< Ayubu 27 >

1 Ndipo Ayubu akaendelea na hoja yake, akasema:
Ayubu akaendelea kuoengea na kusema,
2 “Hakika kama Mungu aishivyo, aliyeninyima haki yangu, Mwenyezi ambaye amenifanya nionje uchungu wa nafsi,
“Kama aishivyo Mungu, ameniondolea haki yangu, Mwenyezi, aliyeyafanya machungu maisha yangu,
3 kwa muda wote nitakaokuwa na uhai ndani yangu, nayo pumzi ya Mungu ikiwa puani mwangu,
kadili uhai ungalimo ndani yangu uzima wa Mungu upo puani mwangu.
4 midomo yangu haitanena uovu, wala ulimi wangu hautatamka udanganyifu.
Hakika midomo yangu haitanena uovu, wala ulimi wangu kunena uongo.
5 Sitakubaliana nanyi kabisa kuwa mko sahihi; hadi nife, sitakana uadilifu wangu.
Sitakiri kwamba mko sahihi; hata nifapo sitakana uadilifu wangu.
6 Nitadumisha haki yangu wala sitaiacha; dhamiri yangu haitanisuta muda wote ninaoishi.
Naishikilia haki yangu na sitaiacha; nafsi yangu haitanisuta kadili ninavyoishi.
7 “Watesi wangu wawe kama waovu, nao adui zangu wawe kama wasio haki!
Adui yangu na awe kama mwovu; anayeinuka kunyume changu na awe kama asiye haki.
8 Kwa maana mtu asiyemcha Mungu analo tegemeo gani anapokatiliwa mbali, Mungu anapouondoa uhai wake?
Kwani tumaini la mwovu ni nini Mungu anapomwondoa, Mungu anapochukua uhai wake?
9 Je, Mungu husikiliza kilio chake, shida zimjiapo?
Je Mungu atasikiliza kilio chake tabu zinapompat?
10 Je, anaweza kumfurahia Mwenyezi? Je, atamwita Mungu nyakati zote?
Je atajifurahisha katika Mwenyezi na kumwita Mungu nyakati zote
11 “Nitawafundisha juu ya uweza wa Mungu; njia za Mwenyezi sitazificha.
Nitawafundisha kuhusu uwezo wa Mungu; sitabatilisha mawazo ya Mwenyezi.
12 Ninyi nyote mmeona hili wenyewe. Ni ya nini basi mazungumzo haya yasiyo na maana?
Tazama, ninyi nyote mmeona; kwa nini basi mmeongea yasiyo na maana.
13 “Hili ndilo fungu ambalo Mungu humpa mtu mwovu, urithi ule mtu mdhalimu anapokea kutoka kwa Mwenyezi:
Hii ndiyo hatima ya waovu mbele za Mungu, urithi wa mtesaji aupokeao kutoka kwa Mwenyezi.
14 Hata kama watoto wake watakuwa wengi kiasi gani, fungu lao ni kuuawa kwa upanga; wazao wake hawatakuwa kamwe na chakula cha kuwatosha.
Ikiwa watoto wake wataongezeka, ni kwa upanga; uzao wake utakuwa na njaa.
15 Tauni itawazika wale watakaonusurika miongoni mwao, nao wajane wao hawatawaombolezea.
Wanaomsalia watauawa kwa tauni, na wajane wao hawatawaombolezea.
16 Ajapokusanya fedha nyingi kama mavumbi, na mavazi kama malundo ya udongo wa mfinyanzi,
Japokuwa waovu hurundika mali kama mavumbi,
17 yale yote mtu mwovu aliyojiwekea akiba, mwenye haki atayavaa, naye asiye na hatia ataigawanya fedha yake.
na kukusanya mavazi kama udongo, atakusanya mavazi, lakini mwenye haki atavaa, na wasio na hatia watagawana mali.
18 Nyumba aijengayo ni kama utando wa buibui, kama kibanda alichotengeneza mlinzi.
Hujenga nyumba yake kama buibui, kama kibanda cha muda afanyacho mlinzi.
19 Yeye hulala akiwa tajiri, lakini ndiyo mara ya mwisho; afunguapo macho yake, yote yametoweka.
Hulala kitandani akiwa tajiri, lakini hataendelea hivyo; na afumbuapo macho, hana kitu.
20 Vitisho humjia kama mafuriko; dhoruba humkumba ghafula usiku.
Vitisho humpata kama maji, dhoruba humwondoa usiku.
21 Upepo mkali wa mashariki humchukua, naye hutoweka; humzoa kutoka mahali pake.
Upepo wa mashariki umwondoa, naye huondoka; humwondoa mahali pake.
22 Humvurumisha bila huruma, huku akikimbia kasi kukwepa nguvu zake.
Humpiga bila kukoma; hujaribu kumnasua katika uwezo wake.
23 Upepo humpigia makofi kwa dharau, na kumfukuza atoke mahali pake.
Unampigia makofi kwa kejeli; humwondoa mahali pake.

< Ayubu 27 >