< Yeremia 21 >

1 Neno lilimjia Yeremia kutoka kwa Bwana wakati Mfalme Sedekia alipowatuma Pashuri mwana wa Malkiya, na kuhani Sefania mwana wa Maaseya kwake, kusema:
Hili ndilo neno lililotoka kwa Bwana kwa Yeremia wakati mfalme Sedekia alimtuma Pashuri mwana wa Malkiya na Sefania mwana wa Maaseya, kuhani. Wakamwambia,
2 “Tuulizie sasa kwa Bwana, kwa sababu Nebukadneza mfalme wa Babeli anatushambulia. Labda Bwana atatenda maajabu kwa ajili yetu kama nyakati zilizopita, ili Nebukadneza atuondokee.”
“Pata ushauri kutoka kwa Bwana kwa ajili yetu, kwa kuwa Nebukadreza, mfalme wa Babeli, analeta vita. Labda Bwana atafanya miujiza kwetu, kama ilivyokuwa zamani, na kumfanya aondoke kwetu.”
3 Lakini Yeremia akawajibu, “Mwambieni Sedekia,
Basi Yeremia akawaambia, “Hivi ndivyo mtakavyomwambia Sedekia
4 ‘Hili ndilo Bwana, Mungu wa Israeli, asemalo: Ninakaribia kuwageuzia silaha za vita zilizo mikononi mwenu, ambazo mnatumia kupigana na mfalme wa Babeli na Wakaldayo ambao wako nje ya ukuta wakiwazunguka kwa jeshi. Nami nitawakusanya ndani ya mji huu.
'Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi: Tazama, niageuza nyuma vyombo vya vita vilivyo mkononi mwenu, ambavyo mnapigana dhidi ya mfalme wa Babeli na Wakaldayo wanaokufunga kutoka nje ya kuta! Kwa maana nitawakusanya katikati ya jiji hili.
5 Mimi mwenyewe nitapigana dhidi yenu kwa mkono wangu ulionyooshwa na mkono wa nguvu, kwa hasira na ghadhabu kali na ukali mwingi.
Nami nitapigana nanyi kwa mkono ulioinuka na mkono wenye nguvu, na ukali, ghadhabu, na hasira kubwa.
6 Nitawaangamiza waishio katika mji huu, watu na wanyama, nao watauawa kwa tauni ya kutisha.
Kwa maana nitawaangamiza wenyeji wa mji huu, wanadamu na wanyama, watakufa kwa tauni kali.
7 Baada ya hayo, nitamtia Sedekia mfalme wa Yuda, maafisa wake na watu wa mji huu ambao walinusurika tauni, upanga na njaa, mkononi mwa Nebukadneza mfalme wa Babeli, na kwa adui zao wale wanaotafuta uhai wao. Atawaua kwa upanga; hatakuwa na rehema juu yao au huruma wala kuwasikitikia,’ asema Bwana.
Baada ya hayo- hii ndiyo ahadi ya Bwana-Sedekia mfalme wa Yuda, watumishi wake, watu, na kila mtu aishiye katika mji huu baada ya tauni, upanga na njaa, nitawatia wote mkononi mwa Nebukadreza mfalme wa Babeli, na mikononi mwa adui zao, na katika mkono wa wale wanaotaka uhai wao. Ndipo atawaua kwa makali ya upanga. Hatawahurumia, hatawaokoa, au kuwa na rehema.'
8 “Zaidi ya hayo, waambie watu hawa, ‘Hili ndilo asemalo Bwana: Tazama, naweka mbele yenu njia ya uzima, na njia ya mauti.
Basi uwaambie watu hawa, 'Bwana asema hivi Angalia, nitaweka mbele yako njia ya uzima na njia ya mauti.
9 Yeyote atakayekaa katika mji huu atakufa kwa upanga, njaa au tauni. Lakini yeyote atakayetoka na kujisalimisha kwa Wakaldayo ambao wameuzunguka mji huu kwa jeshi, atanusurika, naye ataishi.
Mtu yeyote anayeishi katika mji huu atakufa kwa upanga, njaa, na tauni; lakini mtu yeyote atakayetoka na kuanguka kwa magoti mbele ya Wakaldayo ambao wamefungwa dhidi yako ataishi. Yeye ataokoka na maisha yake.
10 Nimekusudia kuufanyia mji huu jambo baya, wala si jema. Utatiwa mikononi mwa mfalme wa Babeli, naye atauteketeza kwa moto, asema Bwana.’
Kwa maana nimeweka uso wangu juu ya mji huu ili kuleta maafa na sio kuleta mema-hili ndilo tamko la Bwana. Utatiwa mkononi mwa mfalme wa Babeli naye atauteketeza.'
11 “Zaidi ya hayo, ambia nyumba ya mfalme ya Yuda, ‘Sikia neno la Bwana,
Kuhusu nyumba ya mfalme wa Yuda, sikiliza neno la Bwana.
12 Ewe nyumba ya Daudi, hili ndilo Bwana asemalo: “‘Hukumuni kwa haki kila asubuhi, mwokoeni mikononi mwa mdhalimu yeye aliyetekwa nyara, la sivyo ghadhabu yangu italipuka na kuwaka kama moto kwa sababu ya uovu mlioufanya: itawaka na hakuna wa kuizima.
Nyumba ya Daudi, Bwana asema, “Hukumuni kwa haki asubuhi. Umuokoe yule aliyeibiwa kwa mkono wa mwenye kuonea, au ghadhabu yangu itatoka kama moto na kuchoma, na hakuna mtu anayeweza kuizima, kwa sababu ya matendo yako mabaya.
13 Niko kinyume nawe, ee Yerusalemu, wewe uishiye juu ya bonde hili kwenye uwanda wa juu wa miamba, asema Bwana, wewe usemaye, “Ni nani awezaye kuja kinyume chetu? Nani ataingia mahali pa kimbilio letu?”
Angalia, mwenyeji wa bonde na mwamba wa nchi ya wazi! Mimi niko juu yako, - hii ndiyo ahadi ya Bwana- Mimi ni juu ya mtu yeyote anayesema, 'Ni nani atashuka kutupiga?' au 'Ni nani atakayeingia kwenye nyumba zetu?'
14 Nitawaadhibu kama istahilivyo matendo yenu, asema Bwana. Nitawasha moto katika misitu yenu ambao utateketeza kila kitu kinachowazunguka.’”
Nitawaadhibu kutokana na matunda ya matendo yako-hili ndilo tamko la Bwana- na nitawasha moto katika misitu, na utateketeza kila kitu.'”

< Yeremia 21 >