< Yeremia 9 >
1 Laiti kichwa changu kingekuwa chemchemi ya maji na macho yangu yangekuwa kisima cha machozi! Ningelia usiku na mchana kwa kuuawa kwa watu wangu.
Kama kichwa changu kingetoa maji, na macho yangu kuwa chemichemi ya machozi! kwa kuwa natamani kulia usiku na mchana kwa ajili yao waliokuwa binti za watu wangu ambao wameuawa.
2 Laiti ningekuwa na nyumba ya kukaa wasafiri jangwani, ningewaacha watu wangu na kwenda mbali nao, kwa kuwa wote ni wazinzi, kundi la watu wadanganyifu.
Kama mtu anganipatia mahali pa wasafiri nyikani ili nikae, mahali ambapo ningeenda kuwatelekeza watu wangu. Kama ningewaacha, kwa kuwa wote ni wazinzi, kundi la wenye hiana!
3 “Huweka tayari ndimi zao kama upinde, ili kurusha uongo; wamekuwa na nguvu katika nchi lakini si katika ukweli. Wanatoka dhambi moja hadi nyingine, hawanitambui mimi,” asema Bwana.
asema BWANA, “Huupinda ulimi wao kana kwamba ni upinde ili wapate kuongea uongo, lakini si kwa uamiinifu wao kwamba wanapata nguvu duniani. Wanatoka uovu mmoja hadi mwiingine. Hawanijui mimi.”
4 “Jihadhari na rafiki zako; usiwaamini ndugu zako. Kwa kuwa kila ndugu ni mdanganyifu, na kila rafiki ni msingiziaji.
Kila mmoja wenu, awe mlinzi wa jirani yake na usimwamini hata ndugu yako yeyote. kwa kuwa kila ndugu ni mwongo,
5 Rafiki humdanganya rafiki, hakuna yeyote asemaye kweli. Wamefundisha ndimi zao kudanganya, wanajichosha wenyewe katika kutenda dhambi.
kila jirani anatembea akilaghai. Kila mwanamume anakejeli jirani yake na haongei ukweli. Ndimi zao hufundisha vitu vya uongo. Hujidhofisha ili kusema uongo.
6 Unakaa katikati ya udanganyifu; katika udanganyifu wao wanakataa kunitambua mimi,” asema Bwana.
Makazi yenu yako kati ya udanganyifu; kwa uongo wao wanakataa kunitambua mimi. Asema BWANA.”
7 Kwa hiyo hili ndilo asemalo Bwana Mwenye Nguvu Zote: “Tazama, nitawasafisha na kuwajaribu, kwani ni nini kingine niwezacho kufanya kwa sababu ya dhambi ya watu wangu?
Kwa hiyo BWANA wa majeshi asema hivi, “Tazama, Niko tayari kuwajaribu. Nitawajaribu nione. Jinsi gani niwezavyo kufanya kwa binti za watu wangu?
8 Ndimi zao ni mshale wenye sumu, hunena kwa udanganyifu. Kwa kinywa chake kila mmoja huzungumza maneno mazuri na jirani yake, lakini moyoni mwake humtegea mtego.
Ndimi zao ni mishale iliyochongoka; huongea vitu vya uasi. Kwa midomo yao wanatangaza amani pamoja na jirani zao, lakini katika mioyo yao wanadanganya wakati wa kusubri.
9 Je, nisiwaadhibu kwa ajili ya jambo hili?” asema Bwana. “Je, nisijilipizie kisasi kwa taifa kama hili?”
Kwa nini nisiwaadhibu kwa sababu ya mambo haya - asema BWANA na kwa nini nisijilipizie kisasi kwa taifa ambalo liko kama hili?
10 Nitalia na kuomboleza kwa ajili ya milima na kuomboleza kuhusu malisho ya jangwani. Yamekuwa ukiwa, wala hakuna apitaye humo, milio ya ngʼombe haisikiki. Ndege wa angani wametoroka na wanyama wamekimbia.
Nitaimba wimbo wa kuomboleza na kulia kwa ajili ya milima, na wimbo wa mazishi utaimbwa nyikani. Kwa kuwa wameteketezwa kwa hiyo hakuna anAyeweza kupita kati kati yao. Hawatasikia sauti ya ng'ombe yeyote. Ndege wa angani na wanyama wote wamekimbia.
11 “Nitaifanya Yerusalemu lundo la magofu, makao ya mbweha; nami nitaifanya miji ya Yuda kuwa ukiwa ili asiwepo atakayeishi humo.”
Kwa hiyo nitaigeuza Yerusalemu kuwa vifusi vya ukiwa, maficho ya mbweha. Nitaifanya miji ya Yuda kuwa miji iliyoharibiwa isiyokaliwa na watu.
12 Ni mtu yupi aliye na hekima ya kutosha ayaelewe haya? Ni nani aliyefundishwa na Bwana awezaye kuyaeleza haya? Kwa nini nchi imeharibiwa na kufanywa ukiwa kama jangwa ambapo hakuna awezaye kupita?
Ni nani mwenye hekima anayeyaelewa haya? Je, kinywa cha BWANA kinatangaza nini kwake ili aweze kuyasema? Kwa nini nchi imepotea? Imeharibiwa kama jangwa, ambapo hakuna apitaye kati kati yake.
13 Bwana akasema, “Ni kwa sababu wameiacha sheria yangu, niliyoiweka mbele yao: hawajaniheshimu mimi wala kufuata sheria yangu.
BWANA asema, “Ni kwa sababu wameziacha sheria zake ambazo niliwatengenezea, kwa sababu hawaisikilizi sauti yangu au kuishi kwa kuifuta.
14 Badala yake wamefuata ukaidi wa mioyo yao, wamefuata Mabaali, kama vile baba zao walivyowafundisha.”
Ni kwa sababu wameishi kwa ushupavu wa mioyo yao na wamewafuata Mabaali kama baba zao walivyowafundisha kufanya.
15 Kwa hiyo, hivi ndivyo asemavyo Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli: “Tazama, nitawafanya watu hawa wale chakula kichungu na kunywa maji yenye sumu.
Kwa hiyo BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, 'Tazama, Ninataka kuwafanya hawa watu wale pakanga na kunywa maji ya sumu.
16 Nitawatawanya katika mataifa ambayo wao wala baba zao hawakuwajua, nikiwafuata kwa upanga mpaka niwe nimewaangamiza kabisa.”
Ndipo nitakapowasambaza kati ya mataifa ambayo hawajayajua, wao wala mababu zao. Nitatuma upanga kwa ajili yao mpaka nimewaangamiza wote kabisa.'”
17 Hivi ndivyo asemavyo Bwana Mwenye Nguvu Zote: “Fikiri sasa! Waite wanawake waombolezao waje, waite wale walio na ustadi kuliko wote.
BWANA wa majeshi asema hivi, “Yafikirini haya: Waiteni waliaji; waje. Tumeni wanawake wenye taaluma ya kuomboleza, waje.
18 Nao waje upesi na kutuombolezea, mpaka macho yetu yafurike machozi na vijito vya maji vitoke kwenye kope zetu.
Waje haraka waimbe wimbo wa maombolezo juu yetu, ili macho yetu yatokwe na machozi na kope zetu zibubujikwe na maji.
19 Sauti ya kuomboleza imesikika kutoka Sayuni: ‘Tazama jinsi tulivyoangamizwa! Tazama jinsi aibu yetu ilivyo kubwa! Ni lazima tuihame nchi yetu kwa sababu nyumba zetu zimekuwa magofu.’”
Kwa kuwa sauti ya kilio imesikika Sayuni, 'Jinsi tulivyoharibiwa. Tumeaibishwa sana, kwa kuwa tumeitelekeza nchi tangu walIpoangusha nyumba zetu.'
20 Basi, enyi wanawake, sikieni neno la Bwana; fungueni masikio yenu msikie maneno ya kinywa chake. Wafundisheni binti zenu kuomboleza; fundishaneni kila mmoja na mwenzake maombolezo.
Kwa hiyo ninyi wanawake, sikieni neno la BWANA; zingatieni ujumbe unaokuja toka kinywani mwake. Kisha wafundisheni binti zenu wimbo wa maombolezo, na kila mwanamke wa jirani wimbo wa kilio.
21 Mauti imeingia ndani kupitia madirishani, imeingia kwenye majumba yetu ya fahari; imewakatilia mbali watoto katika barabara na vijana waume kutoka viwanja vya miji.
Kwa kuwa vifo vimekuja kupitia dirishani; vinaelekea mahali petu. Vinawaharibu watoto kutoka nje na vijana kwenye viwanja vya miji.
22 Sema, “Hili ndilo asemalo Bwana: “‘Maiti za wanaume zitalala kama mavi katika mashamba, kama malundo ya nafaka nyuma ya mvunaji, wala hakuna anayekusanya.’”
Uyatangaze haya, 'Asema BWANA - mizoga ya wanaume itaanguka kama mavi kwenye mashamba na kama mabua baada ya mvunaji, na hapatakuwa na mtu wa kuyakusanya.'”
23 Hili ndilo asemalo Bwana: “Mwenye hekima asijisifu katika hekima yake, au mwenye nguvu ajisifu katika nguvu zake, wala tajiri ajisifu katika utajiri wake,
BWANA asema hivi, “Usimwache mtu mwenye busara ajivune kwa ajili ya hekima yake, au shujaa kwa sababu ya uwezo wake. Usimwache mtu tajiri ajivunie utajiri wake.
24 lakini yeye ajisifuye, na ajisifu kwa sababu hili: kwamba ananifahamu na kunijua mimi, kwamba mimi ndimi Bwana, nitendaye wema, hukumu na haki duniani, kwa kuwa napendezwa na haya,” asema Bwana.
Kwa kuwa kama mtu atajivunia chochote kile, acha iwe hivi, yeye awe na busra na kunijua mimi. Kwa kuwa mimi ni BWANA, atendaye katika agano la wema, haki, na hukumu duniani. Ni katika hili kwamba ninafurahia- asema BWANA.
25 “Siku zinakuja, nitakapowaadhibu wale wote ambao wametahiriwa kimwili tu, asema Bwana,
Tazama, siku zaja - asema BWANA wakati nitakapowaadhibu wote ambao hawajatahiriwa ambao wako hivyo hivyo katika miili yao.
26 yaani Misri, Yuda, Edomu, Amoni, Moabu na wote wanaoishi jangwani sehemu za mbali. Kwa maana mataifa haya yote hayakutahiriwa mioyo yao, nayo nyumba yote ya Israeli haikutahiriwa.”
Nitaiadhibu Misri na Yuda, Edomu, watu wa Amoni, Moabu, na watu wote wanaonyoa denge. Kwani mataifa yote haya hayajatahiriwa, na nyumba yote ya Israeli ina moyo ambao haujatahiriwa.”