< Isaya 65 >

1 “Nilijifunua kwa watu wale ambao hawakuniulizia. Nimeonekana na watu wale ambao hawakunitafuta. Kwa taifa lile ambalo halikuliita Jina langu, nilisema, ‘Niko hapa, niko hapa.’
Nilikuwa tayari kuchaguliwa na wale ambao hawakuniomba; Nilikuwa tayari kupatikana kwa wale ambao hawakunitafuta. Nilisema, ''Niko hapa!' kwa taifa ambalo halikuita jina langu.
2 Mchana kutwa nimeinyoosha mikono yangu kwa watu wakaidi, wanaokwenda katika njia ambazo si nzuri, wafuatao mawazo yao wenyewe:
Nimetawanya mikono yangu siku zote kuwasumbua watu wangu, wanao tembea katika njia isiyopasa, wanaotembea kwa kufuata mawazo yao wenyewe na mipango yao.
3 taifa ambalo daima hunikasirisha machoni pangu, wakitoa dhabihu katika bustani na kufukiza uvumba juu ya madhabahu za matofali;
Kuna watu wanoendelea kunipinga mimi, wanatoa sadaka zao katika bustani, na kuchoma ubani juu ya matofali.
4 watu waketio katikati ya makaburi na kukesha mahali pa siri, walao nyama za nguruwe, nazo sufuria zao zina mchuzi wa nyama zilizo najisi,
Wamekaa miongoni mwa makaburi na kuangalia usiku kucha, na hula nyama ya nguruwe na mchuzi mchafu wa nyama katika vyombo vyao.
5 wasemao, ‘Kaa mbali; usinikaribie, kwa maana mimi ni mtakatifu mno kwako!’ Watu wa aina hiyo ni moshi katika pua zangu, ni moto uwakao mchana kutwa.
Wanasema, 'Simama mbali, usisogee karibu na mimi, maana mimi ni mtakatifu zaidi yako.' Vitu hivi ni moshi katika pua zangu, moto uwakao mchana kutwa.
6 “Tazama, jambo hili hubakia limeandikwa mbele zangu: sitanyamaza, bali nitalipiza kwa ukamilifu; nitalipiza mapajani mwao:
Tazama, imeandikwa mbele yangu: Sitanyamaza, Maana nitawalipa wao tena; nitafanya malipo yao katika miguu yao,
7 dhambi zenu na dhambi za baba zenu,” asema Bwana. “Kwa sababu walitoa dhabihu za kuteketezwa juu ya milima na kunichokoza mimi juu ya vilima, nitawapimia mapajani mwao malipo makamilifu kwa matendo yao ya zamani.”
kwa sababu ya dhambi zao na dhambi za baba zao kwa pamoja.'' asema Yahwe. ''Nitawajibu wao kwa kuchoma ubani juu ya milima na kunifanyia mimi juu ya vilima. Hivyo basi nitapima juu ya matendo yao ya kale katika miguu yao.''
8 Hili ndilo asemalo Bwana: “Kama vile divai mpya ingali bado inapatikana katika kishada cha zabibu, nao watu husema, ‘Usikiharibu, kwa kuwa bado kuna kitu kizuri ndani yake,’ hivyo ndivyo nitakavyofanya kwa ajili ya watumishi wangu; sitawaangamiza wote.
Yahwe asema hivi, ''Ikiwa kama juisi itapatikana katika nguzo ya zabibu, wakati mmoja ataposema, 'Usihiaribu hiyo, maa kuna uzuri ndani yake; hichi ndicho nitakachokifanya kwa niaba ya watumishi wangu: Sitawaribu wao wote.
9 Nitawaleta wazao kutoka kwa Yakobo, na kutoka kwa Yuda wale watakaomiliki milima yangu, nao watu wangu wateule watairithi, nako huko wataishi watumishi wangu.
Nitazileta koo kutoka kwa Yakobo, na kutoka Yuda wao ambao watairithi milima yangu. Niliowachagua watairithi aridhi, na watumishi wangu wataishi pale.
10 Sharoni itakuwa malisho kwa ajili ya makundi ya kondoo, na Bonde la Akori mahali pa kupumzikia kwa makundi ya ngʼombe, kwa ajili ya watu wangu wanaonitafuta.
Sharoni itakuwa malisho ya makundi, na bonde la Akori itakuwa sehemu ya kupumzikia ya makundi yangu, kwa watu wangu wanaonitafuta mimi.
11 “Bali kwenu ninyi mnaomwacha Bwana na kuusahau mlima wangu mtakatifu, ninyi mnaoandaa meza kwa ajili ya Bahati, na kujaza mabakuli ya mvinyo uliochanganywa kwa ajili ya Ajali,
Lakini yeye aliyeachana na Yehwe, anayeusahau mlima wangu mtakatifu, anayeandaa meza kwa bahati ya mungu, na kujaza kikombe cha mvinyo uliochanganywa na miungu inayoitwa Hatama.
12 nitawaagiza mfe kwa upanga, nanyi nyote mtainama chini ili kuchinjwa; kwa kuwa niliwaita lakini hamkuitika, nilisema lakini hamkusikiliza. Mlitenda maovu machoni pangu, nanyi mkachagua mambo yale yanayonichukiza.”
Nitaufikisha mwisho wenu kwa upanga, na wato mtainama chini kwa kuchinjwa, Kwa sababu nilipokuita wewe, haukuitikia; nilipozungumza haukunisikliza. lakini mlifanya yaliyo mabaya katika macho yangu na kuchagua kufanya yasiyo nipendeza mimi.''
13 Kwa hiyo hili ndilo asemalo Bwana Mwenyezi: “Watumishi wangu watakula, lakini ninyi mtaona njaa; watumishi wangu watakunywa lakini ninyi mtaona kiu; watumishi wangu watafurahi, lakini ninyi mtaona haya.
Bwana Yahwe asema hivi, ''Tazama, mtumishi atakula, lakini atashikwa na njaa; tazama mtumishi wangu atakunywa lakini atakuwa na kiu; tazama mtumishi wangu atashangilia, lakini atatiwa katika aibu.
14 Watumishi wangu wataimba kwa furaha ya mioyo yao, lakini ninyi mtalia kutokana na uchungu wa moyoni, na kupiga yowe kwa sababu ya uchungu wa roho zenu.
Tazama, mtumishi wangu atapiga kelele za furaha kwa sababu ya furaha ya moyo, lakini utalia kwa sababu ya maumivu ya moyo, na mtapiga kelele kwa sababu ya kusagwa kwa roho zenu.
15 Mtaliacha jina lenu kuwa laana kwa watu wangu waliochaguliwa; Bwana Mwenyezi atawaua ninyi, lakini watumishi wake atawapa jina jingine.
Nanyi mtaliacha jina lenu nyuma kama laana kwa watu niliowachagua wazungumze; Mimi Bwana Yahwe, Nitakuwa wewe; Nitawaita watumishi wangu kwa jina lingine.
16 Yeye aombaye baraka katika nchi atafanya hivyo kwa Mungu wa kweli; yeye aapaye katika nchi ataapa kwa Mungu wa kweli. Kwa kuwa taabu za zamani zitasahaulika na kufichwa kutoka machoni pangu.
Yeyote atakaye tamka baraka juu ya nchi atabarikiwa na mimi, Mungu wa kweli. Yeyote achukuae kiapo juu ya nchi anaapa na mimi, Mungu wa kweli, kwa sababu matatizo ya nyuma yatasaulika, maana yatafichwa machoni pangu.
17 “Tazama, nitaumba mbingu mpya na dunia mpya. Mambo ya zamani hayatakumbukwa, wala hayatakuja akilini.
Maana tazama, Ninakaribia kuumba mbingu mpya na nchi mpya; na mambo ya kale hayatakumbukwa tena wala kufikiriwa katika akili.
18 Lakini furahini na kushangilia daima katika hivi nitakavyoumba, kwa kuwa nitaumba Yerusalemu uwe wa kupendeza, nao watu wake wawe furaha.
Lakini mtakuwa na furaha na kushangilia daima kwa nitakachokiumba. Tazama, Ninakaribia kuumba Yerusalemu mpya kama furaha na watu wake wenye furaha.
19 Nami nitaifurahia Yerusalemu na kuwafurahia watu wangu; sauti ya maombolezo na ya kilio haitasikika humo tena.
Nitafurahia juu ya Yerusalemu watu wangu; kuomboleza na kilio cha dhiki akitasikika tena ndani yake.
20 “Kamwe hatakuwepo tena ndani yake mtoto mchanga atakayeishi siku chache tu, au mzee ambaye hataishi akatimiza miaka yake. Yeye atakayekufa akiwa na umri wa miaka mia moja atahesabiwa kwamba ni kijana tu, yeye ambaye hatafika miaka mia moja, atahesabiwa kuwa amelaaniwa.
Hakuna tena mtoto atakayeishi pale japo kwa siku chache; wala mzee kufa kabla ya mda wake. Yule atakayekufa katika umri wa miaka mia moja atachukuliwa kama mtu mdogo. Yeyote ambaye atashindwa kufikia umri wa miaka mia moja atachukuliwa kama laana.
21 Watajenga nyumba na kuishi ndani yake; watapanda mashamba ya mizabibu na kula matunda yake.
Watazijenga nyumba na kukaa huko, na watapanda mizabibu na kula matunda yake.
22 Hawatajenga nyumba, nao watu wengine waishi ndani yake, au kupanda mazao na wengine wale. Kwa kuwa kama zilivyo siku za mti, ndivyo zitakavyokuwa siku za watu wangu, wateule wangu watafurahia kwa siku nyingi kazi za mikono yao.
Hawatajenga nyumba na wengine waishi humo; hawatapanda, na wengine wale; maana kama siku za miti zitakuwa siku za watu wangu. Watu wangu wataishi kikamilifu kwa kazi ya mikono yao.
23 Hawatajitaabisha kwa kazi bure, wala hawatazaa watoto ili wapatwe na majanga, kwa kuwa watakuwa taifa lililobarikiwa na Bwana, wao na wazao wao pamoja nao.
Hawatafanya kazi bure, wala kuzaa kwa kusikitishwa. Maana ni watoto wa waliobarikiwa na Yahwe, pamoj na koo zao.
24 Kabla hawajaita, nitajibu, nao wakiwa katika kunena, nitasikia.
Kabla hawajaita, nitaitika; na wakati wanaendele kuzungumza, ntisikia. Mbwa mwitu na kondoo watachungwa pamoja, na simba atakula majani kama ng'ombe; lakini udongo utakuwa chakula cha nyoka.
25 Mbwa mwitu na mwana-kondoo watalisha pamoja, naye simba atakula nyasi kama maksai, lakini mavumbi yatakuwa chakula cha nyoka. Hawatadhuru wala kuharibu katika mlima wangu mtakatifu wote,” asema Bwana.
Hawataumiza tena wala kuharibujuu ya mlima wangu mtakatifu,'' asema Yahwe.

< Isaya 65 >