< Ayubu 14 >

1 “Mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke siku zake ni chache nazo zimejaa taabu.
“Man, who is born of woman, is short of days and full of trouble.
2 Huchanua kama ua kisha hunyauka; huwa kama kivuli kipitacho upesi, wala hadumu.
Like a flower, he comes forth, then withers away; like a fleeting shadow, he does not endure.
3 Je, unamwekea jicho lako mtu kama huyo? Je, utamleta mbele yako katika hukumu?
Do You open Your eyes to one like this? Will You bring him into judgment before You?
4 Ni nani awezaye kutoa kitu safi kutoka kitu najisi? Hakuna awezaye!
Who can bring out clean from unclean? No one!
5 Siku za mwanadamu zimewekewa mpaka; umekwisha kutangaza idadi ya miezi yake na kuweka mpaka ambao hawezi kuuvuka.
Since his days are determined and the number of his months is with You, and since You have set limits that he cannot exceed,
6 Hivyo angalia mbali umwache, hadi awe amekamilisha muda wake kama mtu aliyeajiriwa.
look away from him and let him rest, so he can enjoy his day as a hired hand.
7 “Kwa maana lipo tumaini kwa mti; kama ukikatwa utachipuka tena, nayo machipukizi yake mapya hayatakoma.
For there is hope for a tree: If it is cut down, it will sprout again, and its tender shoots will not fail.
8 Mizizi yake yaweza kuchakaa ardhini na kisiki chake kufa udongoni,
If its roots grow old in the ground and its stump dies in the soil,
9 lakini kwa kupata dalili ya maji utachipua na kutoa machipukizi kama mche.
at the scent of water it will bud and put forth twigs like a sapling.
10 Lakini mwanadamu hufa, na huo ndio mwisho wake; hutoa pumzi ya mwisho, naye hayuko tena!
But a man dies and is laid low; he breathes his last, and where is he?
11 Kama vile maji yatowekavyo katika bahari, au mkondo wa mto ukaushwavyo na kuwa mkavu,
As water disappears from the sea and a river becomes parched and dry,
12 ndivyo mwanadamu alalavyo chini asiamke; hadi mbingu zitakapokuwa hazipo tena, wanadamu hawataamka au kuamshwa kutoka kwenye usingizi wao.
so a man lies down and does not rise. Until the heavens are no more, he will not be awakened or roused from sleep.
13 “Laiti kama ungenificha kaburini, na kunisitiri hadi hasira yako ipite! Laiti ungeniwekea wakati, na kisha ukanikumbuka! (Sheol h7585)
If only You would hide me in Sheol and conceal me until Your anger has passed! If only You would appoint a time for me and then remember me! (Sheol h7585)
14 Je, kama mtu akifa, aweza kuishi tena? Siku zote za kazi zangu ngumu nitangojea kufanywa upya kwangu.
When a man dies, will he live again? All the days of my hard service I will wait, until my renewal comes.
15 Utaniita nami nitakuitika; utakionea shauku kiumbe ambacho mikono yako ilikiumba.
You will call, and I will answer; You will desire the work of Your hands.
16 Hakika ndipo utakapozihesabu hatua zangu, lakini hutazifuatia dhambi zangu.
For then You would count my steps, but would not keep track of my sin.
17 Makosa yangu yatafungiwa kwa lakiri kwenye mfuko, nawe utazifunika dhambi zangu.
My transgression would be sealed in a bag, and You would cover over my iniquity.
18 “Lakini kama mlima umomonyokavyo na kufikichika na kama vile mwamba uondolewavyo mahali pake,
But as a mountain erodes and crumbles and a rock is dislodged from its place,
19 kama maji yamalizavyo mawe, na mafuriko yachukuavyo udongo, ndivyo unavyoharibu tegemeo la mwanadamu.
as water wears away the stones and torrents wash away the soil, so You destroy a man’s hope.
20 Humshinda mara moja kwa daima, naye hutoweka; waibadilisha sura yake na kumwondoa.
You forever overpower him, and he passes on; You change his countenance and send him away.
21 Kama wanawe wakipewa heshima, yeye hafahamu; kama wakidharauliwa, yeye haoni.
If his sons receive honor, he does not know it; if they are brought low, he is unaware.
22 Yeye hasikii kingine isipokuwa maumivu ya mwili wake mwenyewe, naye huomboleza kwa ajili yake mwenyewe.”
He feels only the pain of his own body and mourns only for himself.”

< Ayubu 14 >