< Ayubu 13 >

1 “Macho yangu yameona hili lote, masikio yangu yamesikia na kulielewa.
הן-כל ראתה עיני שמעה אזני ותבן לה
2 Hayo mnayoyajua mimi pia ninayajua; mimi si mtu duni kuliko ninyi.
כדעתכם ידעתי גם-אני לא-נפל אנכי מכם
3 Lakini ninayo shauku ya kuzungumza na Mwenyezi na kuhojiana shauri langu na Mungu.
אולם--אני אל-שדי אדבר והוכח אל-אל אחפץ
4 Ninyi, hata hivyo, hunipakaza uongo; ninyi ni matabibu wasiofaa kitu, ninyi nyote!
ואולם אתם טפלי-שקר רפאי אלל כלכם
5 Laiti wote mngenyamaza kimya! Kwa kuwa kwenu hilo lingekuwa hekima.
מי-יתן החרש תחרישון ותהי לכם לחכמה
6 Sikieni sasa hoja yangu; sikilizeni kusihi kwangu.
שמעו-נא תוכחתי ורבות שפתי הקשיבו
7 Je, mtazungumza kwa uovu kwa niaba ya Mungu? Je, mtazungumza kwa udanganyifu kwa niaba yake?
הלאל תדברו עולה ולו תדברו רמיה
8 Mtamwonyesha upendeleo? Mtamtetea Mungu kwenye mashtaka yake?
הפניו תשאון אם-לאל תריבון
9 Je, ingekuwa vyema Mungu akiwahoji ninyi? Je, mngeweza kumdanganya kama ambavyo mngeweza kuwadanganya wanadamu?
הטוב כי-יחקר אתכם אם-כהתל באנוש תהתלו בו
10 Hakika angewakemea kama mkiwapendelea watu kwa siri.
הוכח יוכיח אתכם-- אם-בסתר פנים תשאון
11 Je, huo ukuu wake haungewatisha ninyi? Je, hofu yake isingewaangukia ninyi?
הלא שאתו תבעת אתכם ופחדו יפל עליכם
12 Maneno yenu ni mithali za majivu; utetezi wenu ni ngome za udongo wa mfinyanzi.
זכרניכם משלי-אפר לגבי-חמר גביכם
13 “Nyamazeni kimya nipate kusema; kisha na yanipate yatakayonipata.
החרישו ממני ואדברה-אני ויעבר עלי מה
14 Kwa nini nijiweke mwenyewe kwenye hatari na kuyaweka maisha yangu mikononi mwangu?
על-מה אשא בשרי בשני ונפשי אשים בכפי
15 Ingawa ataniua, bado nitamtumaini; hakika nitazitetea njia zangu mbele zake.
הן יקטלני לא (לו) איחל אך-דרכי אל-פניו אוכיח
16 Naam, hili litanigeukia kuwa wokovu wangu, kwa maana hakuna mtu asiyemcha Mungu atakayethubutu kuja mbele yake!
גם-הוא-לי לישועה כי-לא לפניו חנף יבוא
17 Sikilizeni maneno yangu kwa makini; nayo masikio yenu yaingize kile nisemacho.
שמעו שמוע מלתי ואחותי באזניכם
18 Sasa kwamba nimekwisha kutayarisha mambo yangu, ninajua mimi nitahesabiwa kuwa na haki.
הנה-נא ערכתי משפט ידעתי כי-אני אצדק
19 Je, kuna yeyote anayeweza kuleta mashtaka dhidi yangu? Kama ndivyo, nitanyamaza kimya na nife.
מי-הוא יריב עמדי כי-עתה אחריש ואגוע
20 “Ee Mungu, unijalie tu mimi haya mambo mawili, nami sitajificha uso wako:
אך-שתים אל-תעש עמדי אז מפניך לא אסתר
21 Ondoa mkono wako uwe mbali nami, nawe uache kuniogofya kwa hofu zako kuu.
כפך מעלי הרחק ואמתך אל-תבעתני
22 Niite kwenye shauri nami nitajibu, au niache niseme, nawe upate kujibu.
וקרא ואנכי אענה או-אדבר והשיבני
23 Ni makosa na dhambi ngapi nilizotenda? Nionyeshe kosa langu na dhambi yangu.
כמה לי עונות וחטאות-- פשעי וחטאתי הדיעני
24 Kwa nini kuuficha uso wako na kunihesabu mimi kuwa adui yako?
למה-פניך תסתיר ותחשבני לאויב לך
25 Je, utaliadhibu jani lipeperushwalo na upepo? Je, utayasaka makapi makavu?
העלה נדף תערוץ ואת-קש יבש תרדף
26 Kwa kuwa unaandika mambo machungu dhidi yangu na kunifanya nizirithi dhambi za ujana wangu.
כי-תכתב עלי מררות ותורישני עונות נעורי
27 Umeifunga miguu yangu kwenye pingu. Unazichunga kwa makini njia zangu zote kwa kutia alama kwenye nyayo za miguu yangu.
ותשם בסד רגלי-- ותשמור כל-ארחתי על-שרשי רגלי תתחקה
28 “Hivyo mwanadamu huangamia kama kitu kilichooza, kama vazi lililoliwa na nondo.
והוא כרקב יבלה כבגד אכלו עש

< Ayubu 13 >