< Ayubu 26 >

1 Kisha Ayubu akajibu:
ויען איוב ויאמר
2 “Tazama jinsi ulivyomsaidia mtu asiye na uwezo! Jinsi ulivyouokoa mkono ulio dhaifu!
מה-עזרת ללא-כח הושעת זרוע לא-עז
3 Ni shauri gani ulilompa yeye asiye na hekima? Nayo ni busara gani kubwa uliyoonyesha!
מה-יעצת ללא חכמה ותשיה לרב הודעת
4 Ni nani aliyekusaidia kutamka maneno hayo? Nayo ni roho ya nani iliyosema kutoka kinywani mwako?
את-מי הגדת מלין ונשמת-מי יצאה ממך
5 “Wafu wako katika maumivu makuu, wale walio chini ya maji na wale waishio ndani yake.
הרפאים יחוללו-- מתחת מים ושכניהם
6 Mauti iko wazi mbele za Mungu; Uharibifu haukufunikwa. (Sheol h7585)
ערום שאול נגדו ואין כסות לאבדון (Sheol h7585)
7 Hutandaza anga la kaskazini mahali patupu; naye huiningʼiniza dunia mahali pasipo na kitu.
נטה צפון על-תהו תלה ארץ על-בלימה
8 Huyafungia maji kwenye mawingu yake, hata hivyo mawingu hayapasuki kwa uzito wake.
צרר-מים בעביו ולא-נבקע ענן תחתם
9 Huufunika uso wa mwezi mpevu, akitandaza mawingu juu yake.
מאחז פני-כסה פרשז עליו עננו
10 Amechora mstari wa upeo juu ya uso wa maji, ameweka mpaka wa nuru na giza.
חק-חג על-פני-מים-- עד-תכלית אור עם-חשך
11 Nguzo za mbingu nazo zatetemeka, zinatishika anapozikemea.
עמודי שמים ירופפו ויתמהו מגערתו
12 Kwa nguvu zake aliisukasuka bahari; kwa hekima yake alimkata Rahabu vipande vipande.
בכחו רגע הים ובתובנתו (ובתבונתו) מחץ רהב
13 Aliisafisha anga kwa pumzi yake; kwa mkono wake alimchoma joka aendaye mbio.
ברוחו שמים שפרה חללה ידו נחש ברח
14 Haya ni mambo madogo tu katika matendo yake; tazama jinsi ulivyo mdogo mnongʼono tunaousikia kumhusu! Ni nani basi awezaye kuelewa ngurumo za nguvu zake?”
הן-אלה קצות דרכו-- ומה-שמץ דבר נשמע-בו ורעם גבורתו מי יתבונן

< Ayubu 26 >