< Yeremia 2 >

1 Neno la Bwana lilinijia kusema,
Neno la BWANA lilinijia likisema,
2 “Nenda ukahubiri masikioni mwa watu wa Yerusalemu: “‘Nakumbuka moyo wako wa uchaji katika ujana wako, jinsi ulivyonipenda kama bibi arusi na kunifuata katika jangwa lile lote, katika nchi isiyopandwa mbegu.
“Nenda ukanene katika masikio ya Yerusalemu. Useme; BWANA asema hivi: Ninakumbuka agano la uaminifu la ujana wako, upendo wako wakati tulipokuwa tumechumbiana, ulipokuwa ukinihitaji kule jangwani, katika ile nchi iliyokuwa haijapandwa.
3 Israeli alikuwa mtakatifu kwa Bwana, kama malimbuko ya kwanza ya mavuno yake; wote waliowaangamiza walihesabiwa kuwa na hatia, nayo maafa yaliwakumba,’” asema Bwana.
Israeli alikuwa ametengwa kwa BWANA, malimbuko yake ya mavuno yake! Wote waliokula malimbuko yake walikuwa na hatia! majanga yaliwajia—asema BWANA.'”
4 Sikia neno la Bwana, ee nyumba ya Yakobo, nanyi nyote jamaa za nyumba ya Israeli.
Sikilizeni neno la BWANA, enyi nyumba ya Yakobo na kila familia katika nyumba ya Israeli.
5 Hivi ndivyo asemavyo Bwana: “Je, baba zenu waliona kosa gani kwangu, hata wakatangatanga mbali nami hivyo? Walifuata sanamu zisizofaa, nao wenyewe wakawa hawafai.
BWANA anasema hivi, “Ni makosa gani ambayo baba zenu waliyaona kwangu, hata wakatae kunifuata mimi? hata wazifuate sanamu ambazo hazina chochote na wao kuwa si kitu?
6 Hawakuuliza, ‘Yuko wapi Bwana, aliyetupandisha kutoka Misri na kutuongoza kupitia nyika kame, kupitia nchi ya majangwa na mabonde, nchi ya ukame na giza, nchi ambayo hakuna mtu asafiriye ndani yake wala hakuna mtu aishiye humo?’
Wala hawakusema, BWANA yuko wapi, ambaye alitutoa katika nchi ya Misri? BWANA yuko wapi, ambaye alituongoza katika jangwa, katika nchi ya Araba na mashimo, katika nchi ya ukame na giza nene, katika nchi ambayo hakuna mtu apitaye wala hakuna mtu anayeishi humo?
7 Niliwaleta katika nchi yenye wingi wa vitu ili mpate kula matunda yake na utajiri wa mazao yake. Lakini mkaja na kuinajisi nchi yangu, na kuufanya urithi wangu chukizo.
Lakini nilwaleta katika nchi ya Kameli, ili mle matunda yake na vitu vingine vyema! Lakini mlipokuja, mliitia unajisi nchi yangu, mliufany urithi wangu kuwa chukizo!
8 Makuhani hawakuuliza, ‘Yuko wapi Bwana?’ Wale wanaoshughulikia sheria hawakunijua mimi; viongozi waliasi dhidi yangu. Manabii walitabiri kwa jina la Baali, wakifuata sanamu zisizofaa.
Hata makuhani hawakusema, 'BWANA yuko wapi?' na watalamu wa sheria hawakunijali mimi! wachungaji wametenda dhambi dhidi yangu. Manabii wamemtolea Baali unabii na kuvitafuta vitu ambvyo havina faida.
9 “Kwa hiyo naleta tena mashtaka dhidi yako,” asema Bwana. “Nami nitaleta mashtaka dhidi ya watoto wa watoto wako.
Kwa hiyo nitaendelea kuwashitaki - hili ni neno la BWANA - na nitawashitiki watoto wa watoto wenu.
10 Vuka, nenda ngʼambo mpaka pwani ya Kitimu nawe uangalie, tuma watu waende Kedari, wachunguze kwa makini, uone kama kumekuwepo kitu kama hiki.
Kwa kuvuka kwenda hadi pwani ya Kitimu na kutazama. Tuma wajumbe kwenda Kedari na tafuta uone kama kama iliwahi kutokea hapo awali vitu kama hivi.
11 Je, taifa limebadili miungu yake wakati wowote? (Hata ingawa hao si miungu kamwe.) Lakini watu wangu wamebadili Utukufu wao kwa sanamu zisizofaa kitu.
Je, taifa limebadilisha miungu, hata kama haikuwa miungu? Lakini watu wangu wameubadili utukufu wao kwa kitu ambacho hakiwezi kuwasaidia.
12 Shangaeni katika hili, ee mbingu, nanyi tetemekeni kwa hofu kuu,” asema Bwana.
Sitajabuni, enyi mbingu kwa sababu ya hili! Tetemekeni na kuogopa -asema BWANA.
13 “Watu wangu wametenda dhambi mbili: Wameniacha mimi, niliye chemchemi ya maji yaliyo hai, nao wamejichimbia visima vyao wenyewe, visima vilivyobomoka, visivyoweza kuhifadhi maji.
Kwa kuwa watu wangu wametenda maovu mawili dhidi yangu: Wameziacha chemichemi za maji ya uhai kwa kuchimba mabarika kwa ajili yao, mabarika yanayovuja yasiyoweza kutunza maji!
14 Je, Israeli ni mtumishi, yaani mtumwa kwa kuzaliwa? Kwa nini basi amekuwa mateka?
Je, Israeli ni mtumwa? Kwani hakuzaliwa nyumbani? Kwa nini sasa amekuwa nyara?
15 Simba wamenguruma; wamemngurumia. Wameifanya nchi yake kuwa ukiwa; miji yake imeteketezwa, nayo imeachwa haina watu.
Wanasimba wameunguruma dhidi yake. Wamepiga kelele sana na kuifanya kuwa ukiwa. Miji yake imeharibiwa na kubaki bila watu.
16 Pia watu wa Memfisi na Tahpanhesi wamevunja taji ya kichwa chako.
Pia watu wa Nufu na Tahapanesi watakinyoa kichwa chako.
17 Je, hukujiletea hili wewe mwenyewe kwa kumwacha Bwana, Mungu wako alipowaongoza njiani?
Je, hamkufanya haya kwa ajili yenu mlipomwacha BWANA, wakati Mungu wenu, alipokuwa akiwaongoza njiani?
18 Sasa kwa nini uende Misri kunywa maji ya Shihori? Nawe kwa nini kwenda Ashuru kunywa maji ya Mto Frati?
Kwa hiyo, kwa nini kutafuta msaada Misri na kunywa maji ya Shihori? Kwa nini kutafuta msaada Ashuru na kunywa maji ya Mto Frati?
19 Uovu wako utakuadhibu; kurudi nyuma kwako kutakukemea. Basi kumbuka, utambue jinsi lilivyo ovu na chungu kwako unapomwacha Bwana Mungu wako na kutokuwa na hofu yangu,” asema Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote.
Uovu wako unakukemea, na maasi yako yatakuadhibu. Kwa hiyo yafikiri hayo; tambua kuwa ni uovu na uchungu kwenu ninyi kuniacha mimi, BWANA Mungu wako, na kutokuwa na hofu yangu - asema BWANA wa majeshi.
20 “Zamani nilivunja nira yako na kukatilia mbali vifungo vyako; ukasema, ‘Sitakutumikia!’ Naam kweli, kwenye kila kilima kirefu na chini ya kila mti uliotanda matawi yake ulijilaza kama kahaba.
Kwa kuwa niliivunja nira yenu mliyokuwa nayo wakati wa kale; Nilivichana vifungo vyako kutoka kwako. Lakini bado ulisema, 'Sitamtumikia!' tangu ulipopiga magoti katika kila kilima kuusogelea kila mti wenye majani mabichhi, enyi makahaba.
21 Nilikupanda ukiwa mzabibu ulio bora sana, mkamilifu na wa mbegu nzuri. Ilikuwaje basi ukawa kinyume nami, ukaharibika na kuwa mzabibu mwitu?
Lakini mimi mwenyewe niliwapanda kama mzabibu niliouchagua, mbegu iliyokamilika. Lakini tazama jinsi ulivyobadilika mbele yangu, na kuwa mzabibu usiofaa na mzabibu pori!
22 Hata ujisafishe kwa magadi na kutumia sabuni nyingi, bado doa la hatia yako liko mbele zangu,” asema Bwana Mwenyezi.
Kwa kuwa hata kama utajisafisha mwenyewe mtoni na kuoga kwa sabuni kali, bado dhambi yako ni madoa mbele yangu - asema BWANA Mungu.
23 “Wawezaje kusema, ‘Mimi si najisi, sijawafuata Mabaali’? Kumbuka jinsi ulivyotenda kule bondeni; fikiri uliyoyafanya. Wewe ni ngamia jike mwenye mbio ukikimbia hapa na pale,
Wawezaje kusema, 'Mimi sijanajisika! Mimi sjaenda kwa Mabaal?' Tazama tabia zako zilivyokuwa bondeni! Tambua kile ulichofanya, wewe ngamia mwepesi! akimbiaye katika njia yake!
24 punda-mwitu aliyezoea jangwa, anayenusa upepo katika tamaa yake kubwa: katika wakati wake wa kuhitaji mbegu ni nani awezaye kumzuia? Madume yoyote yanayomfuatilia hayana haja ya kujichosha; wakati wa kupandwa kwake watampata tu.
Wewe ni punda wa mwitu, aliyeizoelea nyika, avutaye pumzi za upepo usiofaa katika tamaa ya kuishi! Ni nani awezaye kumgeuza anapotafuta dume la kumpanda? Na punda dume amtafutaye hajichoshi mwenyewe. Huenda kwake wakati wa mwezi wa kupandwa.
25 Usikimbie hadi miguu yako iwe haina viatu, na koo lako liwe limekauka. Lakini ulisema, ‘Haina maana! Ninaipenda miungu ya kigeni, nami lazima niifuatie.’
Lazima uizuie miguu yako isikose kiatu na koo lako kuwa na kiu! Lakini umesema, 'Hakuna matumaini! Hapana! Nawapenda wageni nami huwatafuta!'
26 “Kama vile mwizi aaibikavyo wakati amekamatwa, hivyo ndivyo nyumba ya Israeli inavyoaibishwa: wao wenyewe, wafalme wao na maafisa wao, makuhani wao na manabii wao.
Kama aibu ya mwizi ilivyo anapokuwa amekamatwa, ndivyo aibu ya Israeli itakavyokuwa - wao, wafalme wao, malikia wao, makuhani na manabii wao!
27 Wanaiambia miti, ‘Wewe ndiwe baba yangu,’ nalo jiwe, ‘Wewe ndiwe uliyenizaa.’ Wamenipa visogo vyao wala hawakunigeuzia nyuso zao; lakini wakiwa katika taabu, wanasema, ‘Njoo utuokoe!’
Hawa ndio wale waiambiayo miti, 'Ninyi ndio baba zangu,' na mawe, 'Ninyi ndio mlinizaa.' Kwa kuwa migongo yao hunitazama na siyo nyuso zao. Hata hivyo, wakati wa shida husema, 'Amka utuokoe!'
28 Iko wapi basi ile miungu mliyojitengenezea? Yenyewe na ije kama inaweza kuwaokoa wakati mko katika taabu! Kwa maana mna miungu mingi kama mlivyo na miji, ee Yuda.
Lakini iko wapi ile miungu mliyojitengenezea? Acha hao wainuke kama wanaweza kuwaokoa wakati wa shida, kwa kuwa hizo sanamu zenu zina idadi sawa na miji yenu, katika Yuda.
29 “Kwa nini mnaleta mashtaka dhidi yangu? Ninyi nyote mmeniasi,” asema Bwana.
Kwa hiyo kwa nini kunituhumu kwa kufanya makosa? Ninyi nyote mmeniasi - asema BWANA wa majeshi.
30 “Nimeadhibu watu wako bure tu, hawakujirekebisha. Upanga wako umewala manabii wako kama simba mwenye njaa.
Nimewadhibu watu wenu bure. Wala hawakutaka kurudiwa. Upanga wako umewaangamiza manabii wenu kama kama simba aangamizaye!
31 “Enyi wa kizazi hiki, tafakarini neno la Bwana: “Je, nimekuwa jangwa kwa Israeli au nchi ya giza kuu? Kwa nini watu wangu wanasema, ‘Sisi tuko huru kuzurura, hatutarudi kwako tena’?
Enyi watu wa kizazi hiki! Sikilizeni neno langu, neno la BWANA! Je, nimekuwa jangwa kwa Israeli? Au nchi yenye giza nene? Kwa nini watu wangu husema, 'Acha tuzungukezunguke, hatutakuja kwako tena'?
32 Je, mwanamwali husahau vito vyake, au bibi arusi mapambo yake ya arusi? Lakini watu wangu wamenisahau mimi, tena kwa siku zisizo na hesabu.
Je, mwanamwali anaweza kusahau mapambo yake, na bibi arusi mavazi yake? Lakini watu wngu wamenisahau mimi kwa siku nyingi!
33 Je, wewe una ustadi kiasi gani katika kufuatia mapenzi! Hata wale wanawake wabaya kuliko wote wanaweza kujifunza kutokana na njia zako.
Jinsi mlivyotengeneza njia zenu vizuri ili kutafuta mapenzi. Hata mmewafundisha njia zenu wanawake waovu.
34 Katika nguo zako watu huona damu ya uhai ya maskini wasio na hatia, ingawa hukuwakamata wakivunja nyumba. Lakini katika haya yote
Damu ambayo ilikuwa ndio uhai wa watu wasio na hatia, imeonekana katika mavazi yenu. Hawa watu hawajawahi kuonekana katika matendo maovu.
35 unasema, ‘Sina hatia; Mungu hajanikasirikia.’ Lakini nitakuhukumu kwa sababu unasema, ‘Mimi sijatenda dhambi.’
Pamoja na mambo haya yote, wewe unaeendelea kusema kuwa hauna hatia. Kwa hakika hasira ya BWANA itageuka kutoka kwangu. 'Lakini tazama! Utahukumiwa kwa sababu, 'Sikutenda dhambi.'
36 Kwa nini unatangatanga sana, kubadili njia zako? Utakatishwa tamaa na Misri kama ulivyokatishwa na Ashuru.
Kwa nini mnatangatanga kwa urahisi katika njia zenu? Pia Misri itawahuzunisha sana, kama ilivyokuwa kwa Ashuru.
37 Pia utaondoka mahali hapo ukiwa umeweka mikono kichwani, kwa kuwa Bwana amewakataa wale unaowatumainia; hutasaidiwa nao.
Mtaondoka hapo mkiwa mmehuzunika sana, mkiwa mmeweka mikono vichwani mwenu, kwa kuwa BWANA amemkutaa yule mliyemtumainia, kwa hiyo hamtapata msaada toka kwao,”

< Yeremia 2 >