< Yeremia 39 >
1 Hivi ndivyo Yerusalemu ilivyotwaliwa: Katika mwaka wa tisa wa utawala wa Mfalme Sedekia wa Yuda, katika mwezi wa kumi, Nebukadneza mfalme wa Babeli akiwa na jeshi lake lote alifanya vita dhidi ya Yerusalemu na akauzunguka mji.
Katika mwaka wa tisa na mwezi wa kumi wa Sedekia mfalme wa Yuda, Nebukadreza mfalme wa Babeli alikuja pamoja na jeshi lake lote dhidi ya Yerusalem na kuizingira.
2 Katika siku ya tisa ya mwezi wa nne wa mwaka wa kumi na moja wa utawala wa Sedekia, ukuta wa mji ulibomolewa.
Katika mwaka wa kumi na moja na mwezi wa nne wa Sekeia, siku ya tisa ya mwezi, mji uliharibiwa.
3 Kisha maafisa wote wa mfalme wa Babeli wakaja na kuketi kwenye Lango la Kati, nao ni: Nergal-Shareza wa Samgari, Nebo-Sarsekimu afisa mkuu, Nergal-Shareza afisa mwenye cheo cha juu, na maafisa wengine wote wa mfalme wa Babeli.
Kisha maafisa wote wa mfalme wa Babeli walikuja na kukaa kwenye lango la katikati: Nergali Sharezeri, Samgari Nebo, na Sarsechimu, afisa muhimu. Nerga Sharezeri alikuwa afisa mkuu na wote waliobaki maafisa wa mfalme wa Babeli.
4 Mfalme Sedekia wa Yuda na askari wote walipowaona, wakakimbia na kuondoka mjini usiku kwa njia ya bustani ya mfalme, kupitia lango lililokuwa kati ya kuta mbili, wakaelekea Araba.
Ilitokea kwamba wakati Sedekia, mfalme wa Yuda, na wanaume wapiganaji wake wote walipowaona, walikimbia. Walitoka nje usiku toka kwenye mji kwa njia ya bustani ya mfalme, kupitia lango la kati la kuta mbili. Mfalme alitoka nje katika mwelekeo wa Arabah.
5 Lakini jeshi la Wakaldayo likawafuatia na kumpata Sedekia katika sehemu tambarare za Yeriko. Wakamkamata na kumpeleka kwa Nebukadneza mfalme wa Babeli huko Ribla, katika nchi ya Hamathi, mahali ambapo alimtangazia hukumu.
Lakini jeshi la Wakaldayo walimfatilia na kumpata Sedekia kwenye tambarare za mto Yordani karibu na Yeriko. Kisha walimshika na kumleta kwa Nebukadreza, mfalme wa Babeli, Riblah kwenye nchi ya Hamath, ambapo Nebukadreza alipitisha sentensi juu yake.
6 Huko Ribla, mfalme wa Babeli aliwachinja wana wa Sedekia mbele ya macho yake, na pia akawaua wakuu wote wa Yuda.
Mfalme wa Babeli alimchinja binti wa Sedekia mbele ya macho yake huko Ribla. Pia aliwachinja wanaume wote wa heshima wa Yuda.
7 Kisha akayangʼoa macho ya Sedekia na kumfunga kwa pingu za shaba na kumpeleka Babeli.
Kisha alingoa macho ya Sedekia na kumfunga mnyororo wa shaba ili kusudi kumpeleka Babeli.
8 Jeshi la Wakaldayo likachoma moto jumba la kifalme na nyumba za watu, na kuzibomoa kuta za Yerusalemu.
Kisha Wakaldayo walichoma nyumba ya mfalme na nyumba za watu. Pia walivunja kuta za Yerusalem.
9 Nebuzaradani kiongozi wa walinzi wa mfalme akawachukua na kuwapeleka uhamishoni Babeli watu waliokuwa wamebaki ndani ya mji, pamoja na wale waliokuwa wamejisalimisha kwake, na watu wengine wote.
Nebukadreza, nahodha wa walinzi wa mfalme, waliwachukua katika mateka watu wengine waliobaki katika mji. Hii ilijumuisha watu waliotoka jangwa kwenda Wakaldayo na watu wengine walioachwa katika mji.
10 Lakini Nebuzaradani kiongozi wa walinzi aliwabakiza baadhi ya watu maskini katika nchi ya Yuda, ambao hawakuwa na kitu. Naye wakati huo akawapa mashamba ya mizabibu na mashamba mengine.
Lakini Nebukadreza nahodha wa walinzi wa mfalme aliwaruhusu watu maskini ambayo hawakuwa na chochote wao kubaki katika chi ya Yuda. Aliwapa mashamba ya mizabibu na maeneo katika siku ile.
11 Basi, Nebukadneza mfalme wa Babeli alikuwa ametoa maagizo kuhusu Yeremia kupitia Nebuzaradani kiongozi wa walinzi wa mfalme akisema:
Nebukadreza mfalme wa Babeli alikuwa ametoa amri kuhusu Yeremia kwa Nebuzaradani nahodha wa walinzi wa mfalme. Alikuwa amesema,
12 “Mchukue umtunze. Usimdhuru, lakini umfanyie chochote anachotaka.”
“Mchukue na umjali. Usimdhuru. Fanya kwa ajili yake chochote anachokuambia.”
13 Basi Nebuzaradani kiongozi wa walinzi, Nebushazbani afisa mkuu, Nergal-Shareza afisa wa cheo cha juu, na maafisa wengine wote wa mfalme wa Babeli
Basi Nebuzaradani nahodha wa walinzi wa mfalme, Nebushazbani mkuu wa matoashi, Nergali Sharezeri afisa mkuu, na wote maafisa wa muhimu wa mfalme wa Babeli walituma watu nje.
14 wakatuma watu kumwondoa Yeremia kutoka ua wa walinzi. Wakamkabidhi kwa Gedalia mwana wa Ahikamu mwana wa Shafani, ili amrudishe nyumbani kwake. Kwa hiyo akabaki miongoni mwa watu wake mwenyewe.
Watu wao walimchukua Yeremia kutoka uwanja wa mlinzi na kumkabidhi kwa Gedalia mwana wa Ahikami mwana wa Shafani, kumchua nyumbani, basi Yeremia alibaki miongoni mwa watu.
15 Wakati Yeremia alipokuwa amezuiliwa katika ua wa walinzi, neno la Bwana lilimjia kusema:
Sasa neno la Yahwe lilikuwa limekuja kwa Yeremia wakati alipokuwa chini ya kifungo kwenye uwanja wa mlinzi, na alisema,
16 “Nenda ukamwambie Ebed-Meleki Mkushi, ‘Hili ndilo Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo: Ninakaribia kutimiza maneno yangu dhidi ya mji huu kwa njia ya maafa, wala si kwa kuwafanikisha. Wakati huo hayo yatatimizwa mbele ya macho yako.
“Zungumza kwa Ebedi Meleki Mkushi na sema, 'Yahwe wa majeshi, Mungu wa Israel, asema hivi: Ona, Nimekaribia kubeba maneno yangu dhidi ya mji huu kwa ajili ya janga na si kwa uzuri. Kwa kuwa yatakuwa kweli mbele yako katika siku hiyo.
17 Lakini siku hiyo nitakuokoa, asema Bwana; hutatiwa mikononi mwa wale unaowaogopa.
Lakini nitakuokoa katika siku hiyo - hili ni tamko la Yahwe - na hautatiwa katika mkono wa wanaume ambayo unawaogopa.
18 Nitakuokoa; hutaanguka kwa upanga, lakini maisha yako yatakuwa salama, kwa sababu unanitumaini, asema Bwana.’”
Kwa kuwa nitakuokoa hakika. Hautaanguka kwa upanga. Utatoroka pamoja na maisha yako, kwani unanitumaini - hili lilikuwa tamko la Yahwe.”