipofika ufuoni, wakaona moto wa makaa na samaki wakiokwa juu yake na mikate.
Paikite ufukweni, babweni mwoto wa mkala palo nnani yake pabile ni samaki mpamo ni nkate.
10 Yesu akawaambia, “Leteni baadhi ya hao samaki mliovua sasa hivi.”
Yesu kaamakiya, “Munnete baadhi ya omba mwamuapatike nambeambe.”
11 Simoni Petro akapanda kwenye mashua na kuukokota ule wavu pwani. Ulikuwa umejaa samaki wakubwa 153. Ingawa samaki walikuwa wengi kiasi hicho, ule wavu haukuchanika.
Bai Simoni Petro atipanda ni kuutola wavu waubile utopii omba akolo, kiasi cha omba 153; japo babile banyansima, ila wavu upapwanike kwaa.
12 Yesu akawaambia, “Njooni mpate kifungua kinywa.” Hakuna hata mmoja wa wanafunzi aliyethubutu kumuuliza, “Wewe ni nani?” Kwa sababu walijua ya kuwa ni Bwana.
Yesu kaamakiya, “Muiche mpate kipungwa nkanwa.” Ntopo hata yumo wa anapunzi bake ywathubutu kunnaluya, “Wenga wa nyai?” Batangite kuwa abile Ngwana.
13 Yesu akaja, akachukua ule mkate, akawapa na vivyo hivyo akawagawia pia wale samaki.
Yesu kaisa, katola wolo nkate, ni kuapeya, apangite nyonyonyo ni kwa balo omba.
14 Hii ilikuwa mara ya tatu Yesu kuwatokea wanafunzi wake baada yake kufufuliwa kutoka kwa wafu.
Ayee yaibile mara ya itatu kwa Yesu kuidhihirisha kwa anapunzi bake baada ya boka mu'kiwo.
15 Walipokwisha kula, Yesu akamuuliza Simoni Petro, “Je, Simoni mwana wa Yohana, unanipenda kweli kuliko hawa?” Yeye akamjibu, “Ndiyo Bwana, wewe unajua ya kuwa ninakupenda.” Yesu akamwambia, “Lisha wana-kondoo wangu.”
Baada ya kuwa batabilwe mikanwa yabe, Yesu kammakiya Simoni Petro, “Simoni mwana wa Yohana je, wanipenda nenga kuliko aba?” Petro kayangwa, “Eloo, Ngwana; Wenga utangite kuwa nenga nakupenga.” Yesu kammakiya, “Balishe wana ngondolo wango.”
16 Yesu akamwambia tena, “Simoni, mwana wa Yohana, wanipenda?” Petro akamjibu, “Ndiyo Bwana, wewe unajua ya kuwa ninakupenda.” Yesu akamwambia, “Chunga kondoo zangu.”
Kamakiya mara ya ibele, “Simoni mwana wa Yona, je wanipenda?” Petro kammakiya, “Eloo, Ngwana; wenga utangite kuwa nakupenda.” Yesu kammakiya, “Sunga ngondolo wango.”
17 Kwa mara ya tatu Yesu akamuuliza Petro, “Simoni mwana wa Yohana, unanipenda?” Petro akahuzunika sana kwa kuwa Yesu alimuuliza mara ya tatu, “Unanipenda?” Akamjibu, “Bwana, wewe unajua yote, unajua ya kuwa ninakupenda.” Yesu akamwambia, “Lisha kondoo wangu.
Kamakiya kae mara ye itatu, “Simoni mwana wa Yohana, je wanipenda?” Ni ywembe Petro atihuzunika kwa yaammakiye mara ya itatu, “Je wenga wanipenda? Ni ywembe kammakiya, Wenga utangite yote; utangite kuwa nakupenda.”Yesu kammakiya. Ubalishe ngondolo bango.
18 Amin, amin nakuambia, ulipokuwa kijana ulivaa na kwenda unakotaka, lakini utakapokuwa mzee utanyoosha mikono yako na mtu mwingine atakuvika na kukupeleka usipotaka kwenda.”
Amini amini nakubakiya, paubile muinja ulizoea kuwala ngobo mwene na kuyenda kokote paupala yenda; lakini mana ubile mpindo, walowa nyoosha maboko gako, ni ywenge alowa kukuwalisha ngobo ni kukupeleka upalike kwaa kuyenda.”
19 Yesu alisema haya ili kuashiria ni kifo cha aina gani Petro atakachomtukuza nacho Mungu. Kisha Yesu akamwambia Petro, “Nifuate!”
Yesu kabaya nyoo ili kubonekeya ni aina gani ya kiwo ambacho Petro alowa kumtukuza Nnongo. Baada ya kugabaya ago, ammakiye Petro, “Nikengame.”
20 Petro akageuka, akamwona yule mwanafunzi aliyependwa na Yesu akiwafuata. (Huyu ndiye yule mwanafunzi aliyeegama kifuani mwa Yesu walipokula naye chakula cha mwisho na kuuliza, “Bwana, ni nani atakayekusaliti?”)
Petro atikelebuka ni amweni yolo mwanapunzi ywapendilwe ni Yesu atikubakengama-Ayoo nga abile atikuiegemeza mu'kifua sa Yesu wakati wa chakulya cha kitamwinyo ni kunnaluya, “Ngwana, ywa nyai ywapala kukusaliti?
21 Petro alipomwona huyo mwanafunzi, akamuuliza Yesu, “Bwana na huyu je?”
Petro amweni ni kunnaluya Yesu, Ngwana ayoo mundu apanga namani?
22 Yesu akamjibu, “Ikiwa nataka aishi mpaka nitakaporudi, inakuhusu nini? Wewe inakupasa unifuate!”
Yesu kanyangwa”Mana nipala abaki mpaka paniisile, lyakuhusu namani?” Nikengame.”
23 Kwa sababu ya maneno haya ya Yesu, uvumi ukaenea miongoni mwa ndugu kwamba huyu mwanafunzi hangekufa. Lakini Yesu hakusema kuwa hangekufa. Yeye alisema tu kwamba, “Ikiwa nataka aishi mpaka nitakaporudi, inakuhusu nini?”
Kwa eyo habari yee ibayilwe nkati ya balo alongo, kuwa mwanapunzi yoo awaa kwaa. Lakini Yesu ammakiya kwaa Petro kuwa mwanapunzi yoo awaa kwaa, “Kati nipala ywembe atame mpaka paniisile yakuhusu namani?”
24 Huyu ndiye yule mwanafunzi anayeshuhudia mambo haya na ndiye ambaye ameandika habari hizi. Nasi tunajua ya kuwa ushuhuda wake ni kweli.
Ayee nga mwanapunzi ywatoa ushuhuda wa makowe agna nga ywaa aandikile makowe aga, ni tutangite kuwa ushuhuda wake ni kweli,
25 Lakini kuna mambo mengine mengi ambayo Yesu alifanya. Kama yote yangeliandikwa, nadhani hata ulimwengu wote usingekuwa na nafasi ya kutosha kuweka vitabu vyote ambavyo vingeandikwa. Amen.
Kwabile ni makowe yenge yanansima yaapangite Yesu. Kati kila limo mana liandikilwe, ulimwengu wote utosha kwaa kuibeka vitabu vya viandikilwe makowe gake.

< Yohana 21 >