< Yeremia 27 >

1 Mwanzoni mwa utawala wa Yehoyakimu mwana wa Yosia mfalme wa Yuda, neno hili lilimjia Yeremia kutoka kwa Bwana:
In the beginning of the reign of Zedekiah, the son of Josiah, king of Judah, came this word to Jeremiah from Jehovah.
2 Hili ndilo Bwana aliloniambia: “Tengeneza nira, ujivike shingoni mwako, uifunge kwa kamba za ngozi.
Thus said Jehovah to me: Make thee bands and yokes, and put them upon thy neck,
3 Kisha utume ujumbe kwa wafalme wa Edomu, Moabu, Amoni, Tiro na Sidoni kupitia wajumbe ambao wamekuja Yerusalemu kwa Sedekia mfalme wa Yuda.
and send them to the king of Edom, and to the king of Moab, and to the king of the children of Ammon, and to the king of Tyre, and to the king of Zidon, by the hands of the messengers that are come to Jerusalem, to Zedekiah, king of Judah.
4 Wape ujumbe kwa ajili ya mabwana zao na uwaambie: Hili ndilo asemalo Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli: ‘Waambieni hivi mabwana zenu:
And command them to say to their masters, Thus saith Jehovah of hosts, the God of Israel: Thus shall ye say to your masters:
5 Kwa uwezo wangu mkuu na kwa mkono wangu ulionyooshwa nimeumba dunia na watu wake na wanyama walioko ndani yake, nami humpa yeyote inipendezavyo.
The earth, and the men and the beasts which are upon the earth, have I made by my great power and my outstretched arm, and I give it to whomsoever it seemeth meet to me.
6 Sasa nitazitia nchi zenu zote mkononi mwa mtumishi wangu Nebukadneza mfalme wa Babeli, na nitawafanya hata wanyama wa mwituni wamtumikie.
And now I give all these lands into the hand of Nebuchadnezzar, the king of Babylon, my servant; the beasts of the field also I give him to serve him.
7 Mataifa yote yatamtumikia yeye, pamoja na mwanawe na mwana wa mwanawe, hadi wakati wa nchi yake utakapowadia, kisha mataifa mengi na wafalme wenye nguvu nyingi watamshinda.
And all nations shall serve him, and his son, and his son's son, until the time of his land, even his, shall come, and then shall many nations and great kings make him their servant.
8 “‘“Lakini kama kukiwa na taifa lolote au ufalme ambao hautamtumikia Nebukadneza mfalme wa Babeli, ama kuinamisha shingo yake chini ya nira yake, nitaliadhibu taifa hilo kwa upanga, njaa na tauni, asema Bwana, mpaka nitakapoliangamiza taifa hilo kwa mkono wake.
And the nation and the kingdom that will not serve him, Nebuchadnezzar, the king of Babylon, and put their neck under the yoke of the king of Babylon, —with the sword and with famine and with pestilence will I punish that nation, saith Jehovah, until I have consumed them by his hand.
9 Kwa hiyo msiwasikilize manabii wenu, waaguzi wenu, waota ndoto wenu, watabiri na wachawi wanaowaambia ninyi: Hamtamtumikia mfalme wa Babeli.
Therefore hearken ye not to your prophets, and your diviners, and your dreamers, your soothsayers, and your sorcerers, who say to you, Ye shall not serve the king of Babylon.
10 Wanawatabiria uongo ambao utawafanya ninyi mhamishwe mbali kutoka nchi yenu. Nitawafukuzia mbali, nanyi mtaangamia.
For they prophesy a lie to you, to remove you far from your land, and that I should drive you out, and that ye should perish.
11 Lakini ikiwa taifa lolote litainama na kuweka shingo lake katika nira ya mfalme wa Babeli na kumtumikia, nitaliacha taifa hilo katika nchi yake yenyewe ili wailime na kuishi humo, asema Bwana.”’”
But the nations that bring their neck under the yoke of the king of Babylon, and serve him, those will I let remain still in their own land, saith Jehovah, and they shall till it, and dwell therein.
12 Nilitoa ujumbe huo huo kwa Sedekia mfalme wa Yuda. Nilisema, “Ingiza shingo yako katika nira ya mfalme wa Babeli, umtumikie yeye na watu wake, nawe utaishi.
And to Zedekiah, king of Judah, also, spake I according to all these words, and said: Bring your necks under the yoke of the king of Babylon, and serve him and his people, and live.
13 Kwa nini wewe na watu wako mfe kwa upanga, njaa na tauni, ambazo Bwana ameonya juu ya taifa lolote ambalo halitamtumikia mfalme wa Babeli?
Why will ye die, thou and thy people, by the sword, by famine, and by pestilence, as Jehovah hath spoken concerning the nation that will not serve the king of Babylon?
14 Msiyasikilize maneno ya manabii wanaowaambia kwamba, ‘Hamtamtumikia mfalme wa Babeli,’ kwa sababu wanawatabiria uongo.
Therefore hearken not to the prophets, that say to you, Ye shall not serve the king of Babylon; for they prophesy a lie to you.
15 ‘Sikuwatuma hao,’ asema Bwana. ‘Wanatabiri uongo kwa jina langu. Kwa hiyo, nitawafukuzia mbali, nanyi mtaangamia, ninyi pamoja na manabii wanaowatabiria.’”
For I have not sent them, saith Jehovah; but they prophesy a lie in my name, that I may drive you out, and that ye may perish, ye and the prophets that prophesy to you.
16 Kisha nikawaambia makuhani na watu hawa wote, “Hili ndilo asemalo Bwana: Msiwasikilize manabii wanaosema, ‘Hivi karibuni sana vyombo vya nyumba ya Bwana vitarudishwa kutoka Babeli.’ Wanawatabiria ninyi uongo.
To the priests, also, and to all the people; spake I, saying, Thus saith Jehovah: Hearken not to the words of your prophets who prophesy to you, and say, Behold the vessels of the house of Jehovah shall be brought back from Babylon now shortly; for they prophesy a lie to you.
17 Msiwasikilize. Mtumikieni mfalme wa Babeli, nanyi mtaishi. Kwa nini mji huu uwe magofu?
Hearken ye not to them; serve the king of Babylon, and live! Why should this city become a desolation?
18 Kama wao ni manabii na wanalo neno la Bwana, basi na wamsihi Bwana Mwenye Nguvu Zote ili vyombo vilivyobaki katika nyumba ya Bwana na katika jumba la kifalme la mfalme wa Yuda na katika Yerusalemu visipelekwe Babeli.
But if they be indeed prophets, and if the word of Jehovah be with them, let them now make intercession to Jehovah of hosts, that the vessels which are left in the house of Jehovah, and in the house of the king of Judah, and in Jerusalem, may not go to Babylon.
19 Kwa maana hili ndilo asemalo Bwana Mwenye Nguvu Zote kuhusu zile nguzo, ile Bahari, vile vishikizo viwezavyo kuhamishika, vinara na vyombo vingine vilivyoachwa katika mji huu,
For thus saith Jehovah of hosts concerning the pillars, and concerning the sea, and concerning the bases, and concerning the residue of the vessels that are let in this city,
20 ambavyo Nebukadneza mfalme wa Babeli hakuvichukua wakati alipomchukua Yekonia mwana wa Yehoyakimu mfalme wa Yuda kwenda uhamishoni huko Babeli kutoka Yerusalemu, pamoja na wakuu wote wa Yuda na Yerusalemu.
which Nebuchadnezzar, king of Babylon, took not, when he carried away captive Jeconiah, the son of Jehoiakim, king of Judah, from Jerusalem to Babylon, with all the nobles of Judah and Jerusalem;
21 Naam, hili ndilo Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo kuhusu vitu ambavyo vimebaki ndani ya nyumba ya Bwana, na ndani ya jumba la kifalme la mfalme wa Yuda, na katika Yerusalemu:
yea, thus saith Jehovah of hosts, the God of Israel, concerning the vessels that are left in the house of Jehovah, and in the house of the king of Judah and of Jerusalem:
22 ‘Vitachukuliwa kupelekwa Babeli, nako huko vitabaki mpaka siku nitakayovijilia,’ asema Bwana. ‘Kisha nitavirudisha na kuvirejesha mahali hapa.’”
They shall be carried to Babylon, and there shall they be until the day when I shall visit them, saith Jehovah. Then will I bring them up, and restore them to this place.

< Yeremia 27 >