< Yeremia 10 >

1 Sikieni lile ambalo Bwana, anena nanyi ee nyumba ya Israeli.
Ecoutez la parole que Yahweh vous adresse, maison d’Israël:
2 Hili ndilo asemalo Bwana: “Usijifunze njia za mataifa wala usitishwe na ishara katika anga, ingawa mataifa yanatishwa nazo.
Ainsi parle Yahweh: N’apprenez pas la voie des nations, et ne soyez pas effrayés par les signes du ciel, comme les nations s’en effraient;
3 Kwa maana desturi za mataifa hazina maana, wanakata mti msituni, na fundi anauchonga kwa patasi.
Car les coutumes des nations ne sont que vanité; c’est du bois qu’on coupe dans la forêt, un ouvrage de la main du sculpteur, façonné avec le ciseau,
4 Wanaparemba kwa fedha na dhahabu, wanakikaza kwa nyundo na misumari ili kisitikisike.
que l’on décore avec l’argent et l’or. On le fixe avec des clous à coups de marteau, pour qu’il ne bouge pas.
5 Sanamu zao ni kama sanamu iliyowekwa shambani la matango kutishia ndege nazo haziwezi kuongea; sharti zibebwe sababu haziwezi kutembea. Usiziogope; haziwezi kudhuru, wala kutenda lolote jema.”
Ces dieux-là sont comme une colonne faite au tour; car on les porte, ils ne marchent pas. Ne les craignez point: ils ne font pas de mal; ils ne peuvent pas davantage faire du bien.
6 Hakuna aliye kama wewe, Ee Bwana; wewe ni mkuu, jina lako ni lenye nguvu katika uweza.
Nul n’est semblable à vous, Yahweh; vous êtes grand, et votre nom est grand en puissance.
7 Ni nani ambaye haimpasi kukuheshimu wewe, Ee Mfalme wa mataifa? Hii ni stahili yako. Miongoni mwa watu wote wenye hekima katika mataifa na katika falme zao zote, hakuna aliye kama wewe.
Qui ne vous craindrait, Roi des nations! c’est à vous que la crainte est due. Car, parmi tous les sages des nations et dans tous leurs royaumes, nul n’est pareil à vous.
8 Wote hawana akili, tena ni wapumbavu, wanafundishwa na sanamu za miti zisizofaa lolote.
Tous ensemble ils sont stupides et fous; enseignement de vanité; c’est du bois!
9 Huleta fedha iliyofuliwa kutoka Tarshishi na dhahabu kutoka Ufazi. Kile ambacho fundi na sonara wametengeneza huvikwa mavazi ya rangi ya samawi na urujuani: vyote vikiwa vimetengenezwa na mafundi stadi.
Argent battu amené de Tharsis, et or d’Ophaz; œuvre de sculpture et de main d’orfèvre! On les revêt de pourpre violette et rouge; tous ne sont qu’ouvrage d’artistes.
10 Lakini Bwana ni Mungu wa kweli, yeye ndiye Mungu aliye hai, Mfalme wa milele. Anapokasirika, dunia hutetemeka, mataifa hayawezi kustahimili hasira yake.
Mais Yahweh est Dieu en vérité; lui, il est un Dieu vivant et un Roi éternel; à sa colère la terre tremble, et les nations ne soutiennent pas son courroux.
11 “Waambie hivi: ‘Miungu hii, ambayo haikuumba mbingu na dunia, itaangamia kutoka dunia na kutoka chini ya mbingu.’”
Voici comment vous leur parlerez: « Les dieux qui n’ont pas fait le ciel et la terre seront exterminés de la terre et de dessous le ciel. »
12 Lakini Mungu aliiumba dunia kwa uweza wake, akaweka misingi ya ulimwengu kwa hekima yake, na akazitandaza mbingu kwa ufahamu wake.
Il a fait la terre par sa force, affermi le monde par sa sagesse, et par son intelligence il a étendu les cieux.
13 Atoapo sauti yake, maji yaliyo katika mbingu hunguruma; huyafanya mawingu yainuke kutoka miisho ya dunia. Hupeleka umeme wa radi pamoja na mvua, naye huuleta upepo kutoka ghala zake.
A sa voix, les eaux s’amassent dans les cieux; il fait monter les nuages des extrémités de la terre; il fait briller les éclairs d’où jaillit l’averse, et fait sortir le vent de ses réservoirs.
14 Kila mmoja ni mjinga na hana maarifa, kila sonara ameaibishwa na sanamu zake. Vinyago vyake ni vya udanganyifu, havina pumzi ndani yavyo.
Tout homme est stupide, hors de sens; tout artisan a honte de son idole, car son image fondue n’est que mensonge; il n’y a pas de souffle en elle.
15 Havifai kitu, ni vitu vya kufanyia mzaha tu, hukumu yavyo itakapowadia, vitaangamia.
Elle est une vanité, une œuvre de tromperie; au jour de leur châtiment, elle périra.
16 Yeye aliye Fungu la Yakobo sivyo alivyo, kwani ndiye Muumba wa vitu vyote, pamoja na Israeli, kabila la urithi wake: Bwana Mwenye Nguvu Zote ndilo jina lake.
Telle n’est pas la part de Jacob; car Lui, il a formé l’univers, et Israël est la tribu de son héritage; son nom est Yahweh des armées.
17 Kusanyeni mali na vitu vyenu mwondoke nchi hii, enyi mnaoishi katika hali ya kuzingirwa na jeshi.
Ramasse à terre ton bagage, toi qui es assiégée!
18 Kwa kuwa hili ndilo asemalo Bwana: “Wakati huu, nitawatupa nje kwa nguvu wote waishio katika nchi hii; nitawataabisha ili waweze kutekwa.”
Car ainsi parle Yahweh: Voici que cette fois, je vais lancer au loin les habitants du pays; je les serrerai de près, afin que l’ennemi les atteigne.
19 Ole wangu mimi kwa ajili ya kuumia kwangu! Jeraha langu ni kubwa! Lakini nilisema, “Kweli hii ni adhabu yangu, nami sharti niistahimili.”
Malheur à moi à cause de ma meurtrissure! Ma plaie est douloureuse; mais je le dis: « Oui, c’est là mon mal, et je le supporterai.
20 Hema langu limeangamizwa; kamba zake zote zimekatwa. Wana wangu wametekwa na hawapo tena; hakuna hata mmoja aliyebaki wa kusimamisha hema langu wala wa kusimamisha kibanda changu.
Ma tente est dévastée, tous mes cordages sont rompus; mes fils m’ont quittée, ils ne sont plus; je n’ai plus personne pour redresser ma tente, relever mes pavillons. »
21 Wachungaji hawana akili wala hawamuulizi Bwana, hivyo hawastawi na kundi lao lote la kondoo limetawanyika.
Ah! les pasteurs sont stupides; ils n’ont pas cherché Yahweh; aussi n’ont-ils pas prospéré, et tout leur troupeau a été dispersé.
22 Sikilizeni! Taarifa inakuja: ghasia kubwa kutoka nchi ya kaskazini! Hii itafanya miji ya Yuda ukiwa, makao ya mbweha.
Un bruit, une rumeur! Voici qu’elle vient, un grand tumulte arrive du pays du septentrion, pour faire des villes de Juda un désert, un repaire de chacals.
23 Ninajua, Ee Bwana, kwamba maisha ya mwanadamu si yake mwenyewe; hawezi kuziongoza hatua zake mwenyewe.
Je le sais, ô Yahweh, ce n’est pas à l’homme qu’appartient sa voie, ce n’est pas à l’homme qui marche de diriger ses pas.
24 Unirudi, Ee Bwana, lakini kwa kipimo cha haki: si katika hasira yako, usije ukaniangamiza.
Châtiez-moi, Yahweh, mais selon la justice, et non dans votre colère, pour me réduire à néant.
25 Umwage ghadhabu yako juu ya mataifa wasiokujua wewe, juu ya mataifa wasioliitia jina lako. Kwa kuwa wamemwangamiza Yakobo; wamemwangamiza kabisa na kuiharibu nchi yake.
Versez votre fureur sur les nations qui ne vous connaissent pas, sur les peuples qui n’invoquent pas votre nom; car ils ont dévoré Jacob, ils l’ont dévoré, ils l’achèvent, et ils dévastent sa demeure.

< Yeremia 10 >