< Yeremia 1 >

1 Maneno ya Yeremia mwana wa Hilkia, mmoja wa makuhani katika mji wa Anathothi, katika nchi ya Benyamini.
Hili ndilo neno la Yeremia mwana wa Hilikia; yeye alikuwa mmoja wa makuhani kule Anatothi katika nchi ya Benjamini.
2 Neno la Bwana lilimjia katika mwaka wa kumi na tatu wa utawala wa Yosia mwana wa Amoni mfalme wa Yuda,
Neno la BWANA lilimjia katika siku za Yosia mwana wa Amoni, mfalme wa Yuda, katika mwaka wa kumi na tatu wa utawala wake.
3 na pia wakati wa utawala wa Yehoyakimu mwana wa Yosia mfalme wa Yuda, mpaka mwezi wa tano wa mwaka wa kumi na moja wa utawala wa Sedekia mwana wa Yosia mfalme wa Yuda, wakati watu wa Yerusalemu walipopelekwa uhamishoni.
Lakini pia lilimjia katika wakati wa Yehoyakimu mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda, mpaka mwezi wa tano wa mwaka wa kumi na moja wa Zedekia mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda, wakati watu wa Yerusalemu walipochukuliwa kuwa watumwa.
4 Neno la Bwana lilinijia, kusema,
Neno la BWANA lilinijia, likisema,
5 “Kabla sijakuumba ndani ya tumbo la mama yako, nilikujua; kabla hujazaliwa nilikutenga kwa kazi maalum; nilikuweka uwe nabii kwa mataifa.”
“kabla sijakuumba tumboni, Nilikuchagua; kabla hujazailiwa toka tumboni Nilikutenga; Nilikufanya kuwa nabii kwa mataifa.”
6 Nami nikasema, “Aa, Bwana Mwenyezi, sijui kusema, kwani mimi ni mtoto mdogo tu.”
“Ahaa, BWANA!” Nilisema, “mimi sijui kusema, kwa kuwa mimi ni mtoto.”
7 Lakini Bwana akaniambia, “Usiseme, ‘Mimi ni mtoto mdogo tu.’ Utaenda popote nitakapokutuma na kunena lolote nitakalokuagiza.
Lakini BWANA akaniambia, “Usiseme, 'mimi ni mtoto.' Utaenda kila mahali ninapokutuma, na utasema kila kitu ninachokuamuru!
8 Usiwaogope, kwa maana niko pamoja nawe nikuokoe,” asema Bwana.
Usiwaogpe hao, kwa kuwa Mimi niko pamoja na wewe kukuokoa- asema BWANA.”
9 Kisha Bwana akaunyoosha mkono wake na kugusa kinywa changu, akaniambia, “Sasa nimeyaweka maneno yangu kinywani mwako.
Kisha BWANA akanyosh mkono wake, akagusa kinywa changu, na akaniambia, “Nimeweka maneno yangu kinywani mwako.
10 Tazama, leo nimekuweka juu ya mataifa na falme ili kungʼoa na kubomoa, kuharibu na kuangamiza, kujenga na kupanda.”
Nimekuchagua leo juu ya mataifa na juu ya mataifa, ili kung'oa na kuvunja, kuharibu na kutupa, kujenga na kupanda.”
11 Neno la Bwana likanijia kusema, “Je, Yeremia unaona nini?” Nami nikajibu, “Naona tawi la mti wa mlozi.”
Neno la BWANA lilinijia, likisema, “Yeremia, unaona nini?” Nikasema, “Ninaona tawi la mlozi.”
12 Bwana akaniambia, “Umeona vyema kwa maana ninaliangalia neno langu ili kuona kwamba limetimizwa.”
BWANA akaniambia, “umeona vyema, kwa kuwa ninaliangalia neno langu ili nilitimize.”
13 Neno la Bwana likanijia tena, “Unaona nini?” Nikajibu, “Naona chungu kinachochemka, kikiwa kimeinama kutoka kaskazini.”
Neno la BWANA likaniji mara ya pili likisema, “Unaona nini? “Nikasema, “Ninaona chungu kikichemuka, ambacho mdomo wake unaelekea toka upande wa kaskazini,”
14 Bwana akaniambia, “Kutoka kaskazini maafa yatamwagwa kwa wote waishio katika nchi.
BWANA akaniambia, “Janga litatokea kaskazini juu ya wote wanaoishi katika nchi hii.
15 Nitawaita watu wote wa falme za kaskazini,” asema Bwana. “Wafalme wao watakuja na kuweka viti vyao vya enzi katika maingilio ya malango ya Yerusalemu, watakuja dhidi ya kuta zake zote zinazouzunguka, na dhidi ya miji yote ya Yuda.
Kwa kuwa ninayaita makabila yote ya falme za kaskazini, asema BWANA. Yatakuja, na kila mmoja atasimika enzi yake katika malango ya Yerusalemu, dhidi ya kuta zote zinazoizunguka, na dhidi ya miji ya Yuda.
16 Nitatoa hukumu zangu kwa watu wangu kwa sababu ya uovu wao wa kuniacha mimi, kwa kufukiza uvumba kwa miungu mingine na kuabudu kile ambacho mikono yao imekitengeneza.
Nitatamka hukumu dhidi yao juu ya uovu wao wa kuniacha, kwa kufukiza uvumba kwa miungu mingine, na kwa kuabudu kile walichotengeneza kwa mikono yao.
17 “Jiandae! Simama useme chochote nitakachokuamuru. Usiwaogope, la sivyo nitakufanya uwaogope wao.
Jiandae! Simama ukawaambie kila kitu ninachokuamuru. Usifdhaike mbele zao nisije nikakufadhaisha wewe mbele zao!
18 Leo nimekufanya mji wenye ngome, nguzo ya chuma, na ukuta wa shaba ili kusimama dhidi ya nchi yote: dhidi ya wafalme wa Yuda, maafisa wake, makuhani wake na watu wa nchi hiyo.
Tazama! Leo nimekufanya kuwa mji ulio na ngome, kuwa ngome ya chuma, na ukata wa shaba dhidi ya nchi yote - dhidi ya wafalme wa Yuda, na juu ya wakuu wake, na juu ya makuhani wake, na juu ya watu wote wa nchi.
19 Watapigana nawe lakini hawatakushinda, kwa kuwa niko pamoja nawe, nami nitakuokoa,” asema Bwana.
Watapigana na wewe, lakinai hawatakushinda, kwa kuwa nitakuwa pamoja na wewe ili kukuokoa- asema BWANA.”

< Yeremia 1 >