< Ayubu 13 >
1 “Macho yangu yameona hili lote, masikio yangu yamesikia na kulielewa.
Tazama, jicho langu limeyaona haya yote; sikio langu limeyasikia na kuyaelewa hayo.
2 Hayo mnayoyajua mimi pia ninayajua; mimi si mtu duni kuliko ninyi.
Kile mnachokifahamu, ndicho hicho mimi pia ninachokifahamu; Mimi siyo duni kwenu ninyi.
3 Lakini ninayo shauku ya kuzungumza na Mwenyezi na kuhojiana shauri langu na Mungu.
Hata hivyo, Mimi ningeweza kuzungumza na mwenye nguvu; Mimi natamani kusemezana na Mungu.
4 Ninyi, hata hivyo, hunipakaza uongo; ninyi ni matabibu wasiofaa kitu, ninyi nyote!
Lakini ninyi mnauficha ukweli kwa uongo; ninyi nyote ni tabibu msiokuwa na thamani.
5 Laiti wote mngenyamaza kimya! Kwa kuwa kwenu hilo lingekuwa hekima.
Laiti, kwamba kwa pamoja mngeshikilia amani yenu! Hilo lingekuwa hekima yenu ninyi.
6 Sikieni sasa hoja yangu; sikilizeni kusihi kwangu.
Sikia sasa kuhoji kwangu; Sikiliza kusihi kwa midomo yangu mwenyewe.
7 Je, mtazungumza kwa uovu kwa niaba ya Mungu? Je, mtazungumza kwa udanganyifu kwa niaba yake?
Ninyi mtazungumza visivyo haki kwa ajili ya Mungu, na ninyi mtazungumza udanganyifu kwa yeye? Ni kweli ninyi mngeonyesha ukarimu kwa yeye?
8 Mtamwonyesha upendeleo? Mtamtetea Mungu kwenye mashtaka yake?
Ni kweli ninyi mngetetea katika mahakama kama mawakili wa Mungu?
9 Je, ingekuwa vyema Mungu akiwahoji ninyi? Je, mngeweza kumdanganya kama ambavyo mngeweza kuwadanganya wanadamu?
Je, kweli ingekuwa vizuri kwenu wakati yeye akiwatafuta ninyi? Mngeweza ninyi kumdanganya yeye kama mlivyoweza kuwadanganya watu?
10 Hakika angewakemea kama mkiwapendelea watu kwa siri.
Yeye kwa hakika angewathibitisha upya ninyi ikiwa katika siri ninyi mmeonyesha kutokukamilika.
11 Je, huo ukuu wake haungewatisha ninyi? Je, hofu yake isingewaangukia ninyi?
Je, ukuu wake usingewafanya ninyi muogope? Je, utisho wake usingeshuka juu yenu?
12 Maneno yenu ni mithali za majivu; utetezi wenu ni ngome za udongo wa mfinyanzi.
Hadithi zenu za misemo ya kukariri, ni mithali zimetengenezwa kwa majivu; utetezi wenu ni utetezi uliotengenezwa kwa udongo wa mfinyanzi.
13 “Nyamazeni kimya nipate kusema; kisha na yanipate yatakayonipata.
Shikilieni amani yenu, mniache peke yangu, ili ya kwamba nipate kusema, acheni yaje yale yanayoweza kuja kwangu.
14 Kwa nini nijiweke mwenyewe kwenye hatari na kuyaweka maisha yangu mikononi mwangu?
Nitaichukua nyama yangu mwenywewe katika meno yangu; Nitayachukua maisha yangu katika mikono yangu.
15 Ingawa ataniua, bado nitamtumaini; hakika nitazitetea njia zangu mbele zake.
Tazama, ikiwa ataniua mimi, sitakuwa na tumaini lililobakia; hata hivyo, nitazitetea njia zangu mbele zake yeye.
16 Naam, hili litanigeukia kuwa wokovu wangu, kwa maana hakuna mtu asiyemcha Mungu atakayethubutu kuja mbele yake!
Hiki kitakuwa sababu ya kutohesabiwa hatia, kwamba mimi sikuja mbele zake kama mtu asiyemcha Mungu.
17 Sikilizeni maneno yangu kwa makini; nayo masikio yenu yaingize kile nisemacho.
Mungu, sikiliza kwa makini kuzungumza kwangu; ruhusu kutangaza kwangu kuje kwenye masikio yako.
18 Sasa kwamba nimekwisha kutayarisha mambo yangu, ninajua mimi nitahesabiwa kuwa na haki.
Tazama sasa, Nimeuweka utetezi wangu katika mpangilio, Mimi ninafahamu kwamba mimi sina hatia.
19 Je, kuna yeyote anayeweza kuleta mashtaka dhidi yangu? Kama ndivyo, nitanyamaza kimya na nife.
Ni nani anayeweza kushindana na mimi katika mahakama? Ikiwa mlikuja kufanya hivyo, na kama mimi nilithibitishwa kukosea, ndipo ningekuwa kimya na kuyatoa maisha yangu.
20 “Ee Mungu, unijalie tu mimi haya mambo mawili, nami sitajificha uso wako:
Mungu, fanya mambo mawili kwa ajili yangu, na tena Mimi sitajificha kutoka katika uso wako.
21 Ondoa mkono wako uwe mbali nami, nawe uache kuniogofya kwa hofu zako kuu.
Ondoa kutoka kwangu mkono wako unaotesa, na usiache utisho wako unifanye mimi kuogopa.
22 Niite kwenye shauri nami nitajibu, au niache niseme, nawe upate kujibu.
Ndipo niite mimi, na mimi nitakujibu; au uniache mimi niseme na wewe na wewe unijibu mimi.
23 Ni makosa na dhambi ngapi nilizotenda? Nionyeshe kosa langu na dhambi yangu.
Je, maovu yangu na dhambi zangu ni ngapi? Nijulishe kosa langu na dhambi yangu.
24 Kwa nini kuuficha uso wako na kunihesabu mimi kuwa adui yako?
Kwa nini unaficha uso wako kutoka kwangu mimi na kunitendea mimi kama adui yako?
25 Je, utaliadhibu jani lipeperushwalo na upepo? Je, utayasaka makapi makavu?
Je, wewe utalitesa jani linalopeperushwa? Je, utaendelea kulifuatilia bua kavu?
26 Kwa kuwa unaandika mambo machungu dhidi yangu na kunifanya nizirithi dhambi za ujana wangu.
Kwa maana wew unaandika chini vitu vichungu dhidi yangu mimi; wewe unanifanya mimi kurithi uovu wa ujana wangu.
27 Umeifunga miguu yangu kwenye pingu. Unazichunga kwa makini njia zangu zote kwa kutia alama kwenye nyayo za miguu yangu.
Wewe pia unaiweka miguu yangu katika nguo nyembamba; wewe waangalia njia zangu zote; wewe wachunguza chini mahali ambapo nyayo za miguu yangu zimekanyaga.
28 “Hivyo mwanadamu huangamia kama kitu kilichooza, kama vazi lililoliwa na nondo.
japokuwa mimi ni kama kitu kilichooza ambacho hutupwa mbali, kama vazi lile ambalo nondo wamelila.