< Ayubu 17 >

1 Moyo wangu umevunjika, siku zangu zimefupishwa, kaburi linaningojea.
רוחי חבלה ימי נזעכו קברים לי
2 Hakika wenye mizaha wamenizunguka; macho yangu yamebaki kutazama uadui wao.
אם-לא התלים עמדי ובהמרותם תלן עיני
3 “Ee Mungu, nipe dhamana unayodai. Ni nani mwingine atakayeweka dhamana kwa ajili yangu?
שימה-נא ערבני עמך מי הוא לידי יתקע
4 Umezifunga akili zao zisipate ufahamu, kwa hiyo hutawaacha wapate ushindi.
כי-לבם צפנת משכל על-כן לא תרמם
5 Kama mtu akiwashutumu rafiki zake ili apate ujira, macho ya watoto wake yatashindwa kuona.
לחלק יגיד רעים ועיני בניו תכלנה
6 “Mungu amenifanya kitu cha dhihaka kwa kila mtu, mtu ambaye watu humtemea mate usoni.
והציגני למשל עמים ותפת לפנים אהיה
7 Macho yangu yamefifia kwa ajili ya majonzi; umbile langu lote ni kama kivuli.
ותכה מכעש עיני ויצרי כצל כלם
8 Watu wanyofu wanatishwa na hili; watu wasio na hatia wanasimama dhidi ya wasiomcha Mungu.
ישמו ישרים על-זאת ונקי על-חנף יתערר
9 Hata hivyo, waadilifu watazishika njia zao, nao wale wenye mikono safi wataendelea kupata nguvu.
ויאחז צדיק דרכו וטהר-ידים יסיף אמץ
10 “Lakini ninyi njooni, ninyi nyote, jaribuni tena! Sitampata mtu mwenye hekima miongoni mwenu.
ואולם--כלם תשבו ובאו נא ולא-אמצא בכם חכם
11 Siku zangu zimepita, mipango yangu imevunjika, vivyo hivyo shauku za moyo wangu.
ימי עברו זמתי נתקו-- מורשי לבבי
12 Watu hawa hufanya usiku kuwa mchana, kwenye giza wao husema, ‘Mwanga u karibu.’
לילה ליום ישימו אור קרוב מפני-חשך
13 Kama nyumba pekee ninayoitarajia ni kaburi, kama nikikitandika kitanda changu gizani, (Sheol h7585)
אם-אקוה שאול ביתי בחשך רפדתי יצועי (Sheol h7585)
14 kama nikiuambia uharibifu, ‘Wewe u baba yangu,’ na kuliambia buu, ‘Wewe u mama yangu’ au ‘Dada yangu,’
לשחת קראתי אבי אתה אמי ואחתי לרמה
15 liko wapi basi tarajio langu? Ni nani awezaye kuona tarajio lolote kwa ajili yangu?
ואיה אפו תקותי ותקותי מי ישורנה
16 Je, litashuka chini hadi kwenye malango ya mauti? Je, tutashuka pamoja mavumbini?” (Sheol h7585)
בדי שאל תרדנה אם-יחד על-עפר נחת (Sheol h7585)

< Ayubu 17 >