< Yeremia 50 >

1 Hili ndilo neno alilosema Bwana kupitia nabii Yeremia kuhusu Babeli na nchi ya Wakaldayo:
The word that YHWH has spoken concerning Babylon, concerning the land of the Chaldeans, by the hand of Jeremiah the prophet:
2 “Tangazeni na mhubiri katikati ya mataifa, twekeni bendera na mkahubiri; msiache kitu chochote, bali semeni, ‘Babeli utatekwa; Beli ataaibishwa, Merodaki atajazwa na hofu kuu. Sanamu zake zitaaibishwa na vinyago vyake vitajazwa hofu kuu.’
“Declare among nations, and sound, And lift up an ensign, sound, do not hide, Say, Babylon has been captured, Bel has been put to shame, Merodach has been broken, Her grievous things have been put to shame, Her idols have been broken.
3 Taifa kutoka kaskazini litamshambulia, na kuifanya nchi yake ukiwa. Hakuna hata mmoja atakayeishi ndani yake, watu na wanyama wataikimbia.
For a nation from the north has come up against her, It makes her land become a desolation, And there is not an inhabitant in it. From man even to beast, They have moved, they have gone.
4 “Katika siku hizo, wakati huo,” asema Bwana, “watu wa Israeli pamoja na watu wa Yuda wataenda wakilia ili kumtafuta Bwana Mungu wao.
In those days, and at that time,” A declaration of YHWH, “Sons of Israel come in, They and sons of Judah together, Going on and weeping they go, And they seek their God YHWH.
5 Wataiuliza njia iendayo Sayuni na kuelekeza nyuso zao huko. Watakuja na kuambatana na Bwana katika agano la milele ambalo halitasahaulika.
They ask the way [to] Zion, Their faces [are] toward that place: Come in, and we are joined to YHWH, A perpetual covenant—never forgotten.
6 “Watu wangu wamekuwa kondoo waliopotea; wachungaji wao wamewapotosha na kuwasababisha kuzurura juu ya milima. Walitangatanga juu ya mlima na kilima, na kusahau mahali pao wenyewe pa kupumzikia.
My people have been a perishing flock, Their shepherds have caused them to err, Causing them to go back [on] the mountains, They have gone from mountain to hill, They have forgotten their crouching-place.
7 Yeyote aliyewakuta aliwala; adui zao walisema, ‘Sisi hatuna hatia, kwa kuwa wao walitenda dhambi dhidi ya Bwana, malisho yao halisi, Bwana, aliye tumaini la baba zao.’
All finding them have devoured them, And their adversaries have said: We are not guilty, Because that they sinned against YHWH, The habitation of righteousness, And the hope of their fathers—YHWH.
8 “Kimbieni kutoka Babeli; ondokeni katika nchi ya Wakaldayo tena kuweni kama mbuzi wale waongozao kundi.
Move from the midst of Babylon, And go out from the land of the Chaldeans; And be as male goats before a flock.
9 Kwa maana nitaamsha na kuleta dhidi ya Babeli muungano wa mataifa makubwa kutoka nchi ya kaskazini. Watashika nafasi zao dhidi yake, naye kutokea kaskazini atatekwa. Mishale yao itakuwa kama mishale ya mashujaa walio hodari, ambao hawawezi kurudi mikono mitupu.
For behold, I am stirring up, And am causing to come up against Babylon, An assembly of great nations from [the] land of the north, And they have set in array against her, From there she is captured, Its arrow—as a skillful hero—does not return empty,
10 Kwa hiyo Ukaldayo utatekwa nyara; wote wamtekao nyara watapata za kutosha,” asema Bwana.
And Chaldea has been for a spoil, All her spoilers are satisfied,” A declaration of YHWH.
11 “Kwa sababu hushangilia na kufurahi, wewe utekaye urithi wangu, kwa sababu unachezacheza kama mtamba anayepura nafaka, na kulia kama farasi dume,
“Because you rejoice, because you exult, O spoilers of My inheritance, Because you increase as a heifer [at] the tender grass, And cry aloud as bulls,
12 mama yako ataaibika mno, yeye aliyekuzaa atatahayari. Atakuwa mdogo kuliko mataifa mengine yote, atakuwa nyika, nchi kame na jangwa.
Your mother has been greatly ashamed, She who bore you has been confounded, Behold, the last of nations [is] a wilderness, A dry land, and a desert.
13 Kwa sababu ya hasira ya Bwana hatakaliwa na mtu, lakini ataachwa ukiwa kabisa. Wote watakaopita Babeli watatiwa hofu na kudhihaki kwa sababu ya majeraha yake yote.
Because of the wrath of YHWH it is not inhabited, And it has been a desolation—all of it. Everyone passing by at Babylon is astonished, And hisses because of all her plagues.
14 “Shikeni nafasi zenu kuzunguka Babeli, enyi nyote mvutao upinde. Mpigeni! Msibakize mshale wowote, kwa kuwa ametenda dhambi dhidi ya Bwana.
Set yourselves in array against Babylon all around, All you treading a bow, Shoot at her, have no pity on the arrow, For she has sinned against YHWH.
15 Piga kelele dhidi yake kila upande! Anajisalimisha, minara yake inaanguka, kuta zake zimebomoka. Kwa kuwa hiki ni kisasi cha Bwana, mlipizeni kisasi; mtendeeni kama alivyowatendea wengine.
Shout against her all around, She has given forth her hand, Her foundations have fallen, Her walls have been thrown down, For it [is] the vengeance of YHWH, Be avenged of her, as she did—do to her.
16 Katilieni mbali mpanzi kutoka Babeli, pamoja na mvunaji na mundu wake akivuna. Kwa sababu ya upanga wa mdhalimu kila mmoja na arejee kwa watu wake mwenyewe, kila mmoja na akimbilie kwenye nchi yake mwenyewe.
Cut off the sower from Babylon, And him handling the sickle in the time of harvest, Because of the oppressing sword, Each to his people—they turn, And each to his land—they flee.
17 “Israeli ni kundi lililotawanyika ambalo simba wamelifukuzia mbali. Wa kwanza kumla alikuwa mfalme wa Ashuru, wa mwisho kuponda mifupa yake alikuwa Nebukadneza mfalme wa Babeli.”
Israel [is as] a scattered sheep, Lions have driven [him] away, At first, the king of Asshur devoured him, And now, at last, Nebuchadnezzar king of Babylon has broken his bone.
18 Kwa hiyo hili ndilo Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo: “Nitamwadhibu mfalme wa Babeli na nchi yake kama nilivyomwadhibu mfalme wa Ashuru.
Therefore, thus said YHWH of Hosts, God of Israel: Behold, I am seeing after the king of Babylon, And after his land, As I have seen after the king of Asshur;
19 Lakini nitamrudisha Israeli katika malisho yake mwenyewe naye atalisha huko Karmeli na Bashani; njaa yake itashibishwa juu ya vilima vya Efraimu na Gileadi.
And I have brought Israel back to his habitation, And he has fed on Carmel and on Bashan; And his soul is satisfied on Mount Ephraim and on Gilead.
20 Katika siku hizo, wakati huo,” asema Bwana, “uchunguzi utafanyika kwa ajili ya kosa la Israeli, lakini halitakuwepo, kwa ajili ya dhambi za Yuda, lakini haitapatikana hata moja, kwa kuwa nitawasamehe mabaki nitakaowaacha.
In those days, and at that time,” A declaration of YHWH, “The iniquity of Israel is sought, and it is not, And the sin of Judah, and it is not found, For I am propitious to those whom I leave!
21 “Shambulieni nchi ya Merathaimu na wale waishio huko Pekodi. Wafuatieni, waueni na kuwaangamiza kabisa,” asema Bwana. “Fanyeni kila kitu nilichowaamuru.
Against the land of Merathaim, go up against it, And to the inhabitants of Pekod, Dry up and devote their posterity,” A declaration of YHWH, “And do according to all that I have commanded you.
22 Kelele ya vita iko ndani ya nchi, kelele ya maangamizi makuu!
A noise of battle [is] in the land, And of great destruction.
23 Tazama jinsi nyundo ya dunia yote ilivyovunjika na kuharibika! Tazama jinsi Babeli ilivyokuwa ukiwa miongoni mwa mataifa!
How it has been cut and broken, The hammer of the whole earth! How Babylon has been for a desolation among nations!
24 Nimetega mtego kwa ajili yako, ee Babeli, nawe ukakamatwa kabla haujafahamu; ulipatikana na ukakamatwa kwa sababu ulimpinga Bwana.
I have laid a snare for you, And you are also captured, O Babylon, And you have known, You have been found, and are also caught, For you have stirred yourself up against YHWH.
25 Bwana amefungua ghala lake la silaha na kuzitoa silaha za ghadhabu yake, kwa kuwa Bwana Mwenyezi Mwenye Nguvu Zote anayo kazi ya kufanya katika nchi ya Wakaldayo.
YHWH has opened His treasury, And He brings out the weapons of His indignation, For a work [is] to Lord YHWH of Hosts, In the land of the Chaldeans.
26 Njooni dhidi yake kutoka mbali. Zifungueni ghala zake za nafaka; mlundikeni kama lundo la nafaka. Mwangamizeni kabisa na msimwachie mabaki yoyote.
Come in to her from the extremity, Open her storehouses, Raise her up as heaps, and devote her, Let her have no remnant.
27 Waueni mafahali wake wachanga wote; waacheni washuke machinjoni! Ole wao! Kwa kuwa siku yao imewadia, wakati wao wa kuadhibiwa.
Slay all her cows, they go down to slaughter, Woe [is] on them, for their day has come, The time of their inspection.
28 Wasikilizeni watoro na wakimbizi kutoka Babeli wakitangaza katika Sayuni jinsi Bwana, Mungu wetu alivyolipiza kisasi, kisasi kwa ajili ya Hekalu lake.
A voice of fugitives and escaped ones [Is] from the land of Babylon, To declare in Zion the vengeance of our God YHWH, The vengeance of His temple.
29 “Waiteni wapiga mishale dhidi ya Babeli, wote wale wavutao upinde. Pigeni kambi kumzunguka kabisa, asitoroke mtu yeyote. Mlipizeni kwa matendo yake; mtendeeni kama alivyotenda. Kwa kuwa alimdharau Bwana, yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli.
Summon archers to Babylon, all treading the bow, Encamp against her all around, Let [her] have no escape; Repay to her according to her work, According to all that she did—do to her, For she has been proud against YHWH, Against the Holy One of Israel.
30 Kwa hiyo, vijana wake wanaume wataanguka barabarani; askari wake wote watanyamazishwa siku ile,” asema Bwana.
Therefore her young men fall in her broad places, And all her men of war are cut off in that day,” A declaration of YHWH.
31 “Tazama, niko kinyume nawe, ewe mwenye majivuno,” asema Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote, “kwa kuwa siku yako imewadia, yaani, wakati wako wa kuadhibiwa.
“Behold, I [am] against you, O pride,” A declaration of Lord YHWH of Hosts, “For your day has come, the time of your inspection.
32 Mwenye majivuno atajikwaa na kuanguka, wala hakuna yeyote atakayemuinua; nitawasha moto katika miji yake, utakaowateketeza wote wanaomzunguka.”
And pride has stumbled, And he has fallen, and has none raising up, And I have kindled a fire in his cities, And it has devoured all around him.
33 Hili ndilo asemalo Bwana Mwenye Nguvu Zote: “Watu wa Israeli wameonewa, nao watu wa Yuda pia. Wote waliowateka wamewashikilia sana, wanakataa kuwaachia waende.
Thus said YHWH of Hosts: The sons of Israel are oppressed, And the sons of Judah together, And all their captors have kept hold on them, They have refused to send them away.
34 Lakini Mkombozi wao ana nguvu; Bwana Mwenye Nguvu Zote ndilo jina lake. Atatetea kwa nguvu shauri lao ili alete raha katika nchi yao, lakini ataleta msukosuko kwa wale waishio Babeli.
Their Redeemer [is] strong, YHWH of Hosts [is] His Name, He thoroughly pleads their cause, So as to cause the land to rest, And He has given trouble to the inhabitants of Babylon.
35 “Upanga dhidi ya Wakaldayo!” asema Bwana, “dhidi ya wale waishio Babeli na dhidi ya maafisa wake na watu wenye busara!
A sword [is] for the Chaldeans,” A declaration of YHWH, “And it [is] on the inhabitants of Babylon, And on her heads, and on her wise men;
36 Upanga dhidi ya manabii wake wa uongo! Watakuwa wapumbavu. Upanga dhidi ya mashujaa wake! Watajazwa na hofu kuu
A sword [is] on the princes, And they have become foolish; A sword [is] on her mighty ones, And they have been broken down;
37 Upanga dhidi ya farasi na magari yake ya vita pamoja na askari wake wote wa kigeni katika safu zake! Wao watakuwa kama wanawake. Upanga dhidi ya hazina zake! Hizo zitatekwa nyara.
A sword [is] on his horses and on his chariot, And on all the rabble who [are] in her midst, And they have become women; A sword [is] on her treasuries, And they have been spoiled;
38 Ukame juu ya maji yake! Nayo yatakauka. Kwa kuwa ni nchi ya sanamu, wao wanaenda wazimu kwa ajili ya sanamu.
A sword [is] on her waters, and they have been dried up, For it [is] a land of carved images, And they boast themselves in idols.
39 “Kwa hiyo, viumbe vya jangwani na fisi wataishi humo, nao bundi watakaa humo. Kamwe haitakaliwa tena wala watu hawataishi humo kutoka kizazi hadi kizazi.
Therefore desert-dwellers dwell with howlers, Indeed, daughters of the ostrich have dwelt in her, And it is not inhabited anymore forever, Nor dwelt in from generation to generation.
40 Kama vile Mungu alivyoangamiza Sodoma na Gomora pamoja na miji iliyokuwa jirani nayo,” asema Bwana, “vivyo hivyo hakuna mtu yeyote atakayeishi humo. Naam, hakuna mtu yeyote atakayekaa humo.
As the overthrow by God of Sodom, And of Gomorrah, and of its neighbors,” A declaration of YHWH, “None dwell there, Nor does a son of man sojourn in her.
41 “Tazama! Jeshi linakuja kutoka kaskazini; taifa kubwa na wafalme wengi wanaamshwa kutoka miisho ya dunia.
Behold, a people has come from the north, Even a great nation, And many kings are stirred up from the sides of the earth.
42 Wamejifunga pinde na mikuki; ni wakatili na wasio na huruma. Wanatoa sauti kama bahari inayonguruma wanapoendesha farasi zao; wanakuja kama watu waliojipanga tayari kwa vita ili kukushambulia, ee Binti Babeli.
They seize bow and javelin, They [are] cruel, and they have no mercy, Their voice sounds as a sea, and they ride on horses, Set in array as a man for battle, Against you, O daughter of Babylon.
43 Mfalme wa Babeli amesikia habari kuwahusu, nayo mikono yake imelegea. Uchungu umemshika, maumivu kama ya mwanamke katika utungu wa kuzaa.
The king of Babylon has heard their report, And his hands have been feeble, Distress has seized him; pain as a travailing woman.
44 Kama simba anayepanda kutoka vichaka vya Yordani kuja kwenye nchi ya malisho mengi, ndivyo nitamfukuza Babeli kutoka nchi yake ghafula. Ni nani aliye mteule, nitakayemweka kwa ajili ya jambo hili? Ni nani aliye kama mimi, na ni nani awezaye kunipinga? Tena ni mchungaji yupi awezaye kusimama kinyume nami?”
Behold, he comes up as a lion, Because of the rising of the Jordan, To the enduring habitation, But I cause to rest, I cause them to run from off her. And who is chosen? I lay a charge on her, For who [is] like Me? And who convenes Me? And who [is] this shepherd who stands before Me?
45 Kwa hiyo, sikia kile Bwana alichokipanga dhidi ya Babeli, kile alichokusudia dhidi ya nchi ya Wakaldayo: Aliye mchanga katika kundi ataburutwa mbali. Yeye ataharibu kabisa malisho yao kwa sababu yao.
Therefore, hear the counsel of YHWH, That He counseled concerning Babylon, And His plans that He has devised Concerning the land of the Chaldeans; Do little ones of the flock not drag them out, Does He not make the habitation desolate over them?
46 Kwa sauti ya kutekwa kwa Babeli, dunia itatetemeka; kilio chake kitasikika pote miongoni mwa mataifa.
From the sound of Babylon having been captured, The earth has been shaken, And a cry has been heard among nations!”

< Yeremia 50 >