< Yeremia 31 >

1 “Wakati huo, nitakuwa Mungu wa koo zote za Israeli nao watakuwa watu wangu,” asema Bwana.
“Katika wakati huo—hili ni tangazo la Yahwe—Nitakuwa Mungu wa familia zote za Israel, na watakuwa watu wangu.”
2 Hili ndilo asemalo Bwana: “Watu watakaopona upanga watapata upendeleo jangwani; nitakuja niwape Israeli pumziko.”
Yahwe anasema hivi, “Watu ambao wamenusurika na upanga wamepata kibali katika nyika; nitatoka nje kuwapa pumziko Israeli.”
3 Bwana alitutokea wakati uliopita, akisema: “Nimekupenda kwa upendo wa milele, nimekuvuta kwa wema.
Yahwe alionitokea zamani na kusema, “Nimekupenda wewe, Israeli, kwa upendo wa milele. Kwa hiyo nimekuvuta kwang kwa agano la uaminifu.
4 Nitakujenga tena nawe utajengeka upya, ewe Bikira Israeli. Utachukua tena matari yako na kwenda kucheza na wenye furaha.
Nitakujenga tena kwa hiyo utakuwa umejengwa, bikra wa Israeli..... na kwenda nje michezo ya furaha.
5 Utapanda tena shamba la mizabibu juu ya vilima vya Samaria, wakulima watapanda na kufurahia matunda yake.
Utapanda mizabibu tena juu ya milima Samaria; wakulima watatapanda na kuweka matunda kwa ajili ya matumizi mazuri.
6 Itakuja siku wakati walinzi watakapowapigia kelele juu ya vilima vya Efraimu wakisema, ‘Njooni, twendeni juu Sayuni, kwake Bwana Mungu wetu.’”
Kwa maana siku itakuja wakati walizi watakapotangaza katika milima ya Efraimu, 'Inuka, twndeni juu kwenye mlimaa wa Yahwe Mungu wetu.'
7 Hili ndilo asemalo Bwana: “Mwimbieni Yakobo kwa furaha, mpigieni kelele aliye mkuu wa mataifa. Zifanyeni sifa zenu zisikike, nanyi mseme, ‘Ee Bwana, okoa watu wako, mabaki ya Israeli.’
Kwa maana Yahwe anasema hivi, Piga kelele za shangwe juu ya Yakobo! Pigeni za furaha kwa ajili ya watu wakuu wa mataifa! Sifa zisikike. Sema, ''Yahwe amewaokoa watu wake, masalia wa Israeli.'
8 Tazama, nitawaleta kutoka nchi ya kaskazini na kuwakusanya kutoka miisho ya dunia. Miongoni mwao watakuwepo vipofu na viwete, mama wajawazito na wenye utungu wa kuzaa. Umati mkubwa wa watu utarudi.
Ona, niko karibu kuwaletaa kutoka nchi za kusini. Nitawakusanya kutoka sehemu zaa mbali za dunia. Vipofu na wenye ulemavu watakuwa kati kati yao; wanawake wajawazito na wale waliokaribu kujifungua wataakuwa pamoja nao. Kusanyiko kubwa litarudi hapa.
9 Watakuja wakilia; wataomba wakati ninawarudisha. Nitawaongoza kando ya vijito vya maji katika mapito yaliyo tambarare ambapo hawatajikwaa, kwa sababu mimi ndimi baba wa Israeli, naye Efraimu ni mzaliwa wangu wa kwanza.
Watakuja kwa kuomboleza; nitawaongoza huku wakifanya maoambi yao. Nitawafanya wasafiri kataika mikondo ya maji katika bara bara ilinyoka. Hawatajikwaa juu yake, kwa maana nitakuwa baba kwa Israeli, na Afraimu atakuwa mzaliwa wanagau wwa kwanza
10 “Sikieni neno la Bwana, enyi mataifa, litangazeni katika nchi za pwani ya mbali: ‘Yeye aliyewatawanya Israeli atawakusanya na atalichunga kundi lake la kondoo kama mchungaji.’
Sikia neno la Yahwe, mataifa. Litangazeni pembezoni mwa visiwa mbali. Enyi mataifa lazima museme, 'Yule aliyemtawanya Israeli anamkusanya tena na kuwalinda kama mchungaji alindavyo kondoo.'
11 Kwa kuwa Bwana atamlipia fidia Yakobo na kuwakomboa mkononi mwa walio na nguvu kuliko wao.
Kwa maana Yahwe amemfidia Yakobo na kumkomboa kutoka mkono ambao ulikuwa na nguvu sana kwake.
12 Watakuja na kupiga kelele kwa furaha katika miinuko ya Sayuni; watashangilia ukarimu wa Bwana: nafaka, divai mpya na mafuta, wana-kondoo wachanga na ndama wa makundi ya ngʼombe nitakaowapa. Watakuwa kama bustani iliyonyeshewa vizuri, wala hawatahuzunika tena.
Kisha watakuja na kufurahia katika vilele vya Sayuni. Nyuso zao zitamelemeta kwa sababu ya wema wa Yahwe, juu ya nafaka na divai mpya, juu ya mafuta na malimbuko ya kwanza ya makundi na ng'ombe. Kwa maana maisha yao yatakuwa kama busitani iliyomwagiliwa, na hatatajisikia huzuni tena.
13 Kisha wanawali watacheza na kufurahi, vijana waume na wazee pia. Nitageuza maombolezo yao kuwa furaha, nitawapa faraja na furaha badala ya huzuni.
Kisha wanawali watafurahia kwa kucheza, na vijana na wanaume wazee watakuwa pamaoja. Kwa maana nitayageuza maombolezo yao kuwa sherehe. Nitakuwa na huruma juu yao na kuwafanya kufurahi badala ya kuhuzunika.
14 Nitawashibisha makuhani kwa wingi, nao watu wangu watajazwa kwa ukarimu wangu,” asema Bwana.
Kisha nitayaloanaisha sana maisha ya makuhani. Watu wangu watajijaza wenyewe kwa wema—hili ni tangazo la Yahwe.”
15 Hili ndilo asemalo Bwana: “Sauti imesikika huko Rama, maombolezo na kilio kikubwa, Raheli akiwalilia watoto wake na anakataa kufarijiwa, kwa sababu watoto wake hawako tena.”
Yahwe anasema hivi: “Sauti imesikika katika Rama, kilio na maombolezo mengi. Ni Raheli akiomboleza kwa ajili watoto wake. Hataki kufarijiwa tena juu yao, kwa maana hawako hai tena.”
16 Hili ndilo asemalo Bwana: “Izuie sauti yako kulia, na macho yako yasitoe machozi, kwa kuwa kazi yako itapata thawabu,” asema Bwana. “Watarudi kutoka nchi ya adui.
Yahwe anasema hivi, Zuia sauti yako usilie na macho yako yasitoe machizi; kwa maana kuna fidia kwa ajili ya mateso yako—hili ni tangazo la Yahwe—watoto wako watarudi kutoka nchi ya adui.
17 Kwa hiyo kuna tumaini kwa siku zijazo,” asema Bwana. “Watoto wako watarudi nchi yao yenyewe.
Kuna matumaini kwa ajili ya siku zenu za baadaye—hili ni tangazo la Yahwe—uzao wako watarudi ndani ya mipaka yao.”
18 “Hakika nimeyasikia maombolezo ya Efraimu: ‘Ulinirudi kama ndama mkaidi, nami nimekubali kutii. Unirudishe, nami nitarudi, kwa sababu wewe ndiwe Bwana, Mungu wangu.
Kwa hakika nimemsikia Efraimu akilia, 'Uliniadhibu, nami nieadhibika kama ndama assiye na mafunzo. Nirudisha na nitarudishwa, kwa maana wewe ni Yahwe Mungu wangu.
19 Baada ya kupotea, nilitubu; baada ya kuelewa, nilijipiga kifua. Niliaibika na kuona haya kwa sababu niliibeba aibu ya ujana wangu.’
Kwa maana baada ya kurudi kwako, nilikuwa na huzuni; baada ya kufundiswa, nilijipiga kofi sshavu langu. Niliaibika ana dharirika, kwa maana nilizaliwa na hataia ya ujana wangu.'
20 Je, Efraimu si mwanangu mpendwa, mtoto ninayependezwa naye? Ingawa mara kwa mara ninanena dhidi yake, bado ninamkumbuka. Kwa hiyo moyo wangu unamwonea shauku, nina huruma kubwa kwa ajili yake,” asema Bwana.
Efraimu siyo mtoto wangu wa thamani? Yeye si mpendwa wangu, mwanangu anipendezaye? Kwa maana kila ninaponena juu yake, bado nina mwita kipenzi cha akili yangu. Kwa namna hii moyo wangu unamtamani. Kwa hakika nitaakuwa na huruma ajuu yake—hili ni tangazo la Yahwe.”
21 “Weka alama za barabara, weka vibao vya kuelekeza. Zingatia vyema njia kuu, barabara ile unayoipita. Rudi, ee Bikira Israeli, rudi kwenye miji yako.
Jiwekee alama za bara bara kwa ajili yako mwenyewe. Weka matangaazo ya maelekezo kwa ajili yako mwenyewe. Iweke akili yako juu ya njia sahihi, njia unayopaswa kufuata. Rudii, bikra Israeli! Rudi kwenye hii miji yako.
22 Utatangatanga hata lini, ee binti usiye mwaminifu? Bwana ameumba kitu kipya duniani: mwanamke atamlinda mwanaume.”
Utatanga tanga hadi lini, binti usiye mwaminifu? Kwa maana Yahwe ameumba kitu fulani kipya juu ya dunia—mwanamke anamzunguka mwanaume.
23 Hili ndilo Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo, “Nitakapowarudisha toka nchi ya kutekwa kwenu, watu walio katika nchi ya Yuda na miji yake kwa mara nyingine tena watatumia maneno haya: ‘Bwana akubariki, ee makao ya haki, ee mlima mtakatifu.’
Yahwe wa majeshi, Mungu wa Israeli, anasema hivi, '“Nitakapowarudisha watu katika nchi yao, watasema hivi katika anchi ya Yuda na miji yake, “Yahwe akubariki, wewe sehemu takatifu ambapo anaishi, ewe mlima mtakatifu.'
24 Watu wataishi pamoja katika Yuda na miji yake yote, wakulima na wote wanaohamahama na mifugo yao.
Kwa maana Yuda na miji yake yote wataishi pamoja humo, kama vile watakavyoishi wakulima na wachungaji pamaoja na makundi yao.
25 Nitawaburudisha waliochoka na kuwatuliza walio na huzuni.”
Kwa maana nitawapa majai ya kunywa waliochoaka, na nitamjaza kila anayeteseka na kiu.”
26 Kwa jambo hili niliamka na kuangalia pande zote. Usingizi wangu ulikuwa mtamu kwangu.
Baada ya haya niliamka, na nikagundua kwamba usingizi wangu ulikuwa unaburudisha.
27 Bwana asema, “Siku zinakuja, nitakapoongeza idadi ya watu, na kuzidisha hesabu ya mifugo katika nyumba ya Israeli na nyumba ya Yuda.
Angalia, siku zinakuja—hili ni tangazo la Yaahwe—nitakapoipanda nyumba ua Israeli na Yuda pamoja na wazawa wa wanadamaau na wanyama.
28 Kama vile nilivyowaangalia ili kungʼoa na kubomoa, kuharibu, kuangamiza na kuleta maafa juu yao, vivyo hivyo nitawaangalia ili kujenga na kupanda,” asema Bwana.
Zamani, niliwaweka katika uangalizi ili kuwang'oa na kuwabomoa, kuwaangusha, kuwaharibu, na kuwaletea madhara. Lakini katika siku zijazo, nitawaangalia, ili niwajenge na kuwapanda—hili ji tangazo la Yahwe.
29 “Katika siku hizo, watu hawatasema tena, “‘Baba wamekula zabibu chachu, nayo meno ya watoto yakatiwa ganzi.’
Katika siku hizo hakuna atakayesema tena, “Baba za watu wamekula zabibu kali, bali meno ya watoto ni butu.'
30 Badala yake, kila mmoja atakufa kwa ajili ya dhambi zake mwenyewe; yeyote alaye zabibu chachu, meno yake mwenyewe yatatiwa ganzi.
Kwa maana kila mtu atakuwa katika uovu wake mwenyewe; kila alaye zabibu kalai, meno yake yataakuwa butu.
31 “Siku zinakuja,” asema Bwana, “nitakapofanya agano jipya na nyumba ya Israeli na nyumba ya Yuda.
Angalia, siku zinakuja—hili ni tangazo la Yahwe—nitakapoanzisha aganao jipya pamaoja na nyumba aya Israeli na nyumba ya Yuda.
32 Halitafanana na agano nililofanya na baba zao wakati nilipowashika mkono kuwaongoza watoke Misri, kwa sababu walivunja agano langu, ijapokuwa nilikuwa mume kwao,” asema Bwana.
Halitakuwa kama agano ambalo nilianzisha na baba zao nilipowatoa kwa mkono wao nje ya nchi ya Missiri. Hizo zzilikuwa siku ambapo walilivunja aaganao lanaahu, ingawa nilikuwa mme kwao—hili ni tangazo la Yahwe.
33 “Hili ndilo agano nitakalofanya na nyumba ya Israeli baada ya siku zile,” asema Bwana. “Nitaweka sheria yangu katika nia zao, na kuiandika mioyoni mwao. Nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.
Lakaini hili ni agano nitakaloanzisha na nyumba ya Israeli baada ya siku hizi—hili ni tangazo la Yahwe: Nitaiweka sheria yangu ndani yao na nitaiandika juu ya mioyo yao, kwa maana nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watau wangu.
34 Mtu hatamfundisha tena jirani yake, wala mtu kumfundisha ndugu yake akisema, ‘Mjue Bwana Mungu,’ kwa sababu wote watanijua mimi, tangu aliye mdogo kabisa kwao, hadi aliye mkuu sana,” asema Bwana. “Kwa sababu nitasamehe uovu wao, wala sitazikumbuka dhambi zao tena.”
Kisha kila mtu hatamfundisha jiranai yake, wala mtu hatamfundisha ngugu yake akisema, 'Mjue Yahwe!' Kwa maana wao wote, kuanzia mdogo wao hata mkubwa, watanijua—hili ni tangazo la Yahwe—kwa maana nitawasamehe uovu wao na sitazikumbuka tena dhambi zao.”'
35 Hili ndilo asemalo Bwana, yeye aliyeweka jua liwake mchana, yeye anayeamuru mwezi na nyota kungʼaa usiku, yeye aichafuaye bahari ili mawimbi yake yangurume; Bwana Mwenye Nguvu Zote ndilo jina lake:
Yahwe anasema hivi—Yahwe, yeye afanyaye jua kuangaza mchana na kuzipanga mwezi na nyota kuangaza usiku. Yeye ndiye aiwekaye bahari katika mwendo ili mawimbi yake yaungurume. Yahwe wa majeshi katika ajina lake.
36 “Ikiwa amri hizi zitaondoka machoni pangu,” asema Bwana, “ndipo wazao wa Israeli watakoma kuwa taifa mbele yangu daima.”
Anasema hivi, ikiwa tu mambo haya ya akudumu yakitoweka machoni panaagu—hili ni agizo la Yahwe—uzao wa Israeli hawatasimama mbaalai nami wasiwe taiafa.”
37 Hili ndilo asemalo Bwana: “Ikiwa mbingu zilizo juu zitaweza kupimika na misingi ya dunia chini ikaweza kuchunguzwa, ndipo nitakapowakataa wazao wote wa Israeli kwa sababu ya yote waliyoyatenda,” asema Bwana.
Yahwe anasema hivi, “Kama tu urefu wa mbingu unaweza kupimwa, na kama tu misingi ya dunia chini inaweza kugunduliwa, nitawakataa uzao wote wa Israeli kwa sababu ya yote waliyofanya—hili ni tangazo la Yahwe.”
38 “Siku zinakuja,” asema Bwana, “wakati mji huu utajengwa upya kwa ajili yangu, kuanzia mnara wa Hananeli hadi Lango la Pembeni.
“Angalia, siku zinakuja—hili ni tanagazo la Yahwe—ambapo mji utajengwa tena kwa ajili yanagu, kutoka Mnara wa Hananeli hadi kwenye Lango la Pembeni.
39 Kamba ya kupimia itaanzia hapo kuendelea hadi kwenye kilima cha Garebu, na kisha kugeuka kuelekea Goa.
Kisha mistari ya kupimia itaenda nje hadi mbali, hadi kwenye kilima cha Garebu na kuzunguka Goa.
40 Bonde lote watupwapo maiti na majivu pia na matuta yote kutoka Bonde la Kidroni upande wa mashariki hadi pembe ya Lango la Farasi, itakuwa takatifu kwa Bwana. Kamwe mji huu hautangʼolewa tena wala kubomolewa.”
Bonde lote la miili iliyokufa na majivu, na shamaba lenye matuta linalofika hadi Bonde la Kidroni mbali hadi kwenye kona ya Lango la Farasi upande wa mashariki, litateuliwa kwa ajili ya Yahwe. Mji hautang'olewa wala kupinduliwa tena, milele.”

< Yeremia 31 >