< Yeremia 14 >

1 Hili ndilo neno la Bwana kwa Yeremia kuhusu ukame:
Neno la Bwana lilimjia Yeremia kuhusu ukame,
2 “Yuda anaomboleza, miji yake inayodhoofika; wanaomboleza kwa ajili ya nchi, nacho kilio kinapanda kutoka Yerusalemu.
“Wayahudi waomboleze; basi milango yake ianguke. Wao wanaomboleza kwa ajili ya ardhi; Kilio chao kwa Yerusalemu kimepaa juu.
3 Wakuu wanawatuma watumishi wao maji; wanakwenda visimani lakini humo hakuna maji. Wanarudi na vyombo bila maji; wakiwa na hofu na kukata tamaa, wanafunika vichwa vyao.
Wenye nguvu huwatuma watumishi wao kwa ajili ya maji. Wanapoingia kwenye visima, hawawezi kupata maji. Wote wanarudi hawajafanikiwa; Wao hufunika vichwa vyao na aibu.
4 Ardhi imepasuka nyufa kwa sababu hakuna mvua katika nchi; wakulima wana hofu na wanafunika vichwa vyao.
Kwa sababu hii ardhi imepasuka, kwa maana hakuna mvua katika nchi. Wakulima huwa na aibu na kufunika vichwa vyao.
5 Hata kulungu mashambani anamwacha mtoto wake aliyezaliwa wakati huo huo kwa sababu hakuna majani.
Kwa maana hata kunguru huwaacha wanawe katika mashamba, kwa maana hakuna nyasi.
6 Punda-mwitu wanasimama juu ya miinuko iliyo kame na kutweta kama mbweha; macho yao yanakosa nguvu za kuona kwa ajili ya kukosa malisho.”
Punda mwitu husimama kwenye mabonde yaliyo wazi na hupiga upepo kama mbweha. Macho yao yanashindwa kufanya kazi, kwa maana hakuna mimea.
7 Ingawa dhambi zetu zinashuhudia juu yetu, Ee Bwana, tenda jambo kwa ajili ya jina lako. Kwa kuwa kukengeuka kwetu ni kukubwa, nasi tumetenda dhambi dhidi yako.
Hata ingawa maovu yetu yanatushuhudia, Bwana, tenda kwa ajili ya jina lako. Kwa sababu matendo yetu yasiyo na imani yamezidi; tumekutenda dhambi.
8 Ee Tumaini la Israeli, Mwokozi wake wakati wa taabu, kwa nini unakuwa kama mgeni katika nchi, kama msafiri anayekaa kwa usiku mmoja tu?
Matumaini ya Israeli, yule anayemwokoa wakati wa dhiki, kwa nini utakuwa kama mgeni katika nchi, kama mtu akaaye nchi ya kigeni ambaye hujinyoosha na kutumia hutumia usiku mmoja tu?
9 Mbona unakuwa kama mtu aliyeshtukizwa, kama shujaa asiye na uwezo wa kuokoa? Wewe uko katikati yetu, Ee Bwana, nasi tunaitwa kwa jina lako; usituache!
Kwa nini utakuwa kama mtu aliyechanganyikiwa, kama shujaa ambaye hawezi kuokoa mtu yeyote? Kwa maana wewe u katikati yetu, Bwana! Jina lako limetangazwa juu yetu. Usiondoke
10 Hili ndilo Bwana asemalo kuhusu watu hawa: “Wanapenda sana kutangatanga, hawaizuii miguu yao. Hivyo Bwana hawakubali; sasa ataukumbuka uovu wao na kuwaadhibu kwa ajili ya dhambi zao.”
Bwana awaambia hivi watu hawa “Kwa kuwa wanapenda kutanga tanga, hawakuzuia miguu yao kufanya hivyo.” Bwana hafurahi nao. Sasa anawakumbusha uovu wao na ameadhibu dhambi zao.
11 Kisha Bwana akaniambia, “Usiombe kwa ajili ya mafanikio ya watu hawa.
Bwana akaniambia, Usiombe kwa ajili ya watu hawa.
12 Ingawa wanafunga, sitasikiliza kilio chao; hata wakitoa dhabihu za kuteketezwa na dhabihu za nafaka, sitazikubali. Badala yake, nitawaangamiza kwa upanga, njaa na tauni.”
Maana ikiwa wanafunga, sitasikiliza kulia kwao; na wanapotoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za unga, sitawafurahia. Kwa maana nitawaangamiza kwa upanga, njaa, na tauni.
13 Lakini nikasema, “Aa, Bwana Mwenyezi, manabii wanaendelea kuwaambia, ‘Hamtaona upanga wala kukabiliwa na njaa. Naam, nitawapa amani ya kudumu mahali hapa.’”
Ndipo nikasema, “Ee Bwana, Bwana! Angalia! mabii wanawaambia watu, 'Huwezi kuona upanga; hakutakuwa na njaa kwako, kwa kuwa nitakupa usalama wa kweli mahali hapa.'”
14 Ndipo Bwana akaniambia, “Manabii wanatabiri uongo kwa jina langu. Sikuwatuma, wala sikuwaweka, wala sikusema nao. Wanawatabiria maono ya uongo, maaguzi, maono ya sanamu zisizofaa kitu, na madanganyo ya mawazo yao wenyewe.
Bwana akaniambia, 'manabii wanatabiri uongo kwa jina langu. Sikuwafukuza, wala sikuwapa amri au kusema nao. Lakini maono ya udanganyifu na ya maana, uchawi wa udanganyifu unaotokana na akili zao ndicho wanachowahubiria.”
15 Kwa hiyo, hili ndilo Bwana asemalo kuhusu manabii wanaotabiri kwa jina langu: Mimi sikuwatuma, lakini wanasema, ‘Hakuna upanga wala njaa itakayoigusa nchi hii.’ Manabii hao hao watakufa kwa upanga na njaa.
Kwa hiyo Bwana asema hivi, “Kwa habari ya manabii wakihubiri kwa jina langu, ambao mimi siwakutuma; wale wanaosema kuwa hakutakuwa na upanga wala njaa katika nchi hii mabii hawa wataangamia kwa upanga na njaa.
16 Nao watu hao wanaowatabiria watatupwa nje katika barabara za Yerusalemu kwa sababu ya njaa na upanga. Hapatakuwepo yeyote wa kuwazika wao au wake zao, wana wao au binti zao. Nitawamwagia maafa wanayostahili.
Na watu waliopewa utabiri watafukuzwa nje ya barabara za Yerusalemu kwa sababu ya njaa na upanga; kwa kuwa hakuna mtu wa kuwazikas-wao, na wake zao, na wana wao, wala binti zao; kwa maana nitamwaga uovu wao wenyewe juu yao.
17 “Nena nao neno hili: “‘Macho yangu na yatiririkwe na machozi usiku na mchana bila kukoma; kwa kuwa binti yangu aliye bikira, yaani watu wangu, amepata jeraha baya, pigo la kuangamiza.
Sema neno hili kwao 'Acha macho yangu yatokwe machozi, usiku na mchana. wala yasikome, kwa kuwa kutakuwa na kuanguka kwa bikira, binti ya watu wangu - jeraha kubwa lisilotibika.
18 Kama nikienda mashambani, ninaona wale waliouawa kwa upanga; kama nikienda mjini, ninaona maangamizi ya njaa. Nabii na kuhani kwa pamoja wamekwenda katika nchi wasiyoijua.’”
Ikiwa nitatoka kwenye shamba basi angalia! kuna wale waliouawa kwa upanga. Na kama nitakuja mjini, basi, tazama! kuna wale walio na ugonjwa wa njaa. Hata nabii na kuhani wote wanatembea juu ya nchi bila maarifa.'”
19 Je, umemkataa Yuda kabisa? Umemchukia Sayuni kabisa? Kwa nini umetuumiza hata hatuwezi kuponyeka? Tulitarajia amani, lakini hakuna jema lililotujia; tulitarajia wakati wa kupona lakini kuna hofu kuu tu.
Je! Umemkataa kabisa Yuda? Je, unaichukia Sayuni? Kwa nini umetupiga wakati hakuna uponyaji kwetu? Tulitumaini amani, lakini hapakuwa na kitu kizuri-na kwa wakati wa uponyaji, lakini tazama, kuna hofu tu.
20 Ee Bwana, tunatambua uovu wetu na kosa la baba zetu; kweli tumetenda dhambi dhidi yako.
Tunakubali, Bwana, makosa yetu, uovu wa babu zetu, kwa kuwa tumekukosea.
21 Kwa ajili ya jina lako usituchukie kabisa; usikidharau kiti chako cha enzi kilichotukuka. Kumbuka agano lako nasi na usilivunje.
Usitukatae! Kwa ajili ya jina lako, usikifedheheshe kiti chako cha enzi cha utukufu. Kumbuka na usivunje agano lako na sisi.
22 Je, kuna sanamu yoyote isiyofaa kitu ya mataifa iwezayo kuleta mvua? Je, anga peke yake zaweza kutoa mvua? La hasha, ni wewe peke yako, Ee Bwana, Mungu wetu. Kwa hiyo tumaini letu liko kwako, kwa kuwa wewe ndiwe ufanyaye haya yote.
Je, kuna miongoni mwa sanamu za mataifa yeyote zinazoweza kuifanya mbingu kutoa mvua? Je, si wewe, Bwana Mungu wetu, ambaye hufanya jambo hili? Tunatumaini kwako, kwa kuwa umefanya mambo haya yote.

< Yeremia 14 >