< Ayubu 29 >

1 Ayubu akaendelea na hoja yake, akasema:
Ayubu akaendelea na kusema,
2 “Tazama jinsi ninavyoitamani miezi iliyopita, zile siku ambazo Mungu alikuwa akinilinda,
Ee, ningekuwa kama nilivyokuwa miezi iliyopita wakati Mungu aliponiagalia,
3 wakati taa yake iliniangazia kichwani changu, na kwa mwanga wake Mungu nikapita katikati ya giza!
taa yake ilipowaka kichwani pangu, na pale nilipotembea gizani kwa nuru yake.
4 Natamani siku zile nilizokuwa katika ustawi wangu, wakati urafiki wa Mungu wa ndani ulipoibariki nyumba yangu,
Ee, kwamba ningekuwa kama nilivyokuwa katika siku za ujana wangu uhusiano wangu na Mungu ulivyokuwa mzuri,
5 wakati Mwenyezi alikuwa pamoja nami, nao watoto wangu walikuwa wamenizunguka,
wakati Mwenyezi alipokuwa pamoja nami, na wanangu walipokuwa karibu nami,
6 wakati njia yangu ilikuwa imenyweshewa siagi, nao mwamba ukanimiminia vijito vya mafuta ya zeituni.
wakati maisha yangu yalipokuwa yamejawa na utele, na mwamba uliponichuruzishia chemichemi za mafuta.
7 “Wakati nilipokwenda kwenye lango la mji na kuketi katika kiwanja,
Nilipokwenda langoni mwa mji, nilipokaa katika eneo la mji,
8 vijana waliniona wakakaa kando, nao wazee walioketi wakasimama;
vijana waliniona na walikaa mbali kwa kuniheshimu, na wazee waliinuka na kusimama kwa ajili yangu.
9 wakuu wakaacha kuzungumza na kuziba vinywa vyao kwa mikono yao;
Wana wa mfalme waliacha kuongea nilipofika; wangeweka mkono wao katika vinywa vyao.
10 wenye vyeo wakanyamazishwa, nazo ndimi zao zikagandamana na makaakaa ya vinywa vyao.
Sauti za waheshimiwa zililazimishwa, na ndimi zao hazikuweza kuongea vinywani mwao.
11 Yeyote aliyenisikia alinena mema juu yangu, nao walioniona walinisifu,
Kwani baada ya kunisikia, wangenibariki; waliponiona, wangeniona na kuniheshimu
12 kwa sababu nilimwokoa maskini aliyeomba msaada, naye yatima aliyekuwa hana wa kumsaidia.
kwa maana nilikuwa nikiwasaidia masikini waliokuwa wakiteseka, na yatima, asiye na msaada.
13 Mtu aliyekuwa karibu kufa alinibariki, nami niliufanya moyo wa mjane kuimba.
Baraka zao waliokuwa karibu kuangamia zilinipata; niliufanya moyo wa mjane kuimba kwa furaha.
14 Niliivaa haki kama vazi langu; uadilifu ulikuwa joho langu na kilemba changu.
Nilijivika utakatifu, nao ulinifunika; haki yangu ilikuwa kama kanzu na kilemba.
15 Nilikuwa macho ya kipofu na miguu kwa kiwete.
Niliwasaidia vipofu; niliwasaidia walemavu.
16 Nilikuwa baba kwa mhitaji; nilimtetea mgeni.
Niliwasaidia wahitaji; niliwasaidia hata wasionijua.
17 Niliyavunja meno makali ya waovu, na kuwapokonya wahanga kwenye meno yao.
Nilimnyamazisha mwovu; nilimpokonya manusura kutoka katika meno yake.
18 “Nikafikiri, ‘Nitafia katika nyumba yangu mwenyewe, nazo siku zangu zitakuwa nyingi kama chembechembe za mchanga.
Kisha nilisema nitakufa mahali salama; nitazizidisha siku zangu kama mchanga.
19 Mizizi yangu itafika mpaka kwenye maji, nao umande utakaa juu ya matawi yangu usiku kucha.
Mizizi yangu imeenea majini, na umande kukaa usiku wote katika matawi yangu.
20 Utukufu wangu utabakia kuwa mpya ndani yangu, upinde wangu daima utaendelea kuwa mpya mkononi mwangu.’
Heshima yangu ni mpya daima, na nguvu za upinde wangu zipo katika mkono wangu kila wakati.
21 “Watu walinisikiliza kwa tumaini, wakingojea ushauri wangu kwa utulivu.
Watu walinisikiliza; walinisubiri; walisikiliza ushauri wangu.
22 Baada ya mimi kuzungumza, hawakusema zaidi; maneno yangu yaliingia masikioni mwao kwa makini.
Nilipo maliza kuongea hawakunena tena, maneno yangu yaliwatia nguvu kama mvua.
23 Waliningojea kama manyunyu ya mvua na kuyapokea maneno yangu kama ardhi inyonyavyo mvua ya vuli.
Waliningoja kama kungoja mvua; waliyathamini maneno yangu, kama walivyotamani mvua iliyokawia.
24 Walipokata tamaa niliwaonyesha uso wa furaha; nuru ya uso wangu ilikuwa ya thamani kwao.
Niliwafurahia bila wao kutarajia; hawakukataa uzuri wa uso wangu.
25 Niliwachagulia njia na kukaa kama mkuu wao; niliishi kama mfalme katikati ya majeshi yake; nikawa kama yeye anayewafariji waombolezaji.
Nilikuwa kama mfalme wao na kuwachagulia cha kufanya; nilikuwa kama mfalme katika jeshi lake, kama awafarijiye waombolezaji mazishini.

< Ayubu 29 >