< Isaya 66 >

1 Hili ndilo asemalo Bwana, “Mbingu ni kiti changu cha enzi, nayo dunia ni mahali pa kuweka miguu yangu. Iko wapi nyumba mtakayoijenga kwa ajili yangu? Mahali pangu pa kupumzikia patakuwa wapi?
כה אמר יהוה השמים כסאי והארץ הדם רגלי אי זה בית אשר תבנו לי ואי זה מקום מנוחתי
2 Je, mkono wangu haukufanya vitu hivi vyote, hivyo vikapata kuwepo?” asema Bwana. “Mtu huyu ndiye ninayemthamini: yeye ambaye ni mnyenyekevu na mwenye roho yenye toba, atetemekaye asikiapo neno langu.
ואת כל אלה ידי עשתה ויהיו כל אלה נאם יהוה ואל זה אביט--אל עני ונכה רוח וחרד על דברי
3 Lakini yeyote atoaye dhabihu ya fahali ni kama yeye auaye mtu, na yeyote atoaye sadaka ya mwana-kondoo, ni kama yule avunjaye shingo ya mbwa. Yeyote atoaye sadaka ya nafaka, ni kama yule aletaye damu ya nguruwe, na yeyote afukizaye uvumba wa kumbukumbu, ni kama yule aabuduye sanamu. Wamejichagulia njia zao wenyewe, nazo nafsi zao zinafurahia machukizo yao.
שוחט השור מכה איש זובח השה ערף כלב מעלה מנחה דם חזיר מזכיר לבנה מברך און--גם המה בחרו בדרכיהם ובשקוציהם נפשם חפצה
4 Hivyo, mimi pia nitawachagulia mapigo makali, nami nitaleta juu yao kile wanachokiogopa. Kwa maana nilipoita, hakuna yeyote aliyejibu, niliposema, hakuna yeyote aliyesikiliza. Walifanya maovu machoni pangu na kuchagua lile linalonichukiza.”
גם אני אבחר בתעלליהם ומגורתם אביא להם--יען קראתי ואין עונה דברתי ולא שמעו ויעשו הרע בעיני ובאשר לא חפצתי בחרו
5 Sikieni neno la Bwana, ninyi mtetemekao kwa neno lake: “Ndugu zenu wanaowachukia ninyi na kuwatenga ninyi kwa sababu ya Jina langu, wamesema, ‘Bwana na atukuzwe, ili tupate kuona furaha yenu!’ Hata sasa wataaibika.
שמעו דבר יהוה החרדים אל דברו אמרו אחיכם שנאיכם מנדיכם למען שמי יכבד יהוה--ונראה בשמחתכם והם יבשו
6 Sikieni hizo ghasia kutoka mjini, sikieni hizo kelele kutoka hekaluni! Ni sauti ya Bwana ikiwalipa adui zake yote wanayostahili.
קול שאון מעיר קול מהיכל קול יהוה משלם גמול לאיביו
7 “Kabla hajasikia utungu, alizaa; kabla hajapata maumivu, alizaa mtoto mwanaume.
בטרם תחיל ילדה בטרם יבוא חבל לה והמליטה זכר
8 Ni nani amepata kusikia jambo kama hili? Ni nani amepata kuona mambo kama haya? Je, nchi yaweza kuzaliwa kwa siku moja, au taifa laweza kutokea mara? Mara Sayuni alipoona utungu, alizaa watoto wake.
מי שמע כזאת מי ראה כאלה--היוחל ארץ ביום אחד אם יולד גוי פעם אחת כי חלה גם ילדה ציון את בניה
9 Je, nilete mwana hadi wakati wa kuzaliwa na nisizalishe?” asema Bwana. “Je, nifunge tumbo la uzazi wakati mimi ndiye nizalishaye?” asema Mungu wako.
האני אשביר ולא אוליד יאמר יהוה אם אני המוליד ועצרתי אמר אלהיך
10 “Shangilieni pamoja na Yerusalemu na mfurahi kwa ajili yake, ninyi nyote mnaompenda, shangilieni kwa nguvu pamoja naye, ninyi nyote mnaoomboleza juu yake.
שמחו את ירושלם וגילו בה כל אהביה שישו אתה משוש כל המתאבלים עליה
11 Kwa kuwa mtanyonya na kutosheka katika faraja ya matiti yake; mtakunywa sana, na kuufurahia wingi wa mafuriko ya ustawi wake.”
למען תינקו ושבעתם משד תנחמיה למען תמצו והתענגתם מזיז כבודה
12 Kwa kuwa hili ndilo asemalo Bwana: “Nitamwongezea amani kama mto, nao utajiri wa mataifa kama kijito kifurikacho; utanyonya na kuchukuliwa mikononi mwake na kubembelezwa magotini pake.
כי כה אמר יהוה הנני נטה אליה כנהר שלום וכנחל שוטף כבוד גוים--וינקתם על צד תנשאו ועל ברכים תשעשעו
13 Kama mama anavyomfariji mtoto wake, ndivyo nitakavyokufariji wewe, nawe utafarijiwa huko Yerusalemu.”
כאיש אשר אמו תנחמנו--כן אנכי אנחמכם ובירושלם תנחמו
14 Wakati mtakapoona jambo hili, mioyo yenu itashangilia, nanyi mtastawi kama majani; mkono wa Bwana utajulikana kwa watumishi wake, bali ghadhabu yake kali itaonyeshwa kwa adui zake.
וראיתם ושש לבכם ועצמותיכם כדשא תפרחנה ונודעה יד יהוה את עבדיו וזעם את איביו
15 Tazama, Bwana anakuja na moto, magari yake ya vita ni kama upepo wa kisulisuli, atateremsha hasira yake kwa ghadhabu kali, na karipio lake pamoja na miali ya moto.
כי הנה יהוה באש יבוא וכסופה מרכבתיו--להשיב בחמה אפו וגערתו בלהבי אש
16 Kwa maana kwa moto na kwa upanga wake Bwana atatekeleza hukumu juu ya watu wote, nao wengi watakuwa ni wale waliouawa na Bwana.
כי באש יהוה נשפט ובחרבו את כל בשר ורבו חללי יהוה
17 “Watu wote wanaojiweka wakfu na kujitakasa wenyewe ili kwenda bustanini, wakimfuata aliye katikati ya wale ambao hula nyama za nguruwe na panya pamoja na vitu vingine vilivyo machukizo, watafikia mwisho wao pamoja,” asema Bwana.
המתקדשים והמטהרים אל הגנות אחר אחד (אחת) בתוך אכלי בשר החזיר והשקץ והעכבר--יחדו יספו נאם יהוה
18 “Nami, kwa sababu ya matendo yao na mawazo yao, niko karibu kuja na kukusanya mataifa yote na lugha zote, nao watakuja na kuuona utukufu wangu.
ואנכי מעשיהם ומחשבתיהם--באה לקבץ את כל הגוים והלשנות ובאו וראו את כבודי
19 “Nitaweka ishara katikati yao, nami nitapeleka baadhi ya hao walionusurika kwa mataifa, hadi Tarshishi, kwa Puli na Waludi (wanaojulikana kama wapiga upinde), kwa Tubali na Uyunani, hadi visiwa vya mbali ambavyo havijasikia juu ya sifa zangu au kuuona utukufu wangu. Watatangaza utukufu wangu miongoni mwa mataifa.
ושמתי בהם אות ושלחתי מהם פליטים אל הגוים תרשיש פול ולוד משכי קשת--תבל ויון האיים הרחקים אשר לא שמעו את שמעי ולא ראו את כבודי--והגידו את כבודי בגוים
20 Nao watawaleta ndugu zenu wote, kutoka mataifa yote, mpaka kwenye mlima wangu mtakatifu katika Yerusalemu kama sadaka kwa Bwana, juu ya farasi, katika magari ya vita na magari makubwa, juu ya nyumbu na ngamia,” asema Bwana. “Watawaleta, kama Waisraeli waletavyo sadaka zao za nafaka, katika Hekalu la Bwana, katika vyombo safi kwa kufuata desturi za ibada.
והביאו את כל אחיכם מכל הגוים מנחה ליהוה בסוסים וברכב ובצבים ובפרדים ובכרכרות על הר קדשי ירושלם--אמר יהוה כאשר יביאו בני ישראל את המנחה בכלי טהור בית יהוה
21 Nami nitachagua baadhi yao pia wawe makuhani na Walawi,” asema Bwana.
וגם מהם אקח לכהנים ללוים אמר יהוה
22 “Kama vile mbingu mpya na nchi mpya ninazozifanya zitakavyodumu mbele zangu,” asema Bwana, “ndivyo jina lenu na wazao wenu watakavyodumu.
כי כאשר השמים החדשים והארץ החדשה אשר אני עשה עמדים לפני--נאם יהוה כן יעמד זרעכם ושמכם
23 Kutoka Mwezi Mpya hata mwingine, na kutoka Sabato hadi nyingine, wanadamu wote watakuja na kusujudu mbele zangu,” asema Bwana.
והיה מדי חדש בחדשו ומדי שבת בשבתו יבוא כל בשר להשתחות לפני אמר יהוה
24 “Nao watatoka nje na kuona maiti za wale walioniasi mimi. Funza wao hawatakufa, wala moto wao hautazimika, nao watakuwa kitu cha kuchukiza sana kwa wanadamu wote.”
ויצאו וראו--בפגרי האנשים הפשעים בי כי תולעתם לא תמות ואשם לא תכבה והיו דראון לכל בשר

< Isaya 66 >