< Ayubu 23 >

1 Ndipo Ayubu akajibu:
Kisha Ayubu akajibu na kusema,
2 “Hata leo malalamiko yangu ni chungu; mkono wake ni mzito juu yangu hata nikiugua.
“Hata leo malalamiko yangu ni machungu; maumivu yangu ni mazito kuliko manung'uniko yangu.
3 Laiti ningefahamu mahali pa kumwona; laiti ningeweza kwenda mahali akaapo!
Ee, ningejua niwezapokumwona! Ee, kwamba ningeweza kwenda alipo!
4 Ningeliweka shauri langu mbele zake, na kukijaza kinywa changu na hoja.
Ningeweka shitaka langu mbele yake na kukijaza kinywa changu hoja.
5 Ningejua kwamba angenijibu nini, na kuelewa lile ambalo angelisema.
Ningejua ambavyo angenijibu na kufahamu ambavyo angesema juu yangu.
6 Je, angenipinga kwa nguvu nyingi? La, asingenigandamiza.
Je angehojiana nami katika ukuu wa nguvu zake? Hapana, angenisikiliza.
7 Hapo mtu mwadilifu angeweka shauri lake mbele zake, nami ningeokolewa milele na mhukumu wangu.
Pale mwenye haki angehojiana nami. Kwa njia hii ningeonekana bila hatia kwa mwamzi wangu.
8 “Lakini nikienda mashariki, hayupo; nikienda magharibi, simpati.
Tazama, naelekea mashariki, lakini hayupo pale, na upande wa magharibi, lakini siwezi kumwona.
9 Anapokuwa kazini pande za kaskazini, simwoni; akigeukia kusini, nako simwoni hata kidogo.
Kaskazini, anapofanya kazi, lakini siwezi kumwona, na kusini, anapojificha hata nisimwone.
10 Lakini anaijua njia niiendeayo; akiisha kunijaribu, nitatoka kama dhahabu.
Lakini anaijua njia ninayoichukua; atakapokuwa amenipima, nitatoka kama dhahabu.
11 Nyayo zangu zimefuata hatua zake kwa karibu; nimeishika njia yake bila kukengeuka.
Mguu wangu umeunganishwa na hatua zake; nimezitunza njia zake na sijageuka.
12 Sijaziacha amri zilizotoka midomoni mwake; nimeyathamini maneno ya kinywa chake kuliko chakula changu cha kila siku.
Sijaiacha amri ya midomo yake; nimeyatii maneno ya kinywa chake.
13 “Lakini yeye husimama peke yake; ni nani awezaye kumpinga? Yeye hufanya lolote atakalo.
Lakini yeye ni wa pekee, naniawezaye kumgeuza? Analolitaka, hulitenda.
14 Hutimiliza maagizo yake dhidi yangu, na bado anayo mipango mingi kama hiyo ambayo ameiweka akiba.
Kwa maana hulitimiza agizo lake kinyume changu; anamipango mingi kwa ajili yangu; ipo mingi kama hiyo.
15 Hiyo ndiyo sababu ninaingiwa na hofu mbele zake; nifikiriapo haya yote ninamwogopa.
Kwa hiyo, nimetishwa mbele zake; ninapofikiri kumhusu, ninamwogopa.
16 Mungu ameufanya moyo wangu kuzimia; yeye Mwenyezi amenitia hofu.
Kwani Mungu ameudhoofisha moyo wangu; Mwenyezi amenitisha.
17 Hata hivyo sijanyamazishwa na giza, wala kwa giza nene linalofunika uso wangu.
Si kwa sababu nimeondolewa na giza, wala siyo kwamba giza nene limeufunika uso wangu.

< Ayubu 23 >