< Ayubu 18 >

1 Bildadi Mshuhi akajibu:
Ndipo Bildadi Mshuhi alijibu na kusema, “
2 “Je, ni lini utafika mwisho wa maneno haya? Uwe mwenye busara, nasi ndipo tutakapoweza kuongea.
Je, lini utaacha kusema kwako? Fikiri, na baadaye tutazungumza.
3 Kwa nini sisi tunafikiriwa kama wanyama, na kuonekana wajinga machoni pako?
Kwa nini sisi tumehesabiwa kama wanyama mwitu; kwa nini tumekuwa wapumbavu machoni pako?
4 Wewe unayejirarua mwenyewe vipande vipande katika hasira yako, je, dunia iachwe kwa ajili yako wewe? Au ni lazima miamba iondolewe mahali pake?
Wewe ambaye wajirarua mwenyewe katika hasira yako, nchi haipaswi kuachwa kwa ajili yako au miamba inapaswa kuondolewa kutoka mahali pake?
5 “Taa ya mwovu imezimwa, nao mwali wa moto wake umezimika.
Ni dhahiri, nuru ya watu waovu itawekwa nje; cheche ya moto wake haitanga'ra.
6 Mwanga hemani mwake umekuwa giza; taa iliyo karibu naye imezimika.
Nuru itakuwa giza katika hema yake; taa yake juu yake yeye itawekwa nje.
7 Nguvu za hatua zake zimedhoofishwa; shauri lake baya litamwangusha.
Hatua za nguvu zake yeye zitafanywa kuwa fupi; mipango yake yeye mwenyewe itamwangusha yeye chini.
8 Miguu yake imemsukumia kwenye wavu, naye anatangatanga kwenye matundu ya wavu.
Kwa maana yeye atatupwa katika mtego kwa miguu yake mwenyewe; yeye atatembea katika mahangaiko.
9 Tanzi litamkamata kwenye kisigino; mtego utamshikilia kwa nguvu.
Tanzi litamchukua yeye kwa kisigino; mtego utabaki kushikilia juu yake.
10 Kitanzi kimefichwa ardhini kwa ajili yake; mtego uko kwenye njia yake.
Tanzi limefichwa kwa ajili yake chini ya ardhi; na mtego kwa ajili yake katika njia.
11 Vitisho vimemtia hofu kila upande, na adui zake humwandama kila hatua.
Watishao watamfanya yeye aogope juu ya sehemu zote; wao watamkimbiza yeye kwenye visigino vyake.
12 Janga linamwonea shauku; maafa yako tayari kwa ajili yake aangukapo.
Utajiri wake utageuka kuwa njaa, na majanga yatakuwa tayari upande wake.
13 Nayo yatakula sehemu ya ngozi yake; mzaliwa wa kwanza wa mauti atakula maungo yake.
Sehemu za mwili wake zitakuwa zimemezwa; Hakika, mzaliwa wa kwanza wa kifo atazila sehemu zake yeye.
14 Atangʼolewa kutoka usalama wa hema lake, na kupelekwa kwa mfalme wa vitisho.
Yeye ameraruliwa kutoka kwenye usalama wa hema yake na hakuweza kutembea kwenda kwa mfalme mwenye utisho.
15 Moto utakaa katika hema lake; moto wa kiberiti utamwagwa juu ya makao yake.
Watu ambao siyo wa kwake wataishi kwenye hema yake baada ya kuona ule moto mesambaa ndani ya nyumba yake yeye.
16 Mizizi yake chini itakauka na matawi yake juu yatanyauka.
Mizizi yake itanyauka chini yake; juu tawi lake yeye litakatwa.
17 Kumbukumbu lake litatoweka katika dunia, wala hatakuwa na jina katika nchi.
Kumbukumbu lake yeye litapotea kutoka katika nchi; yeye hatakuwa na jina katika mtaa.
18 Ameondolewa nuruni na kusukumiwa gizani, naye amefukuzwa mbali atoke duniani.
Yeye atafukuzwa kutoka katika nuru mpaka kwenye giza na kuwa amefukuzwa nje na ulimwengu huu.
19 Hana mtoto wala mzao miongoni mwa watu wake, wala aliyenusurika mahali alipoishi.
Hatakuwa na mtoto wa kiume wala mjukuu miongonni mwa watu wake, wala kizazi chochote kitakachobakia mahali alipokuwa amekaa.
20 Watu wa magharibi watashangaa yaliyompata; watu wa mashariki watapatwa na hofu.
Wale wanaoishi upande wa magharibi watakuwa wametiwa hofu kwa kile kitakachotokea kwake siku moja; wale wanaoishi upande wa mashariki watakuwa wameogopeshwa kwa hicho.
21 Hakika ndivyo yalivyo makao ya mtu mwovu; ndivyo palivyo mahali pake mtu asiyemjua Mungu.”
Hakika hizo ni nyumba za watu wasio haki, ni sehemu ya wale wasiomjua Mungu.”

< Ayubu 18 >