< Ayubu 21 >

1 Ndipo Ayubu akajibu:
ויען איוב ויאמר
2 “Yasikilizeni maneno yangu kwa makini; hii na iwe faraja mnayonipa mimi.
שמעו שמוע מלתי ותהי-זאת תנחומתיכם
3 Nivumilieni ninapozungumza, nami nikishazungumza, endeleeni kunidhihaki.
שאוני ואנכי אדבר ואחר דברי תלעיג
4 “Je, kwani malalamiko yangu yanaelekezwa kwa mwanadamu? Kwa nini nisikose subira?
האנכי לאדם שיחי ואם-מדוע לא-תקצר רוחי
5 Niangalieni mkastaajabu; mkaweke mkono juu ya vinywa vyenu.
פנו-אלי והשמו ושימו יד על-פה
6 Ninapowaza juu ya hili, ninaogopa, nao mwili wangu unatetemeka.
ואם-זכרתי ונבהלתי ואחז בשרי פלצות
7 Kwa nini waovu wanaendelea kuishi, wakifikia umri wa uzee na kuendelea kuwa na nguvu?
מדוע רשעים יחיו עתקו גם-גברו חיל
8 Huwaona watoto wao wakithibitika wakiwa wamewazunguka, wazao wao mbele za macho yao.
זרעם נכון לפניהם עמם וצאצאיהם לעיניהם
9 Nyumba zao zi salama wala hakuna hofu; fimbo ya Mungu haiko juu yao.
בתיהם שלום מפחד ולא שבט אלוה עליהם
10 Madume yao ya ngʼombe huvyaza bila kushindwa kamwe; ngʼombe wao huzaa wala hawaharibu mimba.
שורו עבר ולא יגעל תפלט פרתו ולא תשכל
11 Huwatoa watoto wao nje kama kundi; wadogo wao huchezacheza.
ישלחו כצאן עויליהם וילדיהם ירקדון
12 Huimba nyimbo kwa matari na kwa kinubi, nao huifurahia sauti ya filimbi.
ישאו כתף וכנור וישמחו לקול עוגב
13 Huitumia miaka yao katika mafanikio nao hushuka kaburini kwa amani. (Sheol h7585)
יבלו (יכלו) בטוב ימיהם וברגע שאול יחתו (Sheol h7585)
14 Lakini humwambia Mungu, ‘Tuache sisi!’ Hatuna haja ya kufahamu njia zako.
ויאמרו לאל סור ממנו ודעת דרכיך לא חפצנו
15 Mwenyezi ni nani hata tumtumikie? Tutapata faida gani kumwomba?
מה-שדי כי-נעבדנו ומה-נועיל כי נפגע-בו
16 Lakini kufanikiwa kwao hakupo mikononi mwao wenyewe, hivyo najitenga mbali na shauri la waovu.
הן לא בידם טובם עצת רשעים רחקה מני
17 “Lakini ni mara ngapi taa ya waovu huzimwa? Ni mara ngapi maafa huwajia, yale yawapatayo ambayo Mungu huwapangia katika hasira yake?
כמה נר-רשעים ידעך-- ויבא עלימו אידם חבלים יחלק באפו
18 Ni mara ngapi huwa kama majani makavu mbele ya upepo, kama makapi yachukuliwayo na dhoruba?
יהיו כתבן לפני-רוח וכמץ גנבתו סופה
19 Imesemekana, ‘Mungu huiweka akiba adhabu ya mtu kwa ajili ya wanawe.’ Mungu na amlipe mtu mwenyewe, ili apate kulijua!
אלוה יצפן-לבניו אונו ישלם אליו וידע
20 Macho yake mwenyewe na yaone maangamizi yake; yeye na ainywe ghadhabu ya Mwenyezi.
יראו עינו כידו ומחמת שדי ישתה
21 Kwani anajali nini kuhusu jamaa anayoiacha nyuma, miezi yake aliyopangiwa ifikapo mwisho?
כי מה-חפצו בביתו אחריו ומספר חדשיו חצצו
22 “Je, yuko mtu yeyote awezaye kumfundisha Mungu maarifa, iwapo yeye ndiye ahukumuye hata walio juu ya wote?
הלאל ילמד-דעת והוא רמים ישפוט
23 Mtu mmoja hufa akiwa na nguvu zake kamili, akiwa salama na mwenye raha kamili,
זה--ימות בעצם תמו כלו שלאנן ושליו
24 mwili wake ukiwa umenawiri, nayo mifupa yake ikiwa imejaa mafuta ndani yake.
עטיניו מלאו חלב ומח עצמותיו ישקה
25 Mtu mwingine hufa katika uchungu wa nafsi, akiwa hajafurahia kamwe jambo lolote zuri.
וזה--ימות בנפש מרה ולא-אכל בטובה
26 Hao wote hulala mavumbini, nao mabuu huwafunika wote.
יחד על-עפר ישכבו ורמה תכסה עליהם
27 “Ninayajua kikamilifu yale mnayoyafikiri, mipango ambayo kwayo mngenitendea mabaya.
הן ידעתי מחשבותיכם ומזמות עלי תחמסו
28 Mwasema, ‘Iko wapi sasa nyumba ya huyo mtu mkuu, mahema ambayo watu waovu walikaa?’
כי תאמרו איה בית-נדיב ואיה אהל משכנות רשעים
29 Je, hamkuwahi kuwauliza hao wanaosafiri? Je, hamkutafakari taarifa zao:
הלא שאלתם עוברי דרך ואתתם לא תנכרו
30 kwamba mtu mwovu huepushwa kutoka siku ya maafa, kwamba huokolewa kutoka siku ya ghadhabu?
כי ליום איד יחשך רע ליום עברות יובלו
31 Ni nani hulaumu matendo yake mbele ya uso wake? Ni nani ampatilizaye kwa yale aliyoyatenda?
מי-יגיד על-פניו דרכו והוא-עשה מי ישלם-לו
32 Hupelekwa kaburini, nao ulinzi ukawekwa kwenye kaburi lake.
והוא לקברות יובל ועל-גדיש ישקוד
33 Udongo ulio bondeni ni mtamu kwake; watu wote watamfuata, nao umati wa watu usiohesabika umemtangulia.
מתקו-לו רגבי-נחל ואחריו כל-אדם ימשוך ולפניו אין מספר
34 “Hivyo ninyi mnawezaje kunifariji kwa upuzi wenu? Hakuna kilichosalia cha majibu yenu isipokuwa uongo!”
ואיך תנחמוני הבל ותשובתיכם נשאר-מעל

< Ayubu 21 >