< Ayubu 17 >
1 Moyo wangu umevunjika, siku zangu zimefupishwa, kaburi linaningojea.
Roho yangu imemezwa, na siku zangu zimekwisha; kaburi lipo tayari kwa ajili yangu mimi.
2 Hakika wenye mizaha wamenizunguka; macho yangu yamebaki kutazama uadui wao.
Hakika kuna wenye mzaha pamoja nami; ni lazima daima jicho langu litazame kukasirisha kwao.
3 “Ee Mungu, nipe dhamana unayodai. Ni nani mwingine atakayeweka dhamana kwa ajili yangu?
Nipe sasa ahadi, uwe uthibitisho kwangu mimi pamoja na wewe mwenyewe; nani mwingine yuko pale ambaye atanisaidia mimi?
4 Umezifunga akili zao zisipate ufahamu, kwa hiyo hutawaacha wapate ushindi.
Kwa kuwa wewe Mungu umemeitunza mioyo yao kutoka katika ufahamu; kwa hiyo, wewe hautawaheshimisha wao juu yangu mimi.
5 Kama mtu akiwashutumu rafiki zake ili apate ujira, macho ya watoto wake yatashindwa kuona.
Yeye ambaye huwapinga rafiki zake hadharani, kwa ajili ya tuzo, macho ya watoto wake yatashindwa kuona.
6 “Mungu amenifanya kitu cha dhihaka kwa kila mtu, mtu ambaye watu humtemea mate usoni.
Lakini amenifanya mimi kuwa neno la kuzungumziwa na watu; wao wananitemea mate katika uso wangu mimi.
7 Macho yangu yamefifia kwa ajili ya majonzi; umbile langu lote ni kama kivuli.
Jicho langu pia halioni vizuri kwa sababu ya huzuni; sehemu zangu zote za mwili ni nyembamba kama vivuli.
8 Watu wanyofu wanatishwa na hili; watu wasio na hatia wanasimama dhidi ya wasiomcha Mungu.
Watu wanyoofu watapendezwa na hiki; mtu asiye na hatia atajitia yeye mwenyewe juu ya kushindana dhidi ya watu wasiomcha Mungu.
9 Hata hivyo, waadilifu watazishika njia zao, nao wale wenye mikono safi wataendelea kupata nguvu.
Mtu mwenye haki ataendelea katika njia yake; yeye ambaye ana mikono iliyo safi ataendelea kuwa mwenye nguvu zaidi na zaidi.
10 “Lakini ninyi njooni, ninyi nyote, jaribuni tena! Sitampata mtu mwenye hekima miongoni mwenu.
Lakini kama ilivyo kwenu ninyi nyote, njooni sasa; Mimi sitampata mtu mwenye hekima miongoni mwenu ninyi.
11 Siku zangu zimepita, mipango yangu imevunjika, vivyo hivyo shauku za moyo wangu.
Siku zangu zimepita; mipango yangu imenyamazishwa na hivyo ni matumaini ya moyo wangu.
12 Watu hawa hufanya usiku kuwa mchana, kwenye giza wao husema, ‘Mwanga u karibu.’
Watu hawa, wenye kukejeli, badili usiku kuwa mchana; mchana uko karibu kuwa giza.
13 Kama nyumba pekee ninayoitarajia ni kaburi, kama nikikitandika kitanda changu gizani, (Sheol )
Tangu mimi nitazame katika Kuzimu kama nyumbani kwangu; tangu Mimi nimetandaza kiti changu katika giza; (Sheol )
14 kama nikiuambia uharibifu, ‘Wewe u baba yangu,’ na kuliambia buu, ‘Wewe u mama yangu’ au ‘Dada yangu,’
tangu Mimi nimesema na shimo 'Wewe ni baba yangu,' na kwa funza, 'Wewe ni mama yangu au dada yangu;
15 liko wapi basi tarajio langu? Ni nani awezaye kuona tarajio lolote kwa ajili yangu?
liko wapi tena tumaini langu? Kama kwa tumaini langu, nani awezaye kuona chochote?
16 Je, litashuka chini hadi kwenye malango ya mauti? Je, tutashuka pamoja mavumbini?” (Sheol )
Tumaini litakwenda pamoja na mimi katika milango ya Kuzimu wakati sisi tutakapokwenda katika mavumbi? (Sheol )