< Ayubu 19 >

1 Ndipo Ayubu akajibu:
ויען איוב ויאמר
2 “Je, mtaendelea kunitesa mpaka lini, na kuniponda kwa maneno yenu?
עד-אנה תוגיון נפשי ותדכאונני במלים
3 Mara kumi hizi mmenishutumu; bila aibu mnanishambulia.
זה עשר פעמים תכלימוני לא-תבשו תהכרו-לי
4 Kama ni kweli nimepotoka, kosa langu ninabaki kuhusika nalo mwenyewe.
ואף-אמנם שגיתי אתי תלין משוגתי
5 Kama kweli mngejitukuza wenyewe juu yangu, na kutumia unyonge wangu dhidi yangu,
אם-אמנם עלי תגדילו ותוכיחו עלי חרפתי
6 basi jueni kuwa Mungu amenitendea yaliyo mabaya, naye amekokota wavu wake kunizunguka.
דעו-אפו כי-אלוה עותני ומצודו עלי הקיף
7 “Ingawa ninalia, ‘Nimetendewa mabaya!’ sipati jibu; ingawa ninaomba msaada, hakuna haki.
הן אצעק חמס ולא אענה אשוע ואין משפט
8 Yeye ameizuia njia yangu hivyo siwezi kupita; ameyafunika mapito yangu na giza.
ארחי גדר ולא אעבור ועל נתיבותי חשך ישים
9 Amenivua heshima yangu, na kuniondolea taji kichwani pangu.
כבודי מעלי הפשיט ויסר עטרת ראשי
10 Amenibomoa kila upande hadi nimeisha; amelingʼoa tegemeo langu kama mti.
יתצני סביב ואלך ויסע כעץ תקותי
11 Hasira yake imewaka juu yangu; amenihesabu kuwa miongoni mwa adui zake.
ויחר עלי אפו ויחשבני לו כצריו
12 Majeshi yake yananisogelea kwa nguvu; yamenizingira, yamepiga kambi kulizunguka hema langu.
יחד יבאו גדודיו--ויסלו עלי דרכם ויחנו סביב לאהלי
13 “Amewatenga ndugu zangu mbali nami; wale tunaojuana nao wamefarakana nami kabisa.
אחי מעלי הרחיק וידעי אך-זרו ממני
14 Watu wa jamaa yangu wamekwenda mbali; rafiki zangu wamenisahau.
חדלו קרובי ומידעי שכחוני
15 Wageni wangu na watumishi wangu wa kike wananiona kama mgeni; wananitazama kama mgeni.
גרי ביתי ואמהתי לזר תחשבני נכרי הייתי בעיניהם
16 Namwita mtumishi wangu, wala haitiki, ingawa namwomba kwa kinywa changu mwenyewe.
לעבדי קראתי ולא יענה במו-פי אתחנן-לו
17 Pumzi ya kinywa changu ni kinyaa kwa mke wangu; nimekuwa chukizo mno kwa ndugu zangu mwenyewe.
רוחי זרה לאשתי וחנתי לבני בטני
18 Hata watoto wadogo hunidhihaki; ninapojitokeza, hunifanyia mzaha.
גם-עוילים מאסו בי אקומה וידברו-בי
19 Rafiki zangu wa moyoni wote wananichukia kabisa; wale niwapendao wamekuwa kinyume nami.
תעבוני כל-מתי סודי וזה-אהבתי נהפכו-בי
20 Mimi nimebaki mifupa na ngozi tu; nimeponea nikiwa karibu kufa.
בעורי ובבשרי דבקה עצמי ואתמלטה בעור שני
21 “Nihurumieni, rafiki zangu, kuweni na huruma, kwa kuwa mkono wa Mungu umenipiga.
חנני חנני אתם רעי כי יד-אלוה נגעה בי
22 Kwa nini mnanifuatia kama Mungu afanyavyo? Hamtosheki kamwe na mwili wangu?
למה תרדפני כמו-אל ומבשרי לא תשבעו
23 “Laiti maneno yangu yangewekwa kwenye kumbukumbu, laiti kwamba yangeandikwa kwenye kitabu,
מי-יתן אפו ויכתבון מלי מי-יתן בספר ויחקו
24 kwamba yangechorwa kwenye risasi kwa kifaa cha chuma, au kuyachonga juu ya mwamba milele!
בעט-ברזל ועפרת-- לעד בצור יחצבון
25 Ninajua kwamba Mkombozi wangu yu hai, naye kwamba mwishoni atasimama juu ya nchi.
ואני ידעתי גאלי חי ואחרון על-עפר יקום
26 Nami baada ya ngozi yangu kuharibiwa, bado nikiwa na mwili huu nitamwona Mungu;
ואחר עורי נקפו-זאת ומבשרי אחזה אלוה
27 mimi nitamwona kwa macho yangu mwenyewe: mimi, wala si mwingine. Tazama jinsi moyo wangu unavyomtamani sana!
אשר אני אחזה-לי--ועיני ראו ולא-זר כלו כליתי בחקי
28 “Kama mkisema, ‘Tazama tutakavyomwinda, maadamu mzizi wa tatizo uko ndani yake,’
כי תאמרו מה-נרדף-לו ושרש דבר נמצא-בי
29 ninyi wenyewe uogopeni upanga, kwa kuwa ghadhabu italeta adhabu kwa upanga, nanyi ndipo mtakapojua kwamba kuna hukumu.”
גורו לכם מפני-חרב--כי-חמה עונות חרב למען תדעון שדין (שדון)

< Ayubu 19 >