< Ayubu 10 >

1 “Nayachukia sana haya maisha yangu; kwa hiyo nitatoa malalamiko yangu kwa wazi bila kujizuia, nami nitanena kutokana na uchungu wa moyo wangu.
נקטה נפשי בחיי אעזבה עלי שיחי אדברה במר נפשי׃
2 Nitamwambia Mungu: Usinihukumu, bali niambie una mashtaka gani dhidi yangu.
אמר אל אלוה אל תרשיעני הודיעני על מה תריבני׃
3 Je, inakupendeza wewe kunionea, kuikataa kwa dharau kazi ya mikono yako, huku wewe ukitabasamu juu ya mipango ya waovu?
הטוב לך כי תעשק כי תמאס יגיע כפיך ועל עצת רשעים הופעת׃
4 Je, wewe una macho ya kimwili? Je, wewe huona kama mwanadamu aonavyo?
העיני בשר לך אם כראות אנוש תראה׃
5 Je, siku zako ni kama zile za mwanadamu, au miaka yako ni kama ile ya mtu,
הכימי אנוש ימיך אם שנותיך כימי גבר׃
6 ili kwamba utafute makosa yangu na kuichunguza dhambi yangu;
כי תבקש לעוני ולחטאתי תדרוש׃
7 ingawa wajua kuwa mimi sina hatia, na hakuna awezaye kunitoa mkononi mwako?
על דעתך כי לא ארשע ואין מידך מציל׃
8 “Mikono yako ndiyo iliyoniumba na kunifanya. Je, sasa utageuka na kuniangamiza?
ידיך עצבוני ויעשוני יחד סביב ותבלעני׃
9 Kumbuka kuwa ulinifinyanga kama udongo wa mfinyanzi. Je, sasa utanifanya kuwa mavumbi tena?
זכר נא כי כחמר עשיתני ואל עפר תשיבני׃
10 Je, wewe hukunimimina mimi kama maziwa, na kunigandisha kama jibini,
הלא כחלב תתיכני וכגבנה תקפיאני׃
11 ukanivika ngozi na nyama, na kuniunga pamoja kwa mifupa na mishipa?
עור ובשר תלבישני ובעצמות וגידים תסככני׃
12 Umenipa uhai na kunitendea wema, katika uangalizi wako umeilinda roho yangu.
חיים וחסד עשית עמדי ופקדתך שמרה רוחי׃
13 “Lakini hili ndilo ulilolificha moyoni mwako, nami ninajua kuwa hili lilikuwa katika nia yako:
ואלה צפנת בלבבך ידעתי כי זאת עמך׃
14 Kama nilifanya dhambi, ungekuwa umeniona, wala usingeacha kosa langu lipite bila kuadhibiwa.
אם חטאתי ושמרתני ומעוני לא תנקני׃
15 Kama nina hatia, ole wangu! Hata kama ningekuwa sina hatia, siwezi kukiinua kichwa changu, kwa kuwa nimejawa na aibu, na kuzama katika mateso yangu.
אם רשעתי אללי לי וצדקתי לא אשא ראשי שבע קלון וראה עניי׃
16 Kama nikiinua kichwa changu juu, unaninyatia kama simba, na kuonyesha tena uwezo wa kutisha dhidi yangu.
ויגאה כשחל תצודני ותשב תתפלא בי׃
17 Wewe waleta mashahidi wapya dhidi yangu na kuzidisha hasira yako juu yangu; nazo nguvu zako zinanijia wimbi moja baada ya jingine.
תחדש עדיך נגדי ותרב כעשך עמדי חליפות וצבא עמי׃
18 “Kwa nini basi ulinitoa tumboni? Ninatamani ningekufa kabla jicho lolote halijaniona.
ולמה מרחם הצאתני אגוע ועין לא תראני׃
19 Laiti nisingekuwako kamwe, au ningekuwa nimechukuliwa moja kwa moja kutoka tumboni kwenda kaburini!
כאשר לא הייתי אהיה מבטן לקבר אובל׃
20 Je, siku zangu chache si zimekaribia kuisha? Niachie ili niweze kupata muda mfupi wa kufurahi
הלא מעט ימי יחדל ישית ממני ואבליגה מעט׃
21 kabla sijaenda mahali ambapo hakuna kurudi tena, katika nchi ya giza na uvuli wa mauti,
בטרם אלך ולא אשוב אל ארץ חשך וצלמות׃
22 nchi ya giza kuu sana, yenye uvuli wa giza na machafuko, mahali ambapo hata nuru ni giza.”
ארץ עפתה כמו אפל צלמות ולא סדרים ותפע כמו אפל׃

< Ayubu 10 >