< Ayubu 27 >

1 Ndipo Ayubu akaendelea na hoja yake, akasema:
ויסף איוב שאת משלו ויאמר
2 “Hakika kama Mungu aishivyo, aliyeninyima haki yangu, Mwenyezi ambaye amenifanya nionje uchungu wa nafsi,
חי-אל הסיר משפטי ושדי המר נפשי
3 kwa muda wote nitakaokuwa na uhai ndani yangu, nayo pumzi ya Mungu ikiwa puani mwangu,
כי-כל-עוד נשמתי בי ורוח אלוה באפי
4 midomo yangu haitanena uovu, wala ulimi wangu hautatamka udanganyifu.
אם-תדברנה שפתי עולה ולשוני אם-יהגה רמיה
5 Sitakubaliana nanyi kabisa kuwa mko sahihi; hadi nife, sitakana uadilifu wangu.
חלילה לי אם-אצדיק אתכם עד-אגוע-- לא-אסיר תמתי ממני
6 Nitadumisha haki yangu wala sitaiacha; dhamiri yangu haitanisuta muda wote ninaoishi.
בצדקתי החזקתי ולא ארפה לא-יחרף לבבי מימי
7 “Watesi wangu wawe kama waovu, nao adui zangu wawe kama wasio haki!
יהי כרשע איבי ומתקוממי כעול
8 Kwa maana mtu asiyemcha Mungu analo tegemeo gani anapokatiliwa mbali, Mungu anapouondoa uhai wake?
כי מה-תקות חנף כי יבצע כי ישל אלוה נפשו
9 Je, Mungu husikiliza kilio chake, shida zimjiapo?
הצעקתו ישמע אל-- כי-תבוא עליו צרה
10 Je, anaweza kumfurahia Mwenyezi? Je, atamwita Mungu nyakati zote?
אם-על-שדי יתענג יקרא אלוה בכל-עת
11 “Nitawafundisha juu ya uweza wa Mungu; njia za Mwenyezi sitazificha.
אורה אתכם ביד-אל אשר עם-שדי לא אכחד
12 Ninyi nyote mmeona hili wenyewe. Ni ya nini basi mazungumzo haya yasiyo na maana?
הן-אתם כלכם חזיתם ולמה-זה הבל תהבלו
13 “Hili ndilo fungu ambalo Mungu humpa mtu mwovu, urithi ule mtu mdhalimu anapokea kutoka kwa Mwenyezi:
זה חלק-אדם רשע עם-אל ונחלת עריצים משדי יקחו
14 Hata kama watoto wake watakuwa wengi kiasi gani, fungu lao ni kuuawa kwa upanga; wazao wake hawatakuwa kamwe na chakula cha kuwatosha.
אם-ירבו בניו למו-חרב וצאצאיו לא ישבעו-לחם
15 Tauni itawazika wale watakaonusurika miongoni mwao, nao wajane wao hawatawaombolezea.
שרידיו במות יקברו ואלמנתיו לא תבכינה
16 Ajapokusanya fedha nyingi kama mavumbi, na mavazi kama malundo ya udongo wa mfinyanzi,
אם-יצבר כעפר כסף וכחמר יכין מלבוש
17 yale yote mtu mwovu aliyojiwekea akiba, mwenye haki atayavaa, naye asiye na hatia ataigawanya fedha yake.
יכין וצדיק ילבש וכסף נקי יחלק
18 Nyumba aijengayo ni kama utando wa buibui, kama kibanda alichotengeneza mlinzi.
בנה כעש ביתו וכסכה עשה נצר
19 Yeye hulala akiwa tajiri, lakini ndiyo mara ya mwisho; afunguapo macho yake, yote yametoweka.
עשיר ישכב ולא יאסף עיניו פקח ואיננו
20 Vitisho humjia kama mafuriko; dhoruba humkumba ghafula usiku.
תשיגהו כמים בלהות לילה גנבתו סופה
21 Upepo mkali wa mashariki humchukua, naye hutoweka; humzoa kutoka mahali pake.
ישאהו קדים וילך וישערהו ממקמו
22 Humvurumisha bila huruma, huku akikimbia kasi kukwepa nguvu zake.
וישלך עליו ולא יחמל מידו ברוח יברח
23 Upepo humpigia makofi kwa dharau, na kumfukuza atoke mahali pake.
ישפק עלימו כפימו וישרק עליו ממקמו

< Ayubu 27 >