< Yeremia 36 >
1 Katika mwaka wa nne wa Yehoyakimu mwana wa Yosia mfalme wa Yuda, neno hili lilimjia nabii Yeremia kutoka kwa Bwana, kusema:
And it came to pass in the fourth year of Jehoiakim, the son of Josiah, king of Judah, that this word came to Jeremiah from Jehovah, saying:
2 “Chukua kitabu uandike ndani yake maneno yote niliyonena nawe kuhusu Israeli, Yuda na mataifa mengine yote, tangu nilipoanza kunena nawe wakati wa utawala wa Yosia hadi sasa.
Take thee a book-roll, and write upon it all the words which I have spoken to thee concerning Israel, and concerning Judah, and concerning all the nations, from the day when I began to speak to thee even to this day.
3 Labda watu wa Yuda watakaposikia juu ya kila maafa ninayokusudia kuwapiga nayo, kila mmoja wao atageuka kutoka njia zake mbaya, kisha nitasamehe uovu wao na dhambi yao.”
It may be that the house of Judah will hear all the evil which I purpose to do to them, and return every one from his evil way, so that I may forgive their iniquity and their sin.
4 Hivyo Yeremia akamwita Baruku mwana wa Neria, naye Yeremia alipokuwa akiyakariri maneno yote aliyoyasema Bwana, Baruku akayaandika katika kitabu.
Then Jeremiah called Baruch, the son of Neriah; and Baruch wrote from the mouth of Jeremiah all the words of Jehovah which he had spoken to him, upon a book-roll.
5 Kisha Yeremia akamwambia Baruku, “Nimezuiliwa, mimi siwezi kuingia katika Hekalu la Bwana.
And Jeremiah commanded Baruch and said: I am shut up; I cannot go into the house of Jehovah;
6 Basi wewe nenda katika nyumba ya Bwana siku ya kufunga, uwasomee watu maneno ya Bwana kutoka kitabu hiki yale uliyoyaandika kutoka kinywani mwangu. Wasomee watu wote wa Yuda waliofika kutoka miji yao.
therefore, go thou, and read in the roll which thou hast written from my mouth the words of Jehovah, in the ears of the people, in the house of Jehovah, upon the fast-day; also in the ears of all Judah, that come out of their cities, shalt thou read them.
7 Labda wataomba na kusihi mbele za Bwana na kila mmoja akageuka kutoka njia zake mbaya, kwa sababu hasira na ghadhabu zilizotamkwa dhidi ya watu hawa na Bwana ni kubwa.”
It may be that they will prostrate themselves in supplication before Jehovah, and will return every one from his evil way. For great is the anger and the indignation which Jehovah hath denounced against this people.
8 Baruku mwana wa Neria akafanya kila kitu nabii Yeremia alichomwambia kufanya. Alisoma maneno ya Bwana katika Hekalu la Bwana kutoka kile kitabu.
And Baruch, the son of Neriah, did according to all that Jeremiah the prophet commanded him, reading in the book the words of Jehovah in the house of Jehovah.
9 Katika mwezi wa tisa, mnamo mwaka wa tano wa Yehoyakimu mwana wa Yosia mfalme wa Yuda, wakati wa kufunga mbele za Bwana, ilitangazwa kwa watu wote walioko Yerusalemu, na wale wote waliokuwa wamekuja kutoka miji ya Yuda.
And it came to pass in the fifth year of Jehoiakim, the son of Josiah, king of Judah, in the ninth month, that all the people in Jerusalem, and all the people that came out of the cities of Judah, proclaimed a fast before Jehovah, in Jerusalem.
10 Kutoka chumba cha Gemaria mwana wa Shafani mwandishi, kilichokuwa katika ua wa juu kwenye ingilio la Lango Jipya la Hekalu, Baruku akawasomea watu wote waliokuwa katika Hekalu la Bwana maneno ya Yeremia kutoka kwenye kile kitabu.
Then read Baruch in the book the words of Jeremiah in the house of Jehovah, in the chamber of Gemariah, the son of Shaphan the scribe, in the higher court, at the entrance of the new gate of the house of Jehovah, in the ears of all the people.
11 Basi Mikaya mwana wa Gemaria, mwana wa Shafani, aliposikia maneno yote ya Bwana kutoka kwenye kile kitabu,
And when Micah, the son of Gemariah, the son of Shaphan, had heard from the book all the words of Jehovah,
12 alishuka hadi kwenye chumba cha mwandishi kwenye jumba la kifalme, mahali walipokuwa wameketi maafisa wote: yaani Elishama mwandishi, Delaya mwana wa Shemaya, Elnathani mwana wa Akbori, Gemaria mwana wa Shafani, Sedekia mwana wa Hanania, na maafisa wengine wote.
he went down to the king's house, into the scribe's chamber; and lo, all the princes were sitting there, Elishama the scribe, and Delaiah, the son of Shemaiah, and Elnathan, the son of Achbor, and Gemariah, the son of Shaphan, and Zedekiah, the son of Hananiah, and all the princes.
13 Baada ya Mikaya kuwaambia kila kitu ambacho alikuwa amesikia Baruku akiwasomea watu kutoka kwenye kile kitabu,
Then Micah declared to them all the words which he had heard when Baruch read the book in the ears of the people.
14 maafisa wote wakamtuma Yehudi mwana wa Nethania, mwana wa Shelemia, mwana wa Kushi, kumwambia Baruku, “Leta hicho kitabu ambacho umewasomea watu, nawe mwenyewe uje.” Ndipo Baruku mwana wa Neria akawaendea akiwa na hicho kitabu mkononi mwake.
Then all the princes sent Jehudi, the son of Nethaniah, the son of Shelemiah, the son of Cushi, to Baruch, and said, “Take in thy hand the roll wherein thou hast read in the ears of the people, and come.” So Baruch, the son of Neriah, took the roll in his hand, and came to them.
15 Wakamwambia, “Tafadhali, keti na utusomee hicho kitabu.” Ndipo Baruku akawasomea kile kitabu.
And they said to him, “Sit down now, and read it in our ears.” And Baruch read it in their ears.
16 Walipoyasikia maneno hayo yote, wakatazamana wao kwa wao kwa woga na kumwambia Baruku, “Lazima tutoe taarifa ya maneno haya yote kwa mfalme.”
And when they had heard all the words, they looked with consternation upon one another, and they said to Baruch, “We must tell the king of all these things.”
17 Kisha wakamuuliza Baruku, “Tuambie, uliandikaje haya yote? Je, yalitoka kinywani mwa Yeremia?”
And they asked Baruch, saying, “Tell us now, how didst thou write all these words from his mouth?”
18 Baruku akajibu, “Ndiyo, maneno haya yote yalitoka kinywani mwa Yeremia, nami nikayaandika kwa wino katika hiki kitabu.”
And Baruch said to them, “With his mouth he pronounced to me all these words, and I wrote them on the book with ink.”
19 Ndipo wale maafisa wakamwambia Baruku, “Wewe na Yeremia nendeni mkajifiche. Mtu yeyote asijue mahali mlipo.”
Then said the princes to Baruch, “Go, hide thee, thou and Jeremiah, and let no man know where ye are.”
20 Baada ya kuhifadhi kile kitabu ndani ya chumba cha Elishama mwandishi, wakamwendea mfalme katika ua wa nje na kumwarifu kila kitu.
And they went in to the king into the court; but they laid up the roll in the chamber of Elishama the scribe, and they told all these things in the ears of the king.
21 Mfalme akamtuma Yehudi akachukue kile kitabu. Yehudi akakileta hicho kitabu kutoka kwenye chumba cha Elishama mwandishi, na akakisoma mbele ya mfalme na maafisa wakiwa wamesimama kando ya mfalme.
Then the king sent Jehudi to fetch the roll, and he took it out of the chamber of Elishama the scribe; and Jehudi read it in the ears of the king, and in the ears of all the princes who stood beside the king.
22 Ulikuwa mwezi wa tisa, na mfalme alikuwa ameketi chumba cha wakati wa baridi akiota moto.
And the king was sitting in the winter-house, in the ninth month, and a brasier was burning before him.
23 Hata ikawa kila wakati Yehudi alipomaliza kusoma kurasa tatu au nne za hicho kitabu, mfalme alizikata kwa kisu cha mwandishi na kuzitupia motoni, hadi kitabu chote kikateketea.
And when Jehudi had read three or four sections, he [[the king]] cut it with the penknife, and cast it into the fire, into the brasier, until the whole roll was consumed in the fire in the brasier.
24 Mfalme na watumishi wake wote waliosikia yote yaliyosomwa hawakuonyesha hofu yoyote, wala hawakuyararua mavazi yao.
And they were not afraid, and rent not their garments, neither the king, nor any of his servants, who heard all these words;
25 Hata ingawa Elnathani, Delaya na Gemaria walimsihi mfalme asikichome kile kitabu, yeye hakuwasikiliza.
and although Elnathan and Delaiah and Gemariah interceded with the king not to burn the roll, yet he would not hearken to them.
26 Badala yake, mfalme akamwamuru Yerameeli, mwana wa mfalme, Seraya mwana wa Azrieli, na Shelemia mwana wa Abdeeli kuwakamata mwandishi Baruku na nabii Yeremia. Lakini Bwana alikuwa amewaficha.
And the king commanded Jerahmeel, the son of Hammelech, and Seraiah, the son of Azreel, and Shelemiah, the son of Abdeel, to seize Baruch the scribe, and Jeremiah the prophet; but Jehovah had hid them.
27 Baada ya mfalme kuchoma kile kitabu kilichokuwa na yale maneno Baruku aliyokuwa ameyaandika kutoka kinywani mwa Yeremia, neno la Bwana lilimjia Yeremia likisema:
Then came the word of Jehovah to Jeremiah, after that the king had burned the roll, and the words which Baruch had written from the mouth of Jeremiah, saying:
28 “Chukua kitabu kingine na uandike juu yake maneno yote yaliyokuwa katika kile kitabu cha kwanza, ambacho Yehoyakimu mfalme wa Yuda amekiteketeza kwa moto.
Take thee another roll, and write in it all the former words that were in the first roll, which Jehoiakim, king of Judah, hath burned.
29 Mwambie pia Yehoyakimu mfalme wa Yuda, ‘Hili ndilo asemalo Bwana: Ulikiteketeza kile kitabu ukasema, “Kwa nini uliandika kwenye kitabu kwamba kwa hakika mfalme wa Babeli angekuja na kuangamiza nchi hii, na kuwakatilia mbali watu na wanyama kutoka humo?”
And concerning Jehoiakim, king of Judah, thou shalt say, Thou hast burned this roll, saying, “Why hast thou written therein and said, The king of Babylon shall surely come and shall destroy this land, and shall cause to cease from it man and beast?”
30 Kwa hiyo, hili ndilo asemalo Bwana kuhusu Yehoyakimu mfalme wa Yuda: Hatakuwa na mtu yeyote atakayekalia kiti cha enzi cha Daudi; maiti yake itatupwa nje kwenye joto wakati wa mchana na kupigwa na baridi wakati wa usiku.
Therefore thus saith Jehovah concerning Jehoiakim, king of Judah: He shall have not one to sit upon the throne of David; and his dead body shall be cast out in the day to the heat, and in the night to the frost.
31 Nitamwadhibu yeye, watoto wake na watumishi wake kwa ajili ya uovu wao. Nitaleta juu yao na wote waishio Yerusalemu na watu wa Yuda kila maafa niliyoyasema dhidi yao, kwa sababu hawajasikiliza.’”
And I will punish him, and his offspring, and his servants, for their iniquity; and I will bring upon them, and upon the inhabitants of Jerusalem, and upon the men of Judah, all the evil which I have pronounced against them, and they have not hearkened.
32 Kisha Yeremia akachukua kitabu kingine na kumpa mwandishi Baruku mwana wa Neria, naye kama Yeremia alivyosema, Baruku akaandika juu yake maneno yote ya kile kitabu ambacho Yehoyakimu mfalme wa Yuda alikuwa amekichoma moto, na maneno mengine mengi yaliyofanana na hayo yaliyoongezewa humo.
Then Jeremiah took another roll, and gave it to Baruch the scribe, the son of Neriah, who wrote therein from the mouth of Jeremiah all the words of the book which Jehoiakim had burned in the fire; and there were added to them many words of the same kind.