< Joeli 1 >

1 Neno la Bwana ambalo lilimjia Yoeli mwana wa Pethueli.
Hili ni neno la Bwana lililomjia Yoeli mwana wa Pethueli.
2 Sikilizeni hili, enyi wazee; sikilizeni, ninyi nyote mnaoishi katika nchi. Je, jambo kama hili lilishawahi kutokea katika siku zenu au katika siku za babu zenu?
Sikieni haya, ninyi wazee, na sikieni, ninyi wenyeji wa nchi. Je! Hii imewahi kuwa kabla ya siku zenu au katika siku za baba zenu?
3 Waelezeni watoto wenu, na watoto wenu wawaambie watoto wao, na watoto wao kwa kizazi kitakachofuata.
Waambie watoto wako kuhusu hilo, na waache watoto wako kuwaambie watoto wao, na watoto wao kizazi kijacho.
4 Kilichosazwa na kundi la tunutu nzige wakubwa wamekula, kilichosazwa na nzige wakubwa parare wamekula, kilichosazwa na parare madumadu wamekula.
Yale yaliyosazwa na tunutu yameliwa na nzige wakubwa; yale yaliyosazwa na nzige panzi wameyala; na yaliyosazwa na panzi yameliwa na madumadu
5 Amkeni, enyi walevi, mlie! Pigeni yowe enyi wanywaji wote wa mvinyo, pigeni yowe kwa sababu ya mvinyo mpya, kwa kuwa mmenyangʼanywa kutoka midomoni mwenu.
Amkeni, enyi walevi, lieni! Omboleza, ninyi nyote mnywao divai, kwa sababu divai nzuri imekatwa kutoka kwenu.
6 Taifa limevamia nchi yangu, lenye nguvu tena lisilo na idadi; lina meno ya simba, magego ya simba jike.
Kwa maana taifa limekuja juu ya nchi yangu, imara na bila idadi. Meno yake ni meno ya simba, neye ana meno ya simba.
7 Limeharibu mizabibu yangu na kuangamiza mitini yangu. Limebambua magome yake na kuyatupilia mbali, likayaacha matawi yake yakiwa meupe.
Amelifanya shamba langu la mizabibu kuwa mahali pa kutisha, amechukua mtini wangu. Amechukua gome lake na kulitupa mbali; matawi yake yamekuwa meupe.
8 Omboleza kama bikira aliyevaa nguo ya gunia anayehuzunika kwa ajili ya mume wa ujana wake.
Omboleza kama bikira aliyevaa magunia kwa kifo cha mumewe mdogo.
9 Sadaka za nafaka na sadaka za kinywaji zimekatiliwa mbali kutoka nyumba ya Bwana. Makuhani wanaomboleza, wale wanaohudumu mbele za Bwana.
Sadaka ya unga na sadaka ya kinywaji zimekatiliwa mbali na nyumba ya Bwana. Makuhani, watumishi wa Bwana, huomboleza.
10 Mashamba yameharibiwa, ardhi imekauka; nafaka imeharibiwa, mvinyo mpya umekauka, mafuta yamekoma.
Mashamba yameharibiwa, na nchi imekuwa dhaifu. Kwa maana nafaka imeharibiwa, divai mpya imekauka, na mafuta yameharibiwa.
11 Kateni tamaa, enyi wakulima, lieni, enyi mlimao mizabibu; huzunikeni kwa ajili ya ngano na shayiri, kwa sababu mavuno ya shambani yameharibiwa.
Oneni aibu, enyi wakulima, lieni, wakulima wa mzabibu, kwa ngano na shayiri. Kwa mavuno ya mashamba yameharibika.
12 Mzabibu umekauka na mtini umenyauka; mkomamanga, mtende na mtofaa, miti yote shambani, imekauka. Hakika furaha yote ya mwanadamu imeondoka.
Mizabibu imeharibika na miti ya mtini imekauka, miti ya mkomamanga, pia mitende, na miti ya epo - miti yote ya shambani imeharibika. Kwa furaha imeharibika kutoka kwa wana wa wanadamu.
13 Vaeni nguo ya gunia, enyi makuhani, muomboleze; pigeni yowe, enyi mnaohudumu madhabahuni. Njooni, vaeni nguo ya gunia usiku kucha, enyi mnaohudumu mbele za Mungu wangu; kwa kuwa sadaka za nafaka na sadaka za kinywaji zimezuiliwa kufika katika nyumba ya Mungu wenu.
Panda magunia na omboleza, enyi makuhani! Mwalia, enyi watumishi wa madhabahu. Njoo, ulala usiku wote kwenye magunia, enyi watumishi wa Mungu wangu. Maana sadaka ya unga na sadaka ya kinywaji zimezuiliwa nyumbani mwa Mungu wenu.
14 Tangazeni saumu takatifu; liiteni kusanyiko takatifu. Iteni wazee na wote waishio katika nchi waende katika nyumba ya Bwana Mungu wenu, wakamlilie Bwana.
Iteni kwa funga takatifu, na iteni kusanyiko takatifu. Mkusanyieni wazee na wenyeji wote wa nchi wafike nyumbani kwa Bwana Mungu wenu, na kumlilia Bwana.
15 Ole kwa siku hiyo! Kwa kuwa siku ya Bwana iko karibu; itakuja kama uharibifu kutoka kwa Mwenyezi.
Ole kwa siku! Kwa maana siku ya Bwana imekaribia. Nayo itakuja uharibifu kutoka kwa Mwenyezi.
16 Je, chakula hakikukatiliwa mbali mbele ya macho yetu: furaha na shangwe kutoka nyumba ya Mungu wetu?
Je, chakula hakikukatiliwa mbali mbele ya macho yetu, na furaha na kicheko kutoka nyumbani mwa Mungu wetu?
17 Mbegu zinakauka chini ya mabonge ya udongo. Ghala zimeachwa katika uharibifu, ghala za nafaka zimebomolewa, kwa maana hakuna nafaka.
Mbegu zinaoza chini ya udongo wake, ghala zimekuwa ukiwa, na mabanda yamevunjika, kwa maana nafaka imeharibika.
18 Jinsi gani ngʼombe wanavyolia! Makundi ya mifugo yanahangaika kwa sababu hawana malisho; hata makundi ya kondoo yanateseka.
Jinsi wanyama hulia! Ng'ombe wa ngome wanateseka kwa sababu hawana malisho. Pia, makundi ya kondoo yanateseka.
19 Kwako, Ee Bwana, naita, kwa kuwa moto umeteketeza malisho ya mbugani na miali ya moto imeunguza miti yote shambani.
Bwana, nakulilia wewe. Kwa maana moto umekula malisho ya jangwani, na moto umeteketeza miti yote ya mashamba.
20 Hata wanyama wa porini wanakuonea shauku; vijito vya maji vimekauka, na moto umeteketeza malisho yote ya mbugani.
Hata wanyama wa mashambani wanapanda kwa ajili yako, kwa maana mito ya maji imekauka, na moto umekula malisho ya jangwani.

< Joeli 1 >