< Ayubu 6 >

1 Kisha Ayubu akajibu:
ויען איוב ויאמר׃
2 “Laiti uchungu wangu ungeweza kupimwa, nayo taabu yangu yote ingewekwa kwenye mizani!
לו שקול ישקל כעשי והיתי במאזנים ישאו יחד׃
3 Kwa kuwa hakika ingekuwa nzito kuliko mchanga wa bahari zote, kwa hiyo si ajabu maneno yangu yamekuwa ya haraka.
כי עתה מחול ימים יכבד על כן דברי לעו׃
4 Mishale ya Mwenyezi iko ndani yangu, roho yangu inakunywa sumu yake; vitisho vya Mungu vimejipanga dhidi yangu.
כי חצי שדי עמדי אשר חמתם שתה רוחי בעותי אלוה יערכוני׃
5 Je, punda-mwitu hulia akiwa na majani, au ngʼombe dume hulia akiwa na chakula?
הינהק פרא עלי דשא אם יגעה שור על בלילו׃
6 Je, chakula kisicho na ladha huliwa bila chumvi, au upo utamu katika ute mweupe wa yai?
היאכל תפל מבלי מלח אם יש טעם בריר חלמות׃
7 Ninakataa kuvigusa; vyakula vya aina hii hunichukiza.
מאנה לנגוע נפשי המה כדוי לחמי׃
8 “Laiti ningepata haja yangu, kwamba Mungu angenijalia hilo nililotarajia,
מי יתן תבוא שאלתי ותקותי יתן אלוה׃
9 kwamba Mungu angekuwa radhi kuniponda, kuuachia mkono wake na kunikatilia mbali!
ויאל אלוה וידכאני יתר ידו ויבצעני׃
10 Ndipo bado ningekuwa na hii faraja, furaha yangu katika maumivu makali: kwamba sikuwa nimeyakana maneno yake yeye Aliye Mtakatifu.
ותהי עוד נחמתי ואסלדה בחילה לא יחמול כי לא כחדתי אמרי קדוש׃
11 “Ninazo nguvu gani, hata niendelee kutumaini? Matazamio yangu ya mbele ni nini, hata niendelee kuwa mvumilivu?
מה כחי כי איחל ומה קצי כי אאריך נפשי׃
12 Je, mimi nina nguvu za jiwe? Je, mwili wangu ni shaba?
אם כח אבנים כחי אם בשרי נחוש׃
13 Je, ninao uwezo wowote wa kujisaidia mimi mwenyewe, wakati ambapo mafanikio yamefukuziwa mbali nami?
האם אין עזרתי בי ותשיה נדחה ממני׃
14 “Mtu anayekata tamaa angetazamia moyo wa kujitoa wa rafiki zake, hata kama akiacha uchaji wa Mwenyezi.
למס מרעהו חסד ויראת שדי יעזוב׃
15 Lakini ndugu zangu sio wa kutegemewa, ni kama vijito vya msimu, ni kama vijito ambavyo hufurika
אחי בגדו כמו נחל כאפיק נחלים יעברו׃
16 wakati vimefunikwa barafu iyeyukayo, ambavyo hujazwa na theluji inayoyeyuka,
הקדרים מני קרח עלימו יתעלם שלג׃
17 lakini hukauka majira ya ukame, na wakati wa hari hutoweka katika mikondo yake.
בעת יזרבו נצמתו בחמו נדעכו ממקומם׃
18 Misafara hugeuka kutoka njia zake; hukwea kwenda kwenye nchi ya ukiwa na kuangamia.
ילפתו ארחות דרכם יעלו בתהו ויאבדו׃
19 Misafara ya Tema inatafuta maji, wafanyabiashara wa Sheba wanaosafiri hutazama kwa matarajio.
הביטו ארחות תמא הליכת שבא קוו למו׃
20 Wamedhikika, kwa sababu walikuwa na matumaini; wanafika huko, lakini wanahuzunika kwa kukosa walichotarajia.
בשו כי בטח באו עדיה ויחפרו׃
21 Sasa nanyi mmethibitika kwamba hamna msaada wowote; mnaona jambo la kutisha, nanyi mnaogopa.
כי עתה הייתם לא תראו חתת ותיראו׃
22 Je, nimewahi kusema, ‘Toeni kitu kwa ajili yangu, au mnilipie fidia kutoka mali zenu,
הכי אמרתי הבו לי ומכחכם שחדו בעדי׃
23 au niokoeni mikononi mwa adui, au nikomboeni kutoka makucha ya wasio na huruma’?
ומלטוני מיד צר ומיד עריצים תפדוני׃
24 “Nifundisheni, nami nitanyamaza kimya; nionyesheni nilikokosea.
הורוני ואני אחריש ומה שגיתי הבינו לי׃
25 Tazama yalivyo ya kuumiza maneno ya kweli! Lakini mabishano yenu yanathibitisha nini?
מה נמרצו אמרי ישר ומה יוכיח הוכח מכם׃
26 Je, mna maana ya kuyasahihisha ninayosema, na kuyafanya maneno ya mtu anayekata tamaa kama upepo?
הלהוכח מלים תחשבו ולרוח אמרי נאש׃
27 Mngeweza hata kupiga kura kwa ajili ya yatima, na kubadilishana rafiki yenu na mali.
אף על יתום תפילו ותכרו על ריעכם׃
28 “Lakini sasa kuweni na huruma mkaniangalie mimi. Je, ningeweza kusema uongo mbele zenu?
ועתה הואילו פנו בי ועל פניכם אם אכזב׃
29 Tulizeni hasira, msiwe wadhalimu; angalieni tena, kwa maana nimehatarisha uadilifu wangu.
שבו נא אל תהי עולה ושבי עוד צדקי בה׃
30 Je, pana uovu wowote midomoni mwangu? Je, kinywa changu hakiwezi kupambanua hila?
היש בלשוני עולה אם חכי לא יבין הוות׃

< Ayubu 6 >