< Yeremia 16 >

1 Kisha neno la Bwana likanijia:
Ndipo neno la Bwana likanijia, kusema,
2 “Kamwe usioe na kuwa na wana wala binti mahali hapa.”
“Usiwe na mke, wala usiwe na wana au binti hapa.
3 Kwa maana hili ndilo asemalo Bwana kuhusu wana na binti wazaliwao katika nchi hii, na kuhusu wale wanawake ambao ni mama zao, na wale wanaume ambao ni baba zao:
Kwa kuwa Bwana asema hivi kwa wana na binti ambao wamezaliwa hapa, kwa mama waliowabeba, na kwa baba waliowafanya wazaliwe katika nchi hii,
4 “Watakufa kwa magonjwa ya kufisha. Hawataombolezewa wala kuzikwa, lakini watakuwa kama mavi yaliyosambaa juu ya ardhi. Watakufa kwa upanga na kwa njaa, nazo maiti zao zitakuwa chakula cha ndege wa angani, na cha wanyama wa nchi.”
'Watakufa vifo vya magonjwa. Hawataliliwa wala kuzikwa. Watakuwa kama samadi juu ya nchi. Kwa maana wataangamizwa kwa upanga na njaa, na miili yao itakuwa chakula cha ndege wa angani na wanyama wa dunia.'
5 Kwa kuwa hili ndilo asemalo Bwana: “Usiingie katika nyumba ambayo kuna chakula cha matanga, usiende kuwaombolezea wala kuwahurumia, kwa sababu nimeziondoa baraka zangu, upendo wangu na huruma zangu kutoka kwa watu hawa,” asema Bwana.
Maana Bwana asema hivi, 'Usiingie nyumba yoyote yenye kuomboleza. Usiende kuwaombolezea, wala usihuzunike kwa ajili ya watu hawa. Kwa maana nimeondoa amani yangu, uaminifu wa agano, na huruma, kutoka kwa watu hawa! Ndivyo asemavyo Bwana;
6 “Wakubwa na wadogo watakufa katika nchi hii. Hawatazikwa wala kuombolezewa, na hakuna atakayejikatakata au kunyoa nywele za kichwa chake kwa ajili yao.
kwa hiyo wakuu na wadogo watakufa katika nchi hii. Wala hawatazikwa, wala hakuna yeyote atakayeomboleza kwa ajili yao. Hakuna mtu atakayejikata-kata au kunyoa vichwa vyao kwa ajili yao.
7 Hakuna yeyote atakayewapa chakula ili kuwafariji wale waombolezao kwa ajili ya wale waliokufa, hata akiwa amefiwa na baba au mama, wala hakuna yeyote atakayewapa kinywaji ili kuwafariji.
Hakuna mtu anayepaswa kugawa chakula chochote wakati wa kuomboleza ili kuwafariji kwa sababu ya vifo, na hawatawapa kikombe cha faraja kwa baba yake au mama yake ili kuwafariji.
8 “Usiingie katika nyumba ambayo kuna karamu, na kuketi humo ili kula na kunywa.
Usiende kwenye nyumba ya karamu ili ukae pamoja nao ili kula au kunywa.
9 Kwa kuwa hili ndilo asemalo Bwana Mwenye Nguvu Zote, aliye Mungu wa Israeli: ‘Mbele ya macho yako na katika siku zako, nitakomesha sauti zote za shangwe na za furaha, na pia sauti za bibi arusi na bwana arusi mahali hapa.’
Kwa maana Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, 'Tazama, mbele yako, siku zako na mahali hapa, nitakomesha sauti ya furaha na sherehe, sauti ya bwana na bibi arusi. '
10 “Utakapowaambia watu hawa mambo haya yote na wakakuuliza, ‘Kwa nini Bwana ameamuru maafa makubwa kama haya dhidi yetu? Tumefanya kosa gani? Tumetenda dhambi gani dhidi ya Bwana, Mungu wetu?’
Kisha itatokea kwamba utawaambia watu hawa maneno haya yote, na watakuambia, 'Mbona Bwana amesema maafa yote haya juu yetu? Uovu wetu ni uovu gani na dhambi yetu tuliyomtendea Bwana, Mungu wetu?'
11 Basi waambie, ‘Ni kwa sababu baba zenu waliniacha mimi, wakafuata miungu mingine ili kuitumikia na kuiabudu. Waliniacha mimi na hawakuishika sheria yangu,’ asema Bwana.
Basi uwaambie, 'hii ndiyo ahadi ya Bwana; Kwa sababu baba zenu waliniacha, nao wakafuata miungu mingine, wakaiabudu na kuisujudia. Waliniacha na hawakuishika sheria yangu.
12 ‘Lakini ninyi mmetenda uovu zaidi kuliko baba zenu. Tazama jinsi ambavyo kila mmoja wenu anafuata ukaidi wa moyo wake mbaya, badala ya kunitii mimi.
Lakini ninyi wenyewe mmeleta uovu zaidi kuliko baba zenu, kwa maana, kila mtu anaenda kwa ukaidi wa moyo wake mbaya; hakuna mtu anayenisikiliza.
13 Kwa hiyo nitawaondoa katika nchi hii na kuwatupa katika nchi ambayo ninyi wala baba zenu hamkuijua, nako huko mtaitumikia miungu mingine usiku na mchana, kwa maana sitawapa fadhili zangu huko.’
Kwa hiyo nitawafukuza kutoka nchi hii mpaka nchi msiyoijua, wewe wala baba zako, nanyi mtaiabudu miungu mingine huko mchana na usiku, kwa maana mimi sitawapa fadhili zangu.'
14 “Hata hivyo, siku zinakuja,” asema Bwana, “wakati ambapo watu hawatasema tena, ‘Hakika kama Bwana aishivyo, aliyewapandisha Waisraeli kutoka Misri,’
Kwa hiyo tazama! Siku zinakuja-hili ndilo tamko la Bwana-ambapo hawatasema tena, 'Kama Bwana aishivyo, yeye aliyewaleta wana wa Israeli kutoka nchi ya Misri.'
15 bali watasema, ‘Hakika kama Bwana aishivyo, aliyewatoa wana wa Israeli kutoka nchi ya kaskazini na nchi zote alizokuwa amewafukuzia.’ Maana nitawarudisha katika nchi niliyowapa baba zao.
Kwa maana, kama Bwana aishivyo, yeye aliyewaleta wana wa Israeli kutoka nchi ya kaskazini, na kutoka nchi aliyowaangamiza, nitawarudisha katika nchi niliyowapa baba zao.
16 “Lakini sasa nitawaagiza wavuvi wengi,” asema Bwana, “nao watawavua. Baada ya hilo, nitawaagizia wawindaji wengi, nao watawawinda kwenye kila mlima na kilima, na katika nyufa za miamba.
Angalia! hili ni tamko la Bwana-Nitatuma wavuvi wengi-kwa hiyo watawavua watu. Baada ya hayo nitatuma wawindaji wengi ili waweze kuwinda kati ya milima na vilima vyote, na katika miamba ya mwamba.
17 Macho yangu yanaziona njia zao zote, hazikufichika kwangu, wala dhambi yao haikusitirika.
Kwa kuwa macho yangu yapo juu ya njia zao zote; hawawezi kujificha mbele yangu. Uovu wao hauwezi kufichika mbele ya macho yangu.
18 Nitawalipiza maradufu kwa ajili ya uovu wao na dhambi yao, kwa sababu wameinajisi nchi yangu kwa maumbo yasiyo na uhai ya vinyago vyao vibaya, na kuujaza urithi wangu na sanamu za kuchukiza.”
Nami kwanza nitawalipa mara mbili uovu na dhambi zao kwa kuwa wameichafua nchi yangu sanamu za machukizo, na kwa kujaza urithi wangu na sanamu zao za machukizo.
19 Ee Bwana, nguvu zangu na ngome yangu, kimbilio langu wakati wa taabu, kwako mataifa yatakujia kutoka miisho ya dunia na kusema, “Baba zetu hawakuwa na chochote zaidi ya miungu ya uongo, sanamu zisizofaa kitu ambazo hazikuwafaidia lolote.
Ee Bwana, wewe ndiwe ngome yangu, na kimbilio langu, na mahali pa usalama wangu siku ya shida. Mataifa yatakujia kwako kutoka mwisho wa dunia na kusema, 'Hakika baba zetu walirithi udanganyifu. Ubatili mtupu; hakuna faida ndani yao. Je!
20 Je, watu hujitengenezea miungu yao wenyewe? Naam, lakini hao si miungu!”
Watu hufanya miungu kwa ajili yao wenyewe? Lakini wao sio miungu.
21 “Kwa hiyo nitawafundisha: wakati huu nitawafundisha nguvu zangu na uwezo wangu. Ndipo watakapojua kuwa Jina langu ndimi Bwana.
Kwa hiyo tazama! Nitawafanya wajue wakati huu, nitawafanya watambue mkono wangu na nguvu zangu, kwa hiyo watajua kwamba Yahweh ni jina langu.”

< Yeremia 16 >