< Ayubu 6 >
Kisha Ayubu akajibu na kusema,
2 “Laiti uchungu wangu ungeweza kupimwa, nayo taabu yangu yote ingewekwa kwenye mizani!
“Oo, laiti maumivu yangu makubwa yangepimwa; laiti misiba yangu yote mikubwa ingewekwa kwenye mizani!
3 Kwa kuwa hakika ingekuwa nzito kuliko mchanga wa bahari zote, kwa hiyo si ajabu maneno yangu yamekuwa ya haraka.
Kwa kuwa sasa ungekuwa mzito kuliko mchanga wa baharini. Kwa sababu hiyo maneno yangu yamekuwa ya haraka.
4 Mishale ya Mwenyezi iko ndani yangu, roho yangu inakunywa sumu yake; vitisho vya Mungu vimejipanga dhidi yangu.
Kwa kuwa mishale ya Mwenyezi ipo ndani yangu, moyo wangu umelewa sumu; Vitisho vya Mungu vimejipanga vyenyewe dhidi yangu.
5 Je, punda-mwitu hulia akiwa na majani, au ngʼombe dume hulia akiwa na chakula?
Je punda mwitu hulia akiwa na malisho? Au ng'ombe huwa dhaifu wakati wa njaa ambapo anachakula?
6 Je, chakula kisicho na ladha huliwa bila chumvi, au upo utamu katika ute mweupe wa yai?
Je inawezekana kitu kisicho na ladha kulika bila chumvi? Au kuna radha yoyote katika ute mweupe wa yai?
7 Ninakataa kuvigusa; vyakula vya aina hii hunichukiza.
Nakataa kuvigusa; kwangu mimi vinafanana na chakula kichukizacho.
8 “Laiti ningepata haja yangu, kwamba Mungu angenijalia hilo nililotarajia,
Oo, kama nigeweza kupata haja yangu; oo, kama Mungu angeridhia jambo nilitamanilo sana:
9 kwamba Mungu angekuwa radhi kuniponda, kuuachia mkono wake na kunikatilia mbali!
kama Mungu ingempendeza kuniangamiza mara moja, kwamba angeulegeza mkono wake na kuyakatilia mbali maisha yangu!
10 Ndipo bado ningekuwa na hii faraja, furaha yangu katika maumivu makali: kwamba sikuwa nimeyakana maneno yake yeye Aliye Mtakatifu.
Hii ingeweza kuwa faraja yangu hata sasa - hata kama nafurahia sana maumivu yasiyopungua: kwa kuwa sikuyakana maneno yake Mtakatifu.
11 “Ninazo nguvu gani, hata niendelee kutumaini? Matazamio yangu ya mbele ni nini, hata niendelee kuwa mvumilivu?
Nguvu yangu ni ipi, hata nijaribu kusubiri? Mwisho wangu ni upi, utakao refusha maisha yangu?
12 Je, mimi nina nguvu za jiwe? Je, mwili wangu ni shaba?
Je nguvu zangu ni nguvu za mawe? Au mwili wangu umeumbwa kwa shaba nyeusi?
13 Je, ninao uwezo wowote wa kujisaidia mimi mwenyewe, wakati ambapo mafanikio yamefukuziwa mbali nami?
Je si kweli kwamba sina msaada ndani yangu, na kwamba hekima imeondolewa mbali nami?
14 “Mtu anayekata tamaa angetazamia moyo wa kujitoa wa rafiki zake, hata kama akiacha uchaji wa Mwenyezi.
Kwa mtu ambaye yu karibu kuzirai, inapasa uaminifu uonyeshwe na rafiki zake; hata kwake yeye aachaye kumcha Mwenyezi.
15 Lakini ndugu zangu sio wa kutegemewa, ni kama vijito vya msimu, ni kama vijito ambavyo hufurika
Lakini ndugu zangu wamekuwa waaminifu kwangu kama mkondo wa maji jangwani, mfano wa mifereji ya maji ipitayo mpaka pasipo kitu,
16 wakati vimefunikwa barafu iyeyukayo, ambavyo hujazwa na theluji inayoyeyuka,
ambayo imekuwa mieusi kwa sababu ya barafu juu yake, na kwa sababu ya theluji ambayo hujificha yenyewe ndani yake.
17 lakini hukauka majira ya ukame, na wakati wa hari hutoweka katika mikondo yake.
Wakati zikiyeyuka, hutoweka; kukiwa na joto, hutoweka mahali hapo.
18 Misafara hugeuka kutoka njia zake; hukwea kwenda kwenye nchi ya ukiwa na kuangamia.
Misafara ambayo husafiri kwa njia yao hugeuka na maji; huzurura jangwani na kisha hupotea.
19 Misafara ya Tema inatafuta maji, wafanyabiashara wa Sheba wanaosafiri hutazama kwa matarajio.
Misafara kutoka Tema huitazama, wakati majeshi ya Sheba huitarajia.
20 Wamedhikika, kwa sababu walikuwa na matumaini; wanafika huko, lakini wanahuzunika kwa kukosa walichotarajia.
Wamevunjika moyo kwa sababu walitumaini kupata maji. Wakaenda huko, lakini walidanganywa.
21 Sasa nanyi mmethibitika kwamba hamna msaada wowote; mnaona jambo la kutisha, nanyi mnaogopa.
Kwa sasa ninyi rafiki si kitu kwangu; mmeona hali yangu ya kutisha nanyi mwaogopa.
22 Je, nimewahi kusema, ‘Toeni kitu kwa ajili yangu, au mnilipie fidia kutoka mali zenu,
Je nilisema kwenu, 'Nipeni kitu furani?' Au, 'nitoleeni zawadi katika mali zenu?'
23 au niokoeni mikononi mwa adui, au nikomboeni kutoka makucha ya wasio na huruma’?
Au, 'Niokoeni toka mkononi mwa mtesi wangu?' Au, 'Nitoleeni fidia kwa watesi wangu?'
24 “Nifundisheni, nami nitanyamaza kimya; nionyesheni nilikokosea.
Nifundishe, nami nitaishika amani yangu; nifanye nifahamu wapi nilipokosea.
25 Tazama yalivyo ya kuumiza maneno ya kweli! Lakini mabishano yenu yanathibitisha nini?
Jinsi gani maneno ya kweli yanavyo umiza! Lakini hoja zenu, jee hasa zimenionya nini mimi?
26 Je, mna maana ya kuyasahihisha ninayosema, na kuyafanya maneno ya mtu anayekata tamaa kama upepo?
Je mnapanga kuyakemea maneno yangu, mnayachukulia maneno ya mtu mwenye kukata tamaa sawa na upepo?
27 Mngeweza hata kupiga kura kwa ajili ya yatima, na kubadilishana rafiki yenu na mali.
Hasa, mna piga kura kwa ajili ya yatima, na kupatana bei juu ya rafiki yenu kama bidhaa.
28 “Lakini sasa kuweni na huruma mkaniangalie mimi. Je, ningeweza kusema uongo mbele zenu?
Sasa, kwa sababu hiyo, tafadhari nitazame, kwa hakika sitasema uongo usoni penu.
29 Tulizeni hasira, msiwe wadhalimu; angalieni tena, kwa maana nimehatarisha uadilifu wangu.
Rudini, nawasihi; lisiwepo neno la uonevu na nyinyi; Hasa, rudini, sababu zangu ni za haki.
30 Je, pana uovu wowote midomoni mwangu? Je, kinywa changu hakiwezi kupambanua hila?
Je mna uovu ulimini mwangu? Je kinywa changu hakiwezi kungundua madhara?