< Ayubu 33 >

1 “Lakini Ayubu, sasa, sikiliza maneno yangu; zingatia kila kitu nitakachosema.
Kwahiyo sasa, nakuomba wewe, Ayubu, usikilize hotuba yangu; sikiliza maneno yangu yote.
2 Karibu nitafungua kinywa changu; maneno yangu yapo katika ncha ya ulimi wangu.
Tazama sasa, nimeufumbua mdomo wangu; ulimi wangu umesema maneno ndani ya mdomo wangu.
3 Maneno yangu yanatoka katika moyo mnyofu; midomo yangu hunena kwa uaminifu yale niyajuayo.
Maneno yangu yatasema uadilifu wa moyo wangu; yatasema kwa unyofu yale ambayo mdomo wangu unayajua.
4 Roho wa Mungu ameniumba; pumzi ya Mwenyezi hunipa uhai.
Roho ya Mungu imeniumba; pumzi ya Mwenye nguvu imenipatia uhai.
5 Unijibu basi, kama unaweza; jiandae kunikabili mimi.
Kama unaweza, nijibu; weka maneno yako katika mpangilio mbele yangu na kisha usimame.
6 Mimi ni kama wewe mbele za Mungu; mimi pia nimetolewa kwenye udongo.
Tazama, niko kama wewe ulivyo mbele za Mungu; nimeumbwa pia kutoka katika udongo.
7 Huna sababu ya kuniogopa, wala mkono wangu haupaswi kukulemea.
Ona, tishio langu halitakufanya wewe uogope; wala mzigo wangu hautakuwa mzito kwako.
8 “Lakini umesema nikiwa ninakusikia, nami nilisikia maneno yenyewe:
Umesema kwa hakika katika masikio yangu; nimeisikia sauti ya maneno yakeo yakisema,
9 ‘Mimi ni safi na sina dhambi; mimi ni safi na sina hatia.
'Mimi ni safi na bila hila; sina hatia, na hakuna dhambi ndani yangu.
10 Lakini bado Mungu amepata dosari kwangu, naye ananiona kama adui yake.
Tazama, Mungu huona nafasi za kunishambulia mimi; huniangalia mimi kama adui yake.
11 Ananifunga miguu kwa pingu, tena anaziangalia njia zangu zote kwa karibu.’
Huweka miguu yangu akiba; naye huangalia njia zangu zote.'
12 “Lakini mimi ninakuambia, katika jambo hili wewe una makosa, kwa maana Mungu ni mkuu kuliko mwanadamu.
Tazama, katika hili hauko sawa, nitakujibu, kwa kuwa Mungu ni mkuu kuliko mtu.
13 Kwa nini unamlalamikia kwamba yeye hamjibu mwanadamu?
Kwanini unashindana naye? Huwa hahesabu matendo yake yoyote.
14 Kwa kuwa Mungu husema, wakati huu kwa njia moja, au wakati mwingine kwa njia nyingine, ingawa mwanadamu anaweza asielewe.
Kwa kuwa Mungu huzungumza mara moja, naam, mara mbili, ingawa mwanadamu hawezi kutambua.
15 Mungu husema na mwanadamu katika ndoto, katika maono ya usiku, wakati usingizi mzito uwaangukiapo wanadamu wasinziapo vitandani mwao,
Katika ndoto, katika maono ya usiku, wakati usingizi mzito unapowapata watu, katika usingizi kitandani -
16 anaweza akasemea masikioni mwao, na kuwatia hofu kwa maonyo,
basi Mungu hufungua masikio ya watu, na kuwatisha kwa vitisho,
17 ili kumgeuza mtu kutoka kwenye kutenda mabaya na kumwepusha na kiburi,
kwa kusudi la kumvuta mtu atoke katika makusudio yake maovu, na kuyaweka majivuno mbali naye.
18 kuiokoa nafsi yake na shimo, uhai wake usiangamizwe kwa upanga.
Mungu huyaokoa maisha ya mwanadamu kutoka katika shimo, na uhai wake dhidi ya kifo.
19 Mtu anaweza kutiwa adabu kwa maumivu kitandani mwake, kwa dhiki za mfululizo katika mifupa yake,
Mtu huadhidibiwa pia na maumivu kitandani mwake, na maumivu makali yanayodumu katika mifupa yake,
20 kiasi kwamba maisha yake yenyewe yanakataa chakula nayo nafsi yake ikakichukia kabisa hata chakula kizuri.
ili kwamba maisha yake yachukie chakula, na roho yake ichukie vyakula vizuri.
21 Nyama ya mwili wake huisha kwa kukonda, nayo mifupa yake ambayo mwanzoni ilikuwa imefichika, sasa inatokeza nje.
Nyama yake imeharibiwa ili kwamba usionekane; mifupa yake, mara moja isionekane, sasa basi ng'ang'ania.
22 Nafsi yake inakaribia kaburi, nao uhai wake karibu na wajumbe wa kifo.
Hakika, roho yake inasogea shimoni, na uhai wake unasogea kwa wale wanaotaka kuuharibu.
23 “Kama bado kuna malaika upande wake kama mtetezi, mmoja miongoni mwa elfu, wa kumwambia mwanadamu lililo jema kwake,
Lakini kama kuna malaika anayeweza kuwa mpatanishi kwa ajili yake, mpatanishi mmoja miongoni mwa maelfu ya malaika, kumwonesha kile kilicho cha haki ili atende haki,
24 kumwonea huruma na kusema, ‘Mwokoe asije akatumbukia shimoni; nimepata ukombozi kwa ajili yake’:
na kama malaika ni mpole kwake na kumwambia Mungu, 'Mwokoe mtu huyu ili asishuke chini shimoni; nimepata fidia kwa ajili yake,'
25 ndipo nyama ya mwili wake hufanywa mpya kama ya mtoto; hurudishwa upya kama siku za ujana wake.
kisha mwili wake utakuwa mororo kuliko mwili wa mtoto, atazirudia siku za nguvu za ujana wake.
26 Humwomba Mungu, akapata kibali kwake, huuona uso wa Mungu na kushangilia kwa furaha; Mungu humrudisha katika hali yake ya uadilifu.
Atamwomba Mungu, na Mungu atakuwa mwema kwake, ili kwamba auone uso wa Mungu akiwa mwenye furaha. Mungu atampa mtu ushindi wake.
27 Ndipo huja mbele za watu na kusema, ‘Nilitenda dhambi na kupotosha kilichokuwa haki, lakini sikuadhibiwa kama nilivyostahili.
Ndipo mtu huyo ataimba mbele ya watu wengine na kusema, 'Nilitenda dhambi na kuasi kile kilichokuwa cha haki, lakini dhambi yangu haikuadhibiwa.
28 Alinikomboa nafsi yangu nisitumbukie shimoni, nami nitaishi ili kuufurahia mwanga.’
Mungu ameiokoa roho yangu isiende chini shimoni; maisha yangu yataendelea kuuona mwanga.'
29 “Mungu hufanya haya yote kwa mwanadamu; mara mbili hata mara tatu,
Tazama, Mungu hufanya mambo haya yote pamoja na mwanadamu, mara mbili, naam, hata mara tatu,
30 ili aigeuze nafsi yake toka shimoni, ili nuru ya uzima imwangazie.
kuirudisha roho yake kutoka shimoni, ili kwamba aweze kumlikwa na mwanga wa maisha.
31 “Ayubu, zingatia, nisikilize mimi; nyamaza, nami nitanena.
Ayubu, zingatia na unisikilize mimi; nyamaza nami nitasema.
32 Kama unalo lolote la kusema, unijibu; sema, kwa maana ninataka uonekane huna hatia.
Ikiwa una kitu cha kusema, na unijibu; sema, maana nataka kuhakikisha kwamba wewe uko katika haki.
33 Lakini kama huna la kusema, basi nisikilize mimi; nyamaza, nami nitakufundisha hekima.”
Kama sivyo, basi nisikilize, ubaki kimya, nami nitakufundisha wewe hekima.”

< Ayubu 33 >