< Yeremia 48 >

1 Kuhusu Moabu: Hili ndilo Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo: “Ole wake Nebo, kwa maana utaharibiwa. Kiriathaimu utaaibishwa na kutekwa; Misgabu itaaibishwa na kuvunjavunjwa.
לְמוֹאָב כֹּה־אָמַר יְהֹוָה צְבָאוֹת אֱלֹהֵי יִשְׂרָאֵל הוֹי אֶל־נְבוֹ כִּי שֻׁדָּדָה הֹבִישָׁה נִלְכְּדָה קִרְיָתָיִם הֹבִישָׁה הַמִּשְׂגָּב וָחָֽתָּה׃
2 Moabu haitasifiwa tena; huko Heshboni watu watafanya shauri baya la anguko lake: ‘Njooni na tuangamize taifa lile.’ Wewe nawe, ee Madmena, utanyamazishwa; upanga utakufuatia.
אֵין עוֹד תְּהִלַּת מוֹאָב בְּחֶשְׁבּוֹן חָשְׁבוּ עָלֶיהָ רָעָה לְכוּ וְנַכְרִיתֶנָּה מִגּוֹי גַּם־מַדְמֵן תִּדֹּמִּי אַחֲרַיִךְ תֵּלֶךְ חָֽרֶב׃
3 Sikiliza kilio kutoka Horonaimu, kilio cha maangamizi makuu na uharibifu.
קוֹל צְעָקָה מֵחֹרוֹנָיִם שֹׁד וָשֶׁבֶר גָּדֽוֹל׃
4 Moabu utavunjwa, wadogo wake watapiga kelele.
נִשְׁבְּרָה מוֹאָב הִשְׁמִיעוּ זְּעָקָה (צעוריה) [צְעִירֶֽיהָ]׃
5 Wanapanda kwenda njia ya kuelekea Luhithi, wakilia kwa uchungu wanapotembea, kwenye njia inayoshuka kwenda Horonaimu, kilio cha uchungu kwa ajili ya uharibifu kinasikika.
כִּי מַעֲלֵה (הלחות) [הַלֻּחִית] בִּבְכִי יַעֲלֶה־בֶּכִי כִּי בְּמוֹרַד חוֹרֹנַיִם צָרֵי צַעֲקַת־שֶׁבֶר שָׁמֵֽעוּ׃
6 Kimbieni! Okoeni maisha yenu, kuweni kama kichaka jangwani.
נֻסוּ מַלְּטוּ נַפְשְׁכֶם וְתִֽהְיֶינָה כַּעֲרוֹעֵר בַּמִּדְבָּֽר׃
7 Kwa kuwa mmetumainia matendo yenu na mali zenu, ninyi pia mtachukuliwa mateka, naye Kemoshi atakwenda uhamishoni, pamoja na makuhani wake na maafisa wake.
כִּי יַעַן בִּטְחֵךְ בְּמַעֲשַׂיִךְ וּבְאוֹצְרוֹתַיִךְ גַּם־אַתְּ תִּלָּכֵדִי וְיָצָא (כמיש) [כְמוֹשׁ] בַּגּוֹלָה כֹּהֲנָיו וְשָׂרָיו (יחד) [יַחְדָּֽיו]׃
8 Mharabu atakuja dhidi ya kila mji, wala hakuna mji utakaookoka. Bonde litaangamizwa na uwanda utaharibiwa, kwa sababu Bwana amesema.
וְיָבֹא שֹׁדֵד אֶל־כׇּל־עִיר וְעִיר לֹא תִמָּלֵט וְאָבַד הָעֵמֶק וְנִשְׁמַד הַמִּישֹׁר אֲשֶׁר אָמַר יְהֹוָֽה׃
9 Wekeni chumvi kwa ajili ya Moabu, kwa kuwa ataangamizwa; miji yake itakuwa ukiwa, pasipo kuwa na mtu atakayeishi ndani yake.
תְּנוּ־צִיץ לְמוֹאָב כִּי נָצֹא תֵּצֵא וְעָרֶיהָ לְשַׁמָּה תִֽהְיֶינָה מֵאֵין יוֹשֵׁב בָּהֵֽן׃
10 “Alaaniwe yeye afanyaye kazi ya Bwana kwa hila! Alaaniwe yeye auzuiaye upanga wake usimwage damu!
אָרוּר עֹשֶׂה מְלֶאכֶת יְהֹוָה רְמִיָּה וְאָרוּר מֹנֵעַ חַרְבּוֹ מִדָּֽם׃
11 “Moabu amestarehe tangu ujana wake, kama divai iliyoachwa kwenye machujo yake, haikumiminwa kutoka chombo kimoja hadi kingine, hajaenda uhamishoni. Kwa hiyo ana ladha ile ile kama aliyokuwa nayo, nayo harufu yake haijabadilika.
שַׁאֲנַן מוֹאָב מִנְּעוּרָיו וְשֹׁקֵט הוּא אֶל־שְׁמָרָיו וְלֹֽא־הוּרַק מִכְּלִי אֶל־כֶּלִי וּבַגּוֹלָה לֹא הָלָךְ עַל־כֵּן עָמַד טַעְמוֹ בּוֹ וְרֵיחוֹ לֹא נָמָֽר׃
12 Lakini siku zinakuja,” asema Bwana, “nitakapotuma watu wamiminao kutoka kwenye magudulia, nao watamimina; wataacha magudulia yake yakiwa matupu na kuvunja mitungi yake.
לָכֵן הִנֵּֽה־יָמִים בָּאִים נְאֻם־יְהֹוָה וְשִׁלַּחְתִּי־לוֹ צֹעִים וְצֵעֻהוּ וְכֵלָיו יָרִיקוּ וְנִבְלֵיהֶם יְנַפֵּֽצוּ׃
13 Kisha Moabu atamwonea aibu mungu wao Kemoshi, kama vile nyumba ya Israeli walivyoona aibu walipotegemea mungu wa Betheli.
וּבֹשׁ מוֹאָב מִכְּמוֹשׁ כַּֽאֲשֶׁר־בֹּשׁוּ בֵּית יִשְׂרָאֵל מִבֵּית אֵל מִבְטֶחָֽם׃
14 “Mwawezaje kusema, ‘Sisi ni mashujaa, watu jasiri katika vita’?
אֵיךְ תֹּֽאמְרוּ גִּבּוֹרִים אֲנָחְנוּ וְאַנְשֵׁי־חַיִל לַמִּלְחָמָֽה׃
15 Moabu ataangamizwa na miji yake itavamiwa, vijana wake waume walio bora sana watachinjwa,” asema Mfalme, ambaye jina lake ni Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote.
שֻׁדַּד מוֹאָב וְעָרֶיהָ עָלָה וּמִבְחַר בַּחוּרָיו יָרְדוּ לַטָּבַח נְאֻם־הַמֶּלֶךְ יְהֹוָה צְבָאוֹת שְׁמֽוֹ׃
16 “Kuanguka kwa Moabu kumekaribia, janga kubwa litamjia kwa haraka.
קָרוֹב אֵיד־מוֹאָב לָבוֹא וְרָעָתוֹ מִהֲרָה מְאֹֽד׃
17 Ombolezeni kwa ajili yake, ninyi nyote mnaomzunguka, ninyi nyote mnaojua sifa zake, semeni, ‘Tazama jinsi ilivyovunjika fimbo ya kifalme yenye nguvu, tazama jinsi ilivyovunjika fimbo iliyotukuka!’
נֻדוּ לוֹ כׇּל־סְבִיבָיו וְכֹל יֹדְעֵי שְׁמוֹ אִמְרוּ אֵיכָה נִשְׁבַּר מַטֵּה־עֹז מַקֵּל תִּפְאָרָֽה׃
18 “Shuka kutoka fahari yako na uketi katika ardhi iliyokauka, enyi wenyeji wa Binti wa Diboni, kwa maana yeye aangamizaye Moabu atakuja dhidi yako, na kuangamiza miji yako iliyozungushiwa maboma.
רְדִי מִכָּבוֹד (ישבי) [וּשְׁבִי] בַצָּמָא יֹשֶׁבֶת בַּת־דִּיבוֹן כִּֽי־שֹׁדֵד מוֹאָב עָלָה בָךְ שִׁחֵת מִבְצָרָֽיִךְ׃
19 Simama kando ya barabara na utazame, wewe unayeishi Aroeri. Muulize mwanaume anayekimbia na mwanamke anayetoroka, waulize, ‘Kumetokea nini?’
אֶל־דֶּרֶךְ עִמְדִי וְצַפִּי יוֹשֶׁבֶת עֲרוֹעֵר שַׁאֲלִי־נָס וְנִמְלָטָה אִמְרִי מַה־נִּֽהְיָֽתָה׃
20 Moabu amefedheheshwa, kwa kuwa amevunjavunjwa. Lieni kwa huzuni na kupiga kelele! Tangazeni kando ya Arnoni kwamba Moabu ameangamizwa.
הֹבִישׁ מוֹאָב כִּי־חַתָּה (הילילי וזעקי) [הֵילִילוּ ׀ וּֽזְעָקוּ] הַגִּידוּ בְאַרְנוֹן כִּי שֻׁדַּד מוֹאָֽב׃
21 Hukumu imefika kwenye uwanda wa juu: katika Holoni, Yahasa na Mefaathi,
וּמִשְׁפָּט בָּא אֶל־אֶרֶץ הַמִּישֹׁר אֶל־חֹלוֹן וְאֶל־יַהְצָה וְעַל־(מופעת) [מֵיפָֽעַת]׃
22 katika Diboni, Nebo na Beth-Diblathaimu,
וְעַל־דִּיבוֹן וְעַל־נְבוֹ וְעַל־בֵּית דִּבְלָתָֽיִם׃
23 katika Kiriathaimu, Beth-Gamuli na Beth-Meoni,
וְעַל קִרְיָתַיִם וְעַל־בֵּית גָּמוּל וְעַל־בֵּית מְעֽוֹן׃
24 katika Keriothi na Bosra; kwa miji yote ya Moabu, iliyoko mbali na karibu.
וְעַל־קְרִיּוֹת וְעַל־בׇּצְרָה וְעַל כׇּל־עָרֵי אֶרֶץ מוֹאָב הָרְחֹקוֹת וְהַקְּרֹבֽוֹת׃
25 Pembe ya Moabu imekatwa, mkono wake umevunjwa,” asema Bwana.
נִגְדְּעָה קֶרֶן מוֹאָב וּזְרֹעוֹ נִשְׁבָּרָה נְאֻם יְהֹוָֽה׃
26 “Mlevye, kwa kuwa amemdharau Bwana. Moabu na agaegae katika matapishi yake, yeye na awe kitu cha dhihaka.
הַשְׁכִּירֻהוּ כִּי עַל־יְהֹוָה הִגְדִּיל וְסָפַק מוֹאָב בְּקִיאוֹ וְהָיָה לִשְׂחֹק גַּם־הֽוּא׃
27 Je, Israeli hakuwa kitu chako cha kudhihakiwa? Je, alikamatwa miongoni mwa wezi, kiasi cha kutikisa kichwa chako kwa dharau kila mara unapozungumza juu yake?
וְאִם ׀ לוֹא הַשְּׂחֹק הָיָה לְךָ יִשְׂרָאֵל אִם־בְּגַנָּבִים (נמצאה) [נִמְצָא] כִּֽי־מִדֵּי דְבָרֶיךָ בּוֹ תִּתְנוֹדָֽד׃
28 Ondokeni kwenye miji yenu, mkaishi katikati ya miamba, enyi mnaoishi Moabu. Kuweni kama huwa ambaye hutengeneza kiota chake kwenye mdomo wa pango.
עִזְבוּ עָרִים וְשִׁכְנוּ בַסֶּלַע יֹשְׁבֵי מוֹאָב וִֽהְיוּ כְיוֹנָה תְּקַנֵּן בְּעֶבְרֵי פִי־פָֽחַת׃
29 “Tumesikia juu ya kiburi cha Moabu: kutakabari kwake kwa kiburi na majivuno, kiburi chake na ufidhuli wake, na kujivuna kwa moyo wake.
שָׁמַעְנוּ גְאוֹן־מוֹאָב גֵּאֶה מְאֹד גׇּבְהוֹ וּגְאוֹנוֹ וְגַאֲוָתוֹ וְרֻם לִבּֽוֹ׃
30 Ninaujua ujeuri wake, lakini ni bure,” asema Bwana, “nako kujisifu kwake hakumsaidii chochote.
אֲנִי יָדַעְתִּי נְאֻם־יְהֹוָה עֶבְרָתוֹ וְלֹא־כֵן בַּדָּיו לֹא־כֵן עָשֽׂוּ׃
31 Kwa hiyo namlilia Moabu, kwa ajili ya Moabu yote ninalia, ninaomboleza kwa ajili ya watu wa Kir-Haresethi.
עַל־כֵּן עַל־מוֹאָב אֲיֵלִיל וּלְמוֹאָב כֻּלֹּה אֶזְעָק אֶל־אַנְשֵׁי קִֽיר־חֶרֶשׂ יֶהְגֶּֽה׃
32 Ninalia machozi kwa ajili yenu, kama Yazeri aliavyo, enyi mizabibu ya Sibma. Matawi yako yameenea hadi baharini; yamefika hadi bahari ya Yazeri. Mharabu ameyaangukia matunda yako yaliyoiva na mizabibu yako iliyoiva.
מִבְּכִי יַעְזֵר אֶבְכֶּה־לָּךְ הַגֶּפֶן שִׂבְמָה נְטִישֹׁתַיִךְ עָבְרוּ יָם עַד יָם יַעְזֵר נָגָעוּ עַל־קֵיצֵךְ וְעַל־בְּצִירֵךְ שֹׁדֵד נָפָֽל׃
33 Shangwe na furaha vimetoweka kutoka bustani na mashamba ya Moabu. Nimekomesha kutiririka kwa divai kutoka mashinikizo; hakuna hata mmoja ayakanyagaye kwa kelele za shangwe. Ingawa kuna kelele, sio kelele za shangwe.
וְנֶאֶסְפָה שִׂמְחָה וָגִיל מִכַּרְמֶל וּמֵאֶרֶץ מוֹאָב וְיַיִן מִיקָבִים הִשְׁבַּתִּי לֹא־יִדְרֹךְ הֵידָד הֵידָד לֹא הֵידָֽד׃
34 “Sauti ya kilio chao inapanda kutoka Heshboni hadi Eleale na Yahazi, kutoka Soari hadi Horonaimu na Eglath-Shelishiya, kwa kuwa hata maji ya Nimrimu yamekauka.
מִזַּעֲקַת חֶשְׁבּוֹן עַד־אֶלְעָלֵה עַד־יַהַץ נָתְנוּ קוֹלָם מִצֹּעַר עַד־חֹרֹנַיִם עֶגְלַת שְׁלִֽשִׁיָּה כִּי גַּם־מֵי נִמְרִים לִמְשַׁמּוֹת יִהְיֽוּ׃
35 Nitakomesha wale wote katika Moabu watoao sadaka mahali pa juu, na kufukiza uvumba kwa miungu yao,” asema Bwana.
וְהִשְׁבַּתִּי לְמוֹאָב נְאֻם־יְהֹוָה מַעֲלֶה בָמָה וּמַקְטִיר לֵאלֹהָֽיו׃
36 “Kwa hiyo moyo wangu unaomboleza kwa ajili ya Moabu kama filimbi; unaomboleza kama filimbi kwa ajili ya watu wa Kir-Haresethi. Utajiri waliojipatia umetoweka.
עַל־כֵּן לִבִּי לְמוֹאָב כַּחֲלִלִים יֶהֱמֶה וְלִבִּי אֶל־אַנְשֵׁי קִֽיר־חֶרֶשׂ כַּחֲלִילִים יֶהֱמֶה עַל־כֵּן יִתְרַת עָשָׂה אָבָֽדוּ׃
37 Kila kichwa kimenyolewa na kila mwenye ndevu zimekatwa; kila mkono umekatwa na kila kiuno kimefunikwa kwa nguo ya gunia.
כִּי כׇל־רֹאשׁ קׇרְחָה וְכׇל־זָקָן גְּרֻעָה עַל כׇּל־יָדַיִם גְּדֻדֹת וְעַל־מׇתְנַיִם שָֽׂק׃
38 Juu ya mapaa yote katika Moabu na katika viwanja hakuna kitu chochote isipokuwa maombolezo, kwa kuwa nimemvunja Moabu kama gudulia ambalo hakuna mtu yeyote anayelitaka,” asema Bwana.
עַל כׇּל־גַּגּוֹת מוֹאָב וּבִרְחֹבֹתֶיהָ כֻּלֹּה מִסְפֵּד כִּי־שָׁבַרְתִּי אֶת־מוֹאָב כִּכְלִי אֵֽין־חֵפֶץ בּוֹ נְאֻם־יְהֹוָֽה׃
39 “Tazama jinsi alivyovunjikavunjika! Jinsi wanavyolia kwa huzuni! Tazama jinsi Moabu anavyogeuka kwa aibu! Moabu amekuwa kitu cha kudhihakiwa, kitu cha kutisha kwa wale wote wanaomzunguka.”
אֵיךְ חַתָּה הֵילִילוּ אֵיךְ הִפְנָה־עֹרֶף מוֹאָב בּוֹשׁ וְהָיָה מוֹאָב לִשְׂחֹק וְלִמְחִתָּה לְכׇל־סְבִיבָֽיו׃
40 Hili ndilo asemalo Bwana: “Tazama! Tai anashuka chini, akitanda mabawa yake juu ya Moabu.
כִּי־כֹה אָמַר יְהֹוָה הִנֵּה כַנֶּשֶׁר יִדְאֶה וּפָרַשׂ כְּנָפָיו אֶל־מוֹאָֽב׃
41 Miji itatekwa na ngome zake zitatwaliwa. Katika siku hiyo, mioyo ya mashujaa wa Moabu itakuwa kama moyo wa mwanamke katika utungu wa kuzaa.
נִלְכְּדָה הַקְּרִיּוֹת וְהַמְּצָדוֹת נִתְפָּשָׂה וְֽהָיָה לֵב גִּבּוֹרֵי מוֹאָב בַּיּוֹם הַהוּא כְּלֵב אִשָּׁה מְצֵרָֽה׃
42 Moabu ataangamizwa kama taifa kwa sababu amemdharau Bwana.
וְנִשְׁמַד מוֹאָב מֵעָם כִּי עַל־יְהֹוָה הִגְדִּֽיל׃
43 Hofu kuu, shimo na mtego vinawangojea, enyi watu wa Moabu,” asema Bwana.
פַּחַד וָפַחַת וָפָח עָלֶיךָ יוֹשֵׁב מוֹאָב נְאֻם־יְהֹוָֽה׃
44 “Yeyote atakayeikimbia hiyo hofu kuu ataanguka ndani ya shimo, yeyote atakayepanda kutoka shimoni, atanaswa katika mtego, kwa sababu nitaletea Moabu mwaka wa adhabu yake,” asema Bwana.
(הניס) [הַנָּס] מִפְּנֵי הַפַּחַד יִפֹּל אֶל־הַפַּחַת וְהָֽעֹלֶה מִן־הַפַּחַת יִלָּכֵד בַּפָּח כִּֽי־אָבִיא אֵלֶיהָ אֶל־מוֹאָב שְׁנַת פְּקֻדָּתָם נְאֻם־יְהֹוָֽה׃
45 “Katika kivuli cha Heshboni, wakimbizi wamesimama pasipo msaada, kwa kuwa moto umezimika huko Heshboni, mwali wa moto kutoka katikati ya Sihoni; unaunguza vipaji vya nyuso za Moabu, mafuvu yao wenye kujivuna kwa kelele.
בְּצֵל חֶשְׁבּוֹן עָמְדוּ מִכֹּחַ נָסִים כִּי־אֵשׁ יָצָא מֵחֶשְׁבּוֹן וְלֶהָבָה מִבֵּין סִיחוֹן וַתֹּאכַל פְּאַת מוֹאָב וְקׇדְקֹד בְּנֵי שָׁאֽוֹן׃
46 Ole wako, ee Moabu! Watu wa Kemoshi wameangamizwa; wana wako wamepelekwa uhamishoni na binti zako wamechukuliwa mateka.
אוֹי־לְךָ מוֹאָב אָבַד עַם־כְּמוֹשׁ כִּֽי־לֻקְּחוּ בָנֶיךָ בַּשֶּׁבִי וּבְנֹתֶיךָ בַּשִּׁבְיָֽה׃
47 “Lakini nitarudisha mateka wa Moabu, katika siku zijazo,” asema Bwana. Huu ndio mwisho wa hukumu juu ya Moabu.
וְשַׁבְתִּי שְׁבוּת־מוֹאָב בְּאַחֲרִית הַיָּמִים נְאֻם־יְהֹוָה עַד־הֵנָּה מִשְׁפַּט מוֹאָֽב׃

< Yeremia 48 >