< Yeremia 44 >

1 Neno hili lilimjia Yeremia kuhusu Wayahudi wote waishio Misri, huko Migdoli, Tahpanhesi na Memfisi, katika nchi ya Pathrosi kusema:
Hili lilikuwa neno ambalo lilikuja kwa Yeremia kuhusu Wayahudi wote walioishi katika nchi ya Misri, wale wanaoishi Migdoli, Tahpanhesi, Memphis, na katika nchi ya Patrosi.
2 “Hili ndilo asemalo Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli: Mliona maangamizi makubwa niliyoyaleta juu ya Yerusalemu na juu ya miji yote ya Yuda. Leo imeachwa ukiwa na magofu
“Yahwe wa majeshi, Mungu wa Israel, asema hivi: Wewe mwenyewe umeyaona maafa yote niliyoleta juu ya Yerusalemu na miji yote ya Yuda. Ona, ni ukiwa leo. Hakuna yeyote anaishi mwao.
3 kwa sababu ya uovu waliokuwa wameufanya. Walinikasirisha kwa kufukiza uvumba na kwa kuabudu miungu mingine ambayo kamwe wao, wala ninyi, wala baba zenu hawakuifahamu.
Hii ni kwa sababu ya mambo maovu waliyofanya kunikosea mimi kwa kwenda kuchoma ubani na kuabudu miungu mengine. Hawa walikuwa miungu ambao wala wao wenyewe, wala ninyi, wala mababu zenu walijua.
4 Tena na tena, niliwatuma watumishi wangu manabii ambao walisema, ‘Msifanye jambo hili la kuchukiza ambalo nalichukia!’
Basi nirudie kuwatuma watumwa wangu wote manabii kwao. Niliwatuma wao kusema, 'Acha kufanya vitu hivi machukizo ambayo nachukia.
5 Lakini hawakusikiliza wala hawakujali, hawakugeuka ili kuuacha uovu wao, wala hawakuacha kufukiza uvumba kwa miungu mingine.
Lakini hawakunisikiliza. Walikataa kuwa makini au kuyaacha maovu kwa kuchoma ubani kwa miungu mingine.
6 Kwa hiyo hasira yangu kali ilimwagika, ikawaka dhidi ya miji ya Yuda na barabara za Yerusalemu, na kuifanya ukiwa na magofu kama ilivyo leo.
Basi hasira yangu na gadhabu yangu zilimwanga na kuwasha moto kwenye miji ya Yuda na mitaa ya Yerusalemu. Basi waliharibiwa na kuteketezwa, kama katika siku ya leo.”
7 “Basi hili ndilo Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo: Kwa nini kujiletea maafa makubwa kama haya juu yenu kwa kujikatilia mbali kutoka Yuda wanaume na wanawake, watoto na wanyonyao, hata kujiacha bila mabaki?
Basi sasa Yahwe, Mungu wa majeshi na Mungu wa Israel, asema hivi, “Kwanini unafanya maovu makubwa dhidi yenu? Kwanini mnasababisha ninyi wenyewe kujitenga kutoka miongoni mwa Yuda - wanaume na wanawake, watoto na wanyonyao? Hakuna mabaki yenu yatabaki.
8 Kwa nini kuichochea hasira yangu kwa kile ambacho mikono yenu imekitengeneza, mkaifukizia uvumba miungu mingine huko Misri, mahali mlipokuja kuishi? Mtajiangamiza wenyewe na kujifanya kitu cha kulaania na shutumu miongoni mwa mataifa yote duniani.
Kwa maovu yenu mmenikosea pamoja na matendo ya mikono yenu, kwa kuchoma ubani kwa miungu mingine kwenye nchi ya Misri, ambapo mmekwenda kuishi. Mmeenda huko ili kwamba mtaangamizwa, ili kwamba mtalaaniwa na mashutumu miongoni mwa mataifa yote ya duniani.
9 Je, mmesahau uovu uliotendwa na baba zenu, na wafalme na malkia wa Yuda, na uovu uliofanywa na ninyi na wake zenu katika nchi ya Yuda na barabara za Yerusalemu?
Mmesahau maovu yaliyofanywa na mababu zenu na maouvu yaliyofanywa na wafalme wa Yuda na wake zao? Mmesahau uovu uliofanywa na ninyi na wake zenu katika nchi ya Yuda na mitaa ya Yerusalemu?
10 Mpaka leo hawajajinyenyekeza au kuonyesha heshima, wala hawajafuata sheria yangu na amri nilizoweka mbele yenu na baba zenu.
Kwa siku hii, hawajanyenyekea bado. Hawashimu sheria yangu au maagizo niliyoweka mbele yao na mababu zao, wala hawatembei nazo.”
11 “Kwa hiyo, hili ndilo Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo: Mimi nimekusudia kuleta maafa juu yenu, na kuiangamiza Yuda yote.
Kwa hiyo sasa Yahwe wa majeshi, Mungu wa Israel, asema hivi, “Ona, Nimekaribia kuweka uso wangu dhidi yenu kuleta maafa kwenu na kuiharibu Yuda yote.
12 Nitawaondoa mabaki ya Yuda waliokusudia kwenda Misri kukaa humo. Wote wataangamia huko Misri, wataanguka kwa upanga au kufa kwa njaa. Kuanzia aliye mdogo kabisa hadi aliye mkuu sana, watakufa kwa upanga au njaa. Watakuwa kitu cha kulaania na cha kutisha, cha laumu na shutumu.
Kwa kuwa nitachukua mabaki wa Yuda ambaye ameanza safari kwenda nchi ya Misri kuishi huko. Nitafanya hivi ili kwamba wataangamia wote katika nchi ya Misri. Wataanguka kwa upanga na njaa. Kutoka wadogo kwa wakubwa wataangamia kwa upanga na njaa. Watakufa na watakuwa sababu ya kuaapa, kulaani, mashutumu, na kitu kibaya.
13 Nitawaadhibu wale waishio Misri kwa upanga, njaa na tauni kama nilivyoiadhibu Yerusalemu.
Kwa kuwa nitawaadhibu watu wakazi wa nchi ya Misri kama nilivyoadhibu Yerusalem kwa upanga, njaa, na pigo.
14 Hakuna hata mmoja wa mabaki ya Yuda ambaye amekwenda kuishi Misri atakayeepuka au kunusurika ili kurudi katika nchi ya Yuda, ambayo wanaitamani sana kurudi na kuishi ndani yake, hakuna hata mmoja atakayerudi isipokuwa wakimbizi wachache.”
Hakuna mkimbizi au mwathirika wa mabaki ya Yuda ambaye wataenda kuishi huko kwenye nchi ya Misri watarudi kwenye nchi ya Yuda, hata kama wanataka kurudi na kuishi huko. Hakuna kati yao atarudi, ijapokuwa wachache ambayo watatoroka kutoka huko.”
15 Kisha wanaume wote ambao walijua kwamba wake zao walikuwa wakifukiza uvumba kwa miungu mingine, pamoja na wanawake wote waliokuwako, yaani, kusanyiko kubwa na watu wote walioishi nchi ya Misri na Pathrosi, wakamwambia Yeremia,
Kisha watu wote ambao walijua kwamba wake zao walikuwa wakichoma ubani kwa miungu mingine, na wanawake wote waliokuwa katika kusanyiko kuu, na watu wote ambao walikuwa wakiishi kwenye nchi ya Misri katika Pathrosi walimjibu Yeremia.
16 “Hatutausikiliza ujumbe uliotuambia katika jina la Bwana!
Walisema, “Kuhusu neno ambalo mmetuambia sisi kwa jina la Yahwe: Hatutakusikiliza.
17 Hakika tutafanya kila kitu tulichosema tutakifanya: Tutafukiza uvumba kwa Malkia wa Mbinguni na tutammiminia sadaka zetu za kinywaji kama vile sisi na baba zetu, wafalme wetu na maafisa wetu tulivyofanya katika miji ya Yuda na katika barabara za Yerusalemu. Wakati ule tulikuwa na chakula tele, tulikuwa matajiri wala hatukupata dhara lolote.
Kwa hakika tutafanya mambo yote ambayo tulisema tungefanya: kuchoma ubani kwa malkia wa Mbingu na kumwaga kinywaji cha sadaka kwake kama sisi, mababu zetu, wafalme wetu, na viongozi wetu walivyofanya kwenye miji ya Yuda na mitaa ya Yerusalemu. Kisha tutajazwa pamoja na chakula na tutafanikiwa, pasipo kupata maafa yoyote.
18 Lakini tangu tulipoacha kumfukizia uvumba Malkia wa Mbinguni na kummiminia sadaka za kinywaji, hatupati chochote, na tumekuwa tukiangamizwa kwa upanga na njaa.”
Wakati tunajiepusha kutofanya mambo haya, si kutoa sadaka ya ubani kwa Malkia wa Mbinguni na si kumwanga kinywaji cha sadaka kwake, tulikuwa wote tunaumwa umaskini na tulikuwa tunakufa kwa upanga na njaa.”
19 Wanawake wakaongeza kusema, “Wakati tulipomfukizia uvumba Malkia wa Mbinguni na kummiminia sadaka zetu za kinywaji, je, waume zetu hawakujua kwamba tulikuwa tukitengeneza maandazi kwa mfano wake, na kummiminia yeye sadaka za kinywaji?”
Wanawake walisema, “Wakati tulipokuwa tunatengeneza ubani wa sadaka mbele ya Malkia wa Mbinguni na kumwaga kinywaji cha sadaka kwake, tulifanya hivi vitu pasipo waume wetu kujua.”
20 Ndipo Yeremia akawaambia watu wote, wanaume na wanawake waliokuwa wakimjibu,
Kisha Yeremia alisema kwa watu wote - kwa wanaume na wanawake, na watu wote waliomjibu yeye - alihubiri na kusema,
21 “Je, Bwana hakukumbuka na kufikiri juu ya uvumba uliofukizwa katika miji ya Yuda na barabara za Yerusalemu na ninyi pamoja na baba zenu, wafalme wenu, maafisa wenu na watu wa nchi?
“Je Yahwe hakukumbuka ubani ambao mliuchoma kwenye miji ya Yuda na mitaa ya Yerusalem - wewe na mababu zenu, wafalme wenu na viongozi, na watu wa nchi? Kwa kuwa Yahwe anakumbuka hili kwenye akili; inakuja kwenye mawazo yake.
22 Bwana alipokuwa hawezi kuendelea kuvumilia matendo yenu maovu na mambo ya machukizo mliyoyafanya, nchi yenu ilikuwa kitu cha kulaania na kuachwa ukiwa pasipo wakazi, kama ilivyo leo.
Basi hawakuweza tena kuvumilia kwa sababu ya matendo yenu maovu, kwa sababu machukizo ambayo mlifanya. Basi nchi yenu imekuwa ukiwa, kutisha, na laana basi hapakuwa na mkazi tena kwa siku hii.
23 Kwa sababu mmefukiza uvumba na kufanya dhambi dhidi ya Bwana, nanyi hamkumtii wala kufuata sheria yake au amri zake au maagizo yake, maafa haya yamekuja juu yenu, kama mnavyoona sasa.”
Kwa sababu mlichoma ubani na kufanya dhambi dhidi ya Yahwe, na kwa sababu msingesikiliza sauti yake, sheria yake, amri zake, au maagizo ya agano lake, maafa haya dhidi yenu yemetokea kama kwa siku hii. “
24 Kisha Yeremia akawaambia watu wote, pamoja na wanawake, “Sikieni neno la Bwana, enyi watu wote wa Yuda mlioko Misri.
Kisha Yeremia alisema kwa watu wote na wanawake wote, “Sikia neno la Yahwe, Yuda yote ambao wamo katika nchi ya Misri.
25 Hili ndilo asemalo Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli: Ninyi na wake zenu mmeonyesha kwa matendo yenu kile mlichoahidi mliposema, ‘Hakika tutatimiza nadhiri tulizoziweka za kumfukizia uvumba na kummiminia sadaka za kinywaji Malkia wa Mbinguni.’ “Endeleeni basi, fanyeni yale mliyoahidi! Timizeni nadhiri zenu!
Yahwe wa majeshi, Mungu wa Israel, asema hivi, Wewe na wake zako wote mmesema kwa vinywa vyenu na kubeba kwa mikono yenu kile mlichosema, “Hakika tutabeba viapo ambavyo tulifanya kumwabudu Malkia wa Mbinguni, kwanga kinywaji cha sadaka kwake.” Sasa timiza viapo vyenu, vibebe.”
26 Lakini sikieni neno la Bwana, enyi Wayahudi wote mnaoishi Misri: ‘Ninaapa kwa Jina langu lililo kuu,’ asema Bwana, ‘kwamba hakuna hata mmoja atokaye Yuda anayeishi popote Misri ambaye kamwe ataomba tena kwa Jina langu au kuapa, akisema, “Hakika kama Bwana Mwenyezi aishivyo.”
Basi, sikiliza neno la Yahwe, Yuda yote ambao mnaishi katika nchi ya Misri, 'Ona, Nimeapa kwa jina langu kuu-asema Yahwe. Jina langu halitaitwa kwa vinywa vya wanaume wowote wa Yuda kwenye nchi ya Misri, wewe ambaye sasa unasema, “Kama Bwana Yahwe aishivyo.”
27 Kwa maana ninawaangalia kwa ajili ya madhara, wala sio kwa mema. Wayahudi walioko Misri wataangamia kwa upanga na njaa, hadi wote watakapoangamizwa.
Ona, Ninakutazama juu yako kwa ajili ya maafa na si kwa uzuri. Kila mtu wa Yuda katika nchi ya Misri ataangamia kwa upanga na njaa mpaka wote wameishia.
28 Wale watakaonusurika upanga na kurudi katika nchi ya Yuda kutoka Misri watakuwa wachache sana. Ndipo mabaki wote wa Yuda waliokuja kuishi Misri watakapojua ni neno la nani litakalosimama, kwamba ni langu au lao.
Kisha waathirika wa upanga watarudi kutoka nchi ya Misri kwa nchi ya Yuda, peke idadi ndogo yao. Basi mabaki yote ya Yuda walioenda kwenye nchi ya Misri kuishi huko watajua ambao neno litakuwa kweli: yangu au yao.
29 “‘Hii itakuwa ndiyo ishara kwenu kwamba nitawaadhibu mahali hapa, asema Bwana, ili mpate kujua kuwa onyo langu la madhara dhidi yenu hakika litatimizwa.’
Hii itakuwa ishara kwa ajili yako - hili ni tamko la Yahwe - kwamba ninaweka dhidi yenu katika eneo hili, ili kwamba mtajua kwamba maneno yangu hakika yatawavamia pamoja na maafa.
30 Hili ndilo asemalo Bwana: ‘Nitamtia Farao Hofra mfalme wa Misri mikononi mwa adui zake wanaoutafuta uhai wake, kama vile nilivyomtia Sedekia mfalme wa Yuda mikononi mwa Nebukadneza mfalme wa Babeli, adui aliyekuwa akiutafuta uhai wake.’”
Yahwe asema hivi, 'Tazama, ninakaribia kumtoa Farao Hofra mfalme wa Misri kwenye mkono wa adui zake na kwenye mkono wa wale wanaotafuta kumuua. Itakuwa sawa kama wakati nilimpa Sedekia mfalme wa Yuda kwenye mkono wa Nebukadreza mfalme wa Babeli, adui wake aliyetafuta maisha yake.

< Yeremia 44 >