< Ayubu 26 >
Kisha Ayubu akajibu na kusema,
2 “Tazama jinsi ulivyomsaidia mtu asiye na uwezo! Jinsi ulivyouokoa mkono ulio dhaifu!
“Mmemsaidiaje aliyedhaifu!
3 Ni shauri gani ulilompa yeye asiye na hekima? Nayo ni busara gani kubwa uliyoonyesha!
Jinsi gani mmemshauri asiye na hekima na kutamka maneno yenye maarifa kwake!
4 Ni nani aliyekusaidia kutamka maneno hayo? Nayo ni roho ya nani iliyosema kutoka kinywani mwako?
Kwa msaada wa nani mmesema maneno haya? Ni roho ya nani iliyotoka ndani yenu?
5 “Wafu wako katika maumivu makuu, wale walio chini ya maji na wale waishio ndani yake.
Maiti inatetemeka chini ya maji, na vyote wilivyomo ndani yake.
6 Mauti iko wazi mbele za Mungu; Uharibifu haukufunikwa. (Sheol )
Kuzimu kuko wazi mbele ya Mungu; uharibifu hauna kizuizi dhidi yake. (Sheol )
7 Hutandaza anga la kaskazini mahali patupu; naye huiningʼiniza dunia mahali pasipo na kitu.
Huitandaza kaskazi juu ya nafasi wazi na kuining'iniza dunia hewani.
8 Huyafungia maji kwenye mawingu yake, hata hivyo mawingu hayapasuki kwa uzito wake.
Huyafunga maji katika mawingu yake mazito, lakini hayagawanyiki chini yake.
9 Huufunika uso wa mwezi mpevu, akitandaza mawingu juu yake.
Huufunika uso wa mwezi na kueneza mawingu yake juu yake.
10 Amechora mstari wa upeo juu ya uso wa maji, ameweka mpaka wa nuru na giza.
Amechora ukingo wa duara juu ya maji kama mpaka kati ya nuru na giza.
11 Nguzo za mbingu nazo zatetemeka, zinatishika anapozikemea.
Nguzo za mbinguni zinatikisika na zimestushwa na kukemea kwake.
12 Kwa nguvu zake aliisukasuka bahari; kwa hekima yake alimkata Rahabu vipande vipande.
Aliituliza bahari kwa uwezo wake; kwa ufahamu wake alimwaribu Rahab
13 Aliisafisha anga kwa pumzi yake; kwa mkono wake alimchoma joka aendaye mbio.
Kwa pumzi yake, aliziondoa mbingu kwa dhorubu; mbingu ziliondolewa kwa dhorubu; mkono wake ulimchoma nyoka anayekimbia.
14 Haya ni mambo madogo tu katika matendo yake; tazama jinsi ulivyo mdogo mnongʼono tunaousikia kumhusu! Ni nani basi awezaye kuelewa ngurumo za nguvu zake?”
Tazama, hizi si zaidi ya madogo ya njia zake; Jinsi gani tunasikia akitunong'oneza! Ni nani awezaye kufahamu uwezo wake.