< Ayubu 34 >

1 Kisha Elihu akasema:
ויען אליהוא ויאמר׃
2 “Sikieni maneno yangu, enyi watu wenye hekima; nisikilizeni mimi, ninyi watu wenye maarifa.
שמעו חכמים מלי וידעים האזינו לי׃
3 Kwa kuwa sikio huyajaribu maneno kama vile ulimi uonjavyo chakula.
כי אזן מלין תבחן וחך יטעם לאכל׃
4 Tujichagulie wenyewe yaliyo sawa, nasi tujifunze pamoja yaliyo mema.
משפט נבחרה לנו נדעה בינינו מה טוב׃
5 “Ayubu anasema, ‘Mimi sina hatia, lakini Mungu ameninyima haki yangu.
כי אמר איוב צדקתי ואל הסיר משפטי׃
6 Ingawa niko sawa, ninaonekana mwongo; nami ingawa sina kosa, kidonda changu hakiponi.’
על משפטי אכזב אנוש חצי בלי פשע׃
7 Ni mtu gani aliye kama Ayubu, anywaye dharau kama maji?
מי גבר כאיוב ישתה לעג כמים׃
8 Ashirikianaye na watenda mabaya na kuchangamana na watu waovu.
וארח לחברה עם פעלי און וללכת עם אנשי רשע׃
9 Kwa kuwa anasema, ‘Haimfaidi mwanadamu kitu chochote anapojitahidi kumpendeza Mungu.’
כי אמר לא יסכן גבר ברצתו עם אלהים׃
10 “Hivyo nisikilizeni mimi, ninyi watu wenye ufahamu. Kamwe Mungu hatendi uovu, Mwenyezi hafanyi kosa.
לכן אנשי לבב שמעו לי חללה לאל מרשע ושדי מעול׃
11 Humlipa mwanadamu kwa ajili ya lile alilotenda; huleta juu yake kile ambacho matendo yake yanastahili.
כי פעל אדם ישלם לו וכארח איש ימצאנו׃
12 Ni jambo lisiloweza kufikiriwa kwamba Mungu angefanya makosa, kwamba Mwenyezi angepotosha hukumu.
אף אמנם אל לא ירשיע ושדי לא יעות משפט׃
13 Je, ni nani aliyemtawaza juu ya dunia? Ni nani aliyemweka kuwa mwangalizi wa ulimwengu wote?
מי פקד עליו ארצה ומי שם תבל כלה׃
14 Kama lilikuwa kusudi la Mungu, naye akaiondoa Roho yake na pumzi yake,
אם ישים אליו לבו רוחו ונשמתו אליו יאסף׃
15 wanadamu wote wangeliangamia kwa pamoja, na mtu angerudi mavumbini.
יגוע כל בשר יחד ואדם על עפר ישוב׃
16 “Kama ninyi mnaufahamu, sikieni hili; sikilizeni hili nisemalo.
ואם בינה שמעה זאת האזינה לקול מלי׃
17 Je, yeye aichukiaye haki aweza kutawala? Je, utamhukumu mwenye haki, Aliye na Nguvu Zote?
האף שונא משפט יחבוש ואם צדיק כביר תרשיע׃
18 Je, si ni yeye awaambiaye wafalme, ‘Ninyi hamfai kitu,’ nao watu mashuhuri, ‘Ninyi ni waovu,’
האמר למלך בליעל רשע אל נדיבים׃
19 yeye asiyependelea wakuu, wala haonyeshi upendeleo kwa matajiri kuliko maskini, kwa kuwa wote ni kazi ya mikono yake?
אשר לא נשא פני שרים ולא נכר שוע לפני דל כי מעשה ידיו כלם׃
20 Wanakufa ghafula, usiku wa manane; watu wanatikiswa nao hupita; wenye nguvu huondolewa bila mkono wa mwanadamu.
רגע ימתו וחצות לילה יגעשו עם ויעברו ויסירו אביר לא ביד׃
21 “Macho yake yanazitazama njia za wanadamu; anaona kila hatua yao.
כי עיניו על דרכי איש וכל צעדיו יראה׃
22 Hakuna mahali penye giza nene, wala uvuli mkubwa, ambapo watenda mabaya wanaweza kujificha.
אין חשך ואין צלמות להסתר שם פעלי און׃
23 Mungu hana haja ya kumchunguza mtu sana, ili apate kuja mbele zake kwa hukumu.
כי לא על איש ישים עוד להלך אל אל במשפט׃
24 Bila kuuliza huwapondaponda wenye nguvu nyingi na kuwaweka wengine mahali pao.
ירע כבירים לא חקר ויעמד אחרים תחתם׃
25 Kwa sababu huyaangalia matendo yao yote, huwaondoa usiku, nao wakaangamia.
לכן יכיר מעבדיהם והפך לילה וידכאו׃
26 Anawaadhibu kwa ajili ya uovu wao mahali ambapo kila mmoja ataweza kuwaona,
תחת רשעים ספקם במקום ראים׃
27 kwa sababu wameacha kumfuata Mungu, nao hawakuiheshimu njia yake hata moja.
אשר על כן סרו מאחריו וכל דרכיו לא השכילו׃
28 Wamesababisha kilio cha maskini kifike mbele zake, hivyo akasikia kilio cha wahitaji.
להביא עליו צעקת דל וצעקת עניים ישמע׃
29 Lakini kama akinyamaza kimya, ni nani awezaye kumhukumu? Kama akiuficha uso wake, ni nani awezaye kumwona? Ikiwa ni taifa au mtu mmoja, kwake ni sawa,
והוא ישקט ומי ירשע ויסתר פנים ומי ישורנו ועל גוי ועל אדם יחד׃
30 ili kumzuia mtu mwovu kutawala, au wale ambao huwategea watu mitego.
ממלך אדם חנף ממקשי עם׃
31 “Kama mwanadamu akimwambia Mungu, ‘Nimekosa lakini sitatenda dhambi tena.
כי אל אל האמר נשאתי לא אחבל׃
32 Nifundishe nisichoweza kuona; kama nimekukosea, sitafanya hivyo tena.’
בלעדי אחזה אתה הרני אם עול פעלתי לא אסיף׃
33 Je basi, Mungu atakulipa kwa masharti yako, wakati wewe umekataa kutubu? Yakupasa wewe uamue, wala si mimi; sasa niambie lile ulijualo.
המעמך ישלמנה כי מאסת כי אתה תבחר ולא אני ומה ידעת דבר׃
34 “Wanadamu wenye ufahamu husema, wenye hekima wanaonisikia huniambia,
אנשי לבב יאמרו לי וגבר חכם שמע לי׃
35 ‘Ayubu huongea bila maarifa; maneno yake hayana busara.’
איוב לא בדעת ידבר ודבריו לא בהשכיל׃
36 Laiti Ayubu angejaribiwa hadi kikomo cha mwisho, kwa sababu anajibu kama mtu mwovu!
אבי יבחן איוב עד נצח על תשבת באנשי און׃
37 Kwenye dhambi yake huongeza uasi; kwa dharau hupiga makofi miongoni mwetu, na kuzidisha maneno yake dhidi ya Mungu.”
כי יסיף על חטאתו פשע בינינו יספוק וירב אמריו לאל׃

< Ayubu 34 >