< Ayubu 32 >

1 Basi watu hawa watatu wakaacha kumjibu Ayubu, kwa kuwa alikuwa mwadilifu machoni pake mwenyewe.
וישבתו שלשת האנשים האלה-- מענות את-איוב כי הוא צדיק בעיניו
2 Lakini Elihu mwana wa Barakeli, wa kabila la Buzi wa jamaa ya Ramu, akamkasirikia sana Ayubu, kwa sababu ya kujihesabia haki mwenyewe badala ya Mungu.
ויחר אף אליהוא בן-ברכאל הבוזי-- ממשפחת-רם באיוב חרה אפו-- על-צדקו נפשו מאלהים
3 Pia aliwakasirikia hao rafiki watatu wa Ayubu, kwa sababu hawakuweza kupata njia ya kuthibitisha ya kuwa hayo maneno ya Ayubu hayakuwa ya kweli, nao bado walikuwa wamemlaumu.
ובשלשת רעיו חרה אפו על אשר לא-מצאו מענה-- וירשיעו את-איוב
4 Basi Elihu alikuwa amesubiri kwanza waongee na Ayubu kwa sababu walikuwa na umri mkubwa kumliko yeye.
ואליהו--חכה את-איוב בדברים כי זקנים-המה ממנו לימים
5 Lakini alipoona watu hao watatu hawakuwa na kitu zaidi cha kusema, hasira yake ikaamka.
וירא אליהוא--כי אין מענה בפי שלשת האנשים ויחר אפו
6 Basi Elihu mwana wa Barakeli wa kabila la Buzi akasema: “Mimi ni mdogo kwa umri, nanyi ni wazee; ndiyo sababu niliogopa, sikuthubutu kuwaambia kile ninachojua.
ויען אליהוא בן ברכאל הבוזי-- ויאמר צעיר אני לימים ואתם ישישים על-כן זחלתי ואירא מחות דעי אתכם
7 Nilifikiri, ‘Yafaa umri useme, nao wingi wa miaka ungefundisha hekima.’
אמרתי ימים ידברו ורב שנים ידיעו חכמה
8 Lakini ni Roho iliyoko ndani ya mwanadamu, pumzi ya Mwenyezi, ndiyo impayo yeye ufahamu.
אכן רוח-היא באנוש ונשמת שדי תבינם
9 Sio wazee peke yao walio na hekima, sio wenye umri mkubwa peke yao wanaofahamu lililo sawa.
לא-רבים יחכמו וזקנים יבינו משפט
10 “Kwa hiyo nasema: Nisikilizeni mimi; mimi nami nitawaambia lile ninalojua.
לכן אמרתי שמעה-לי אחוה דעי אף-אני
11 Nilingojea mlipokuwa mnaongea, nilizisikiliza hoja zenu; mlipokuwa mkitafuta maneno ya kusema,
הן הוחלתי לדבריכם--אזין עד-תבונתיכם עד-תחקרון מלין
12 niliwasikiliza kwa makini. Lakini hakuna hata mmoja wenu aliyethibitisha kwamba Ayubu amekosa; hakuna hata mmoja wenu aliyeweza kujibu hoja zake.
ועדיכם אתבונן והנה אין לאיוב מוכיח--עונה אמריו מכם
13 Msiseme, ‘Tumepata hekima; Mungu na amthibitishe kuwa mwongo, wala si mwanadamu.’
פן-תאמרו מצאנו חכמה אל ידפנו לא-איש
14 Lakini Ayubu hajayapanga maneno yake dhidi yangu, nami sitamjibu kwa kutumia hoja zenu.
ולא-ערך אלי מלין ובאמריכם לא אשיבנו
15 “Wametiwa hofu na hawana la zaidi la kusema; maneno yamewaishia.
חתו לא-ענו עוד העתיקו מהם מלים
16 Je, ningoje sasa kwa sababu wamekuwa kimya, kwa vile sasa wanasimama bila kuwa na la kujibu?
והוחלתי כי-לא ידברו כי עמדו לא-ענו עוד
17 Mimi nami nitakuwa na la kusema; mimi nami nitasema lile nilijualo.
אענה אף-אני חלקי אחוה דעי אף-אני
18 Kwa kuwa nimejawa na maneno, nayo Roho iliyomo ndani yangu yanisukuma;
כי מלתי מלים הציקתני רוח בטני
19 ndani yangu niko kama chupa iliyojazwa divai, kama kiriba kipya cha divai kilicho tayari kupasuka.
הנה-בטני--כיין לא-יפתח כאבות חדשים יבקע
20 Ni lazima niseme ili niweze kutulia; ni lazima nifumbue midomo yangu nipate kujibu.
אדברה וירוח-לי אפתח שפתי ואענה
21 Sitampendelea mtu yeyote, wala sitajipendekeza kwa mtu yeyote;
אל-נא אשא פני-איש ואל-אדם לא אכנה
22 kwa kuwa kama ningekuwa stadi wa kujipendekeza, Muumba wangu angeniondolea mbali kwa upesi.
כי לא ידעתי אכנה כמעט ישאני עשני

< Ayubu 32 >