< Joeli 3 >
1 “Katika siku hizo na wakati huo, nitakaporejesha neema ya Yuda na Yerusalemu,
Tazama, katika siku hizo na wakati huo, nitakaporudi mateka wa Yuda na Yerusalemu,
2 nitayakusanya mataifa yote na kuyaleta katika Bonde la Yehoshafati Hapo nitaingia kwenye hukumu dhidi yao kuhusu urithi wangu, watu wangu Israeli, kwa kuwa waliwatawanya watu wangu miongoni mwa mataifa na kuigawa nchi yangu.
Nami nitakusanya mataifa yote, na kuwaleta mpaka bonde la Yehoshafati. Nitawahukumu huko, kwa sababu ya watu wangu na warithi wangu Israeli, ambao waliwatawanya kati ya mataifa, na kwa sababu waligawanya nchi yangu.
3 Wanawapigia kura watu wangu na kuwauza wavulana ili kupata makahaba; waliwauza wasichana ili wapate kunywa mvinyo.
Wamepiga kura kwa ajili ya watu wangu, walinunua kijana kwa ajili ya kahaba, kuuza msichana kwa divai ili waweze kunywa.
4 “Sasa una nini dhidi yangu, ee Tiro na Sidoni, nanyi nchi zote za Ufilisti? Je, mnanilipiza kwa yale niliyoyafanya? Kama mnalipa, mimi nitalipiza juu ya vichwa vyenu kwa kasi na kwa haraka yale mliyoyatenda.
Sasa, kwa nini unanikasirikia, Tiro, Sidoni na mikoa yote ya Wafilisti? Je! mutanirudishia malipo? Hata kama mutanilipa, mara moja nitawarudishia malipo yenu juu ya vichwa vyenu wenyewe.
5 Kwa kuwa mlichukua fedha na dhahabu yangu pia mkabeba hazina zangu nzuri sana mkapeleka kwenye mahekalu yenu.
Kwa maana mumechukua fedha zangu na dhahabu zangu, nanyi mukachukua hazina zangu za thamani na kuzileta katika hekalu zenu.
6 Mliwauza watu wa Yuda na Yerusalemu kwa Wayunani, ili kwamba mpate kuwapeleka mbali na nchi yao.
Mumewauza watu wa Yuda na Yerusalemu kwa Wayunani, ili kuwaondoa mbali na maeneo yao.
7 “Tazama nitawaamsha kutoka zile sehemu mlizowauza, nami nitawalipiza juu ya vichwa vyenu kile mlichofanya.
Tazama, nitawaamsha, watoke mahali ambako muliwauza, na nitawarudishia malipo juu ya vichwa vyenu wenyewe.
8 Nitawauza wana wenu na binti zenu kwa watu wa Yuda, nao watawauza kwa Waseba, taifa lililo mbali.” Bwana amesema.
Nitawauza wana wako na binti zako, kwa mkono wa watu wa Yuda. Wao watawauza Sheba, kwa taifa mbali. Kwa maana Bwana amesema.
9 Tangazeni hili miongoni mwa mataifa: Jiandaeni kwa vita! Amsha askari! Wanaume wote wapiganaji wasogee karibu na kushambulia.
Tangaza hii kati ya mataifa, 'Jitayarisheni wenyewe kwa ajili ya vita, waamsheni mashujaa, waacheni wakaribie, mashujaa wote wa vita wapande juu.
10 Majembe yenu yafueni yawe panga na miundu yenu ya kukatia iwe mikuki. Aliye dhaifu na aseme, “Mimi nina nguvu!”
Yafueni majembe yenu kuwa panga na visu vyenu vya kuchongea kuwa mikuki. Basi wadhaifu waseme, 'Nina nguvu.'
11 Njooni haraka, ninyi mataifa yote kutoka pande zote, kusanyikeni huko. Shusha wapiganaji wako, Ee Bwana!
Haraka na mje, mataifa yote ya karibu, jikusanyeni pamoja huko. Ee Bwana, washushe mashujaa wako.
12 “Mataifa na yaamshwe; na yasonge mbele kuelekea Bonde la Yehoshafati, kwa kuwa nitaketi mahali pale kuhukumu mataifa yote yaliyoko kila upande.
Naam, mataifa yajihimize yenyewe kuja hadi bonde la Yehoshafati. Kwa maana nitakaa huko kuhukumu mataifa yote ya jirani.
13 Tia mundu, kwa kuwa mavuno yamekomaa. Njooni, mkanyage zabibu, kwa kuwa shinikizo la kukamua zabibu limejaa na mapipa yanafurika: kwa kuwa uovu wao ni mkubwa!”
Wekeni katiki mundu, kwa maana mavuno yameiva. Njoo, muponde zabibu, kwa ajiri pipa la divai limejaa. Vipuri vilivyofurika, kwa sababu uovu wao ni mkubwa sana.
14 Umati mkubwa, umati mkubwa katika bonde la uamuzi! Kwa kuwa siku ya Bwana ni karibu katika bonde la uamuzi.
Kuna mshtuko, mshtuko katika bonde la Hukumu. Kwa maana siku ya Bwana i karibu katika bonde la hukumu.
15 Jua na mwezi vitatiwa giza, na nyota hazitatoa mwanga wake tena.
Jua na mwezi vinakuwa giza, nyota zimeacha kuangaza.
16 Bwana atanguruma kutoka Sayuni na mshindo wa ngurumo kutoka Yerusalemu; dunia na mbingu vitatikisika. Lakini Bwana atakuwa kimbilio la watu wake, ngome imara kwa ajili ya watu wa Israeli.
Bwana ataunguruma kutoka Sayuni, na kuinua sauti yake kutoka Yerusalemu. Mbingu na nchi zitatikisika, lakini Bwana atakuwa makao kwa ajili ya watu wake, na ngome kwa wana wa Israeli.
17 “Ndipo mtakapojua kwamba Mimi, Bwana Mungu wenu, nakaa Sayuni, mlima wangu mtakatifu. Yerusalemu utakuwa mtakatifu; kamwe wageni hawatavamia tena.
Kwa hiyo mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana, Mungu wenu, anayeishi Sayuni, mlima wangu mtakatifu. Kisha Yerusalemu itakuwa takatifu, na hakuna jeshi litaklozunguka tena.
18 “Katika siku hiyo milima itadondosha divai mpya, na vilima vitatiririka maziwa; mabonde yote ya Yuda yatatiririka maji. Chemchemi itatiririka kutoka kwenye nyumba ya Bwana na kunywesha Bonde la Shitimu.
Katika siku hiyo, milima itatayarisha divai nzuri, milima itatiririsha maziwa, miito yote ya Yuda itapita katikati ya maji, na chemchemi zitakuja kutoka nyumba ya Bwana na maji ya bonde la Shitimu.
19 Lakini Misri itakuwa ukiwa, Edomu itakuwa jangwa tupu, kwa sababu ya jeuri waliofanya kwa watu wa Yuda, ambao katika nchi yao walimwaga damu isiyo na hatia.
Misri itakuwa ukiwa, na Edomu itakuwa jangwa tupu, kwa sababu ya vurugu iliyofanyika kwa watu wa Yuda, kwa sababu walimwaga damu isiyo na hatia katika nchi yao.
20 Yuda itakaliwa na watu milele na Yerusalemu itadumu vizazi vyote.
Lakini Yuda utakua mwenyeji milele, na Yerusalemu itakuwa kizazi hata kizazi.
21 Hatia yao ya damu, ambayo sijasamehe, nitasamehe.”
Nitawalipizia damu yao, ambayo sijajilipizia kisasi, kwa maana Bwana anaishi Sayuni.