< Ayubu 19 >

1 Ndipo Ayubu akajibu:
Ndipo Ayubu akajibu na kusema,
2 “Je, mtaendelea kunitesa mpaka lini, na kuniponda kwa maneno yenu?
lini mtanifanya mimi kuteseka na kunivunja vunja mimi vipande vipnde kwa maneno?
3 Mara kumi hizi mmenishutumu; bila aibu mnanishambulia.
Mara kumi hivi mmenishutumu mimi; ninyi hamuoni aibu kwamba mmenitendea mimi kwa ukatili.
4 Kama ni kweli nimepotoka, kosa langu ninabaki kuhusika nalo mwenyewe.
Kama ni dhahiri kweli mimi nimekosa, makosa yangu hubaki kuwa wajibu wangu.
5 Kama kweli mngejitukuza wenyewe juu yangu, na kutumia unyonge wangu dhidi yangu,
Kama ni dhahiri ninyi mtajiinua juu yangu mimi na kuutumia uvumilivu wangu kunipinga mimi,
6 basi jueni kuwa Mungu amenitendea yaliyo mabaya, naye amekokota wavu wake kunizunguka.
kisha ninyi mnapaswa kutambua kwamba Mungu amefanya mabaya kwangu mimi na amenikamata mimi katika mtego wake yeye.
7 “Ingawa ninalia, ‘Nimetendewa mabaya!’ sipati jibu; ingawa ninaomba msaada, hakuna haki.
Tazama, Mimi ninalia kwa sauti, “dhuluma!” lakini sipati jibu. Mimi ninaita kwa ajili ya msaada, lakini hakuna haki.
8 Yeye ameizuia njia yangu hivyo siwezi kupita; ameyafunika mapito yangu na giza.
Yeye ameiwekea ukuta njia yangu, ili kwamba mimi nisiweze kupita, na yeye ameweka giza katika njia yangu.
9 Amenivua heshima yangu, na kuniondolea taji kichwani pangu.
Yeye ameniondoa Mimi kutoka katika utukufu wangu, na ameichukua taji kutoka kwenye kichwa changu mimi.
10 Amenibomoa kila upande hadi nimeisha; amelingʼoa tegemeo langu kama mti.
Yeye amenivunjavunja mimi chini kwa kila upande, na Mimi nimetoweka; yeye amelikokota juu tumaini langu kama mti.
11 Hasira yake imewaka juu yangu; amenihesabu kuwa miongoni mwa adui zake.
Yeye pia ameiongeza ghadhabu yake dhidi yangu mimi; yeye ananihesabu mimi kama mmoja wa adui zake.
12 Majeshi yake yananisogelea kwa nguvu; yamenizingira, yamepiga kambi kulizunguka hema langu.
Majeshi yake huja juu pamoja; wao wananikosesha tumaini kwa kuniteka nyara kwa kundi kubwa kupigana na mimi wakizunguka hema yangu.
13 “Amewatenga ndugu zangu mbali nami; wale tunaojuana nao wamefarakana nami kabisa.
Yeye amewaweka ndugu zangu mbali kutoka kwangu mimi; watu wangu wa karibu wote wamejitenga kutoka kwangu mimi.
14 Watu wa jamaa yangu wamekwenda mbali; rafiki zangu wamenisahau.
Vizazi vyangu vimeniangusha mimi; rafiki zangu wa karibu wamenisahamu mimi.
15 Wageni wangu na watumishi wangu wa kike wananiona kama mgeni; wananitazama kama mgeni.
Wale ambao mwanzoni walikaa kama wageni ndani ya nyumba yangu na watumishi wangu wa kike, hunihesabu mimi kama mgeni. Mimi nimekuwa mgeni katika macho yao.
16 Namwita mtumishi wangu, wala haitiki, ingawa namwomba kwa kinywa changu mwenyewe.
Mimi ninamwita mtumishi wangu, lakini yeye hanipi jibu japokuwa Mimi nimemsihi yeye kwa midomo yangu.
17 Pumzi ya kinywa changu ni kinyaa kwa mke wangu; nimekuwa chukizo mno kwa ndugu zangu mwenyewe.
Pumzi yangu mimi ni chukizo kwa mke wangu; Hata mimi ninachukiwa na wale ambao walizaliwa kutoka katika tumbo la mama yangu mimi.
18 Hata watoto wadogo hunidhihaki; ninapojitokeza, hunifanyia mzaha.
Hata watoto wachanga wananichukia mimi; ikiwa Mimi nitainuka kuzungumza, wao huzungumza dhidi yangu mimi.
19 Rafiki zangu wa moyoni wote wananichukia kabisa; wale niwapendao wamekuwa kinyume nami.
Rafiki zangu wote ninaowazoea wananichukia sana mimi; wale ambao Mimi ninawapenda wamegeuka kinyume na mimi.
20 Mimi nimebaki mifupa na ngozi tu; nimeponea nikiwa karibu kufa.
Mifupa yangu inashikamana kwenye ngozi yangu na kwenye mwili wangu; Mimi ninaishi tu kwa ngozi ya meno yangu.
21 “Nihurumieni, rafiki zangu, kuweni na huruma, kwa kuwa mkono wa Mungu umenipiga.
Iweni na huruma juu yangu mimi, muwe na huruma juu yangu mimi, rafiki zangu, kwa maana mkono wa Mungu umenigusa mimi.
22 Kwa nini mnanifuatia kama Mungu afanyavyo? Hamtosheki kamwe na mwili wangu?
Kwa nini mnanitesa mimi kama ninyi mlikuwa Mungu? kwa nini hamjatosheka bado kwa kula mwili wangu?
23 “Laiti maneno yangu yangewekwa kwenye kumbukumbu, laiti kwamba yangeandikwa kwenye kitabu,
Laiti, hayo maneno yangu yangekuwa yameandikwa chini! Laiti, hayo yangekuwa yameandikwa katika kitabu!
24 kwamba yangechorwa kwenye risasi kwa kifaa cha chuma, au kuyachonga juu ya mwamba milele!
Laiti, kwa kalamu ya chuma na risasi hayo yangekuwa yamechorwa katika mwamba siku zote!
25 Ninajua kwamba Mkombozi wangu yu hai, naye kwamba mwishoni atasimama juu ya nchi.
Lakini kama ilivyo kwangu mimi, Mimi ninafahamu kwamba mkombozi wangu anaishi, na kwamba hata mwisho atasimama katika nchi;
26 Nami baada ya ngozi yangu kuharibiwa, bado nikiwa na mwili huu nitamwona Mungu;
baada ya ngozi yangu, hivyo ndivyo, mwili huu, unaharibiwa, ndipo katika mwili wangu mimi Nitamwona Mungu.
27 mimi nitamwona kwa macho yangu mwenyewe: mimi, wala si mwingine. Tazama jinsi moyo wangu unavyomtamani sana!
Mimi nitamwona yeye kwa macho yangu mwenyewe-Mimi, na siyo mtu mwingine. Moyo wangu hushindwa ndani yangu mimi.
28 “Kama mkisema, ‘Tazama tutakavyomwinda, maadamu mzizi wa tatizo uko ndani yake,’
Kama mnatasema, 'Kwa jinsi gani tutamtesa yeye? Mzizi wa mahangaiko yake unakaa katika yeye;
29 ninyi wenyewe uogopeni upanga, kwa kuwa ghadhabu italeta adhabu kwa upanga, nanyi ndipo mtakapojua kwamba kuna hukumu.”
ndipo uwe umeogopeshwa kwa ule upanga, kwa sababu ghadhabu huleta hukumu ya upanga, hivyo kwamba wewe uweze kutambua kuna hukumu.”

< Ayubu 19 >