< Isaya 63 >

1 Ni nani huyu anayekuja kutoka Edomu, kutoka Bosra, mwenye mavazi yaliyotiwa madoa mekundu? Ni nani huyu, aliyevikwa joho la kifahari, anayetembea kwa ukuu wa nguvu zake? “Mimi ndimi, nisemaye katika haki, mwenye nguvu wa kuokoa.”
Ni nani ajaye kutoka Edomu, aliyevaa mavazi rangi nyekundu kutoka Bozra? Ni nani aliye katika mavazi ya kifahari, anayetembea kwa kujiamini kwa sababu ya ukuu wa nguvu zake? Ndiye mimi, nizungumzae haki na uwezo mkubwa wa kuokoa.
2 Kwa nini mavazi yako ni mekundu, kama ya yule akanyagaye shinikizo la zabibu?
Kwa nini umevaa mavazi ya rangi nyekundu, na kwan nini wanaonekana kama akanyagae mizabibu katika vyombo vyake.
3 “Nimekanyaga shinikizo la zabibu peke yangu; kutoka mataifa hakuna mtu aliyekuwa pamoja nami. Nimewaponda kwa miguu katika hasira yangu na kuwakanyaga chini katika ghadhabu yangu; damu yao ilitia matone kwenye mavazi yangu, na kutia madoa nguo zangu zote.
Nimekanyaga zabibu lililoko katika vyombo vyenyewe, na hakuna hata mmoja kutoka mataifa aliyeungana na mimi. Niliwakanyaga kwa hasira yangu na niliwakanyaga wao kwa hasira yangu. Damu zao zimeruka katika nguo zangu na kuweka madoa nguo zangu zote.
4 Kwa kuwa siku ya kisasi ilikuwa moyoni mwangu, mwaka wa ukombozi wangu umefika.
Maana niliangalia mbele katika siku ya kisasi, na mwaka wa ukombozi ulikwishawadia.
5 Nilitazama, lakini hakuwepo yeyote wa kunisaidia, nilishangaa kwa kuwa hakuwepo yeyote aliyetoa msaada; hivyo mkono wangu wenyewe ndio ulionifanyia wokovu, na ghadhabu yangu mwenyewe ndiyo iliyonitegemeza.
Mimi nilitazama, na hapo hapakuwa na mtu mmoja hata wa kutoa msaada, lakini mkono wangu mwenywe uliniletea ushindi mimi, na hasira yangu kubwa iliniongoza mimi.
6 Nilikanyaga mataifa kwa miguu katika hasira yangu, katika ghadhabu yangu niliwalewesha, na kumwaga damu yao juu ya ardhi.”
Niliwakanyaga watu wangu chini kwa hasira yangu na kuwafanya wao wanywe laana yangu, na nilimwaga damu zao juu ya nchi.
7 Nitasimulia juu ya wema wa Bwana, kwa matendo ambayo apaswa kusifiwa, sawasawa na yote ambayo Bwana ametenda kwa ajili yetu: naam, mambo mengi mema aliyoyatenda kwa ajili ya nyumba ya Israeli, sawasawa na huruma zake na wema wake mwingi.
Nitakusimulia matendo ya agano la Yahwe lenye kuaminika, matendo ya kusifu ya Yahwe. Nitawasimulia yote ambayo Yahwe ametutendea sisi, na ukuu wa uzuri wake katika nyumba ya Israeli. Huruma hii aliyetuonyesha sisi kwa sababu ya rehema zake na matendo ya agano lake la kuaminika.
8 Alisema, “Hakika wao ni watu wangu, wana ambao hawatanidanganya”; hivyo akawa Mwokozi wao.
Maana alisema, ''Baadhi yao ni watu wangu, watoto ambao sio waaminifu.'' Amekuwa mwokozi wao.
9 Katika taabu zao zote naye alitaabika, na malaika wa uso wake akawaokoa. Katika upendo wake na rehema zake aliwakomboa, akawainua na kuwachukua siku zote zilizopita.
Kupitia mateso yao yote, aliteseka pia, na malaika kutoka mbele yake aliwaokoa wao. Katika upendo wake na rehema aliwakomboa wao, na aliwanyanyua juu na aliwabeba wote katika kipindi chote cha kale.
10 Lakini waliasi, na kumhuzunisha Roho Mtakatifu wake. Hivyo aligeuka na kuwa adui yao, na yeye mwenyewe akapigana dhidi yao.
Lakini walimuasi na kumuuzunisha roho mtakatifu. Hivyo basi akkawa adui wao na kupigana dhidi yao.
11 Ndipo watu wake wakazikumbuka siku zilizopita, siku za Mose na watu wake: yuko wapi yeye aliyewaleta kupitia katikati ya bahari, pamoja na wachungaji wa kundi lake? Yuko wapi yule aliyeweka Roho wake Mtakatifu katikati yao,
Watu wake walifikiri kuhushu nyakati za kale za Musa. Walisema, ''Yuko wapi Mungu, aliyewaleta juu nje ya bahari pamoja na mchungaji wa kundi lake? Yuko wapi Mungu, ambaye aliyeweka roho mtakatifu mwiongoni mwenu?
12 aliyetuma mkono wake uliotukuka wenye nguvu kuwa katika mkono wa kuume wa Mose, aliyegawa maji ya bahari mbele yao, ili kujipatia jina milele,
Yuko wapi Mungu, aliyeufanya wingi wa utukufu wake kwenda katika mkono wa kuume wa Musa, na ukaganya maji mbele yao, kulifanya jina lake milele yeye mwenyewe?
13 aliyewaongoza kupitia kwenye vilindi? Kama farasi katika nchi iliyo wazi, wao hawakujikwaa,
Yuko wapi Mungu, aliyewaongoza katika maji mengi? Kama farasi anayekimbia kwenye aridhi ambayo ni tambarare, hawakua na mashaka.
14 kama ngʼombe washukao bondeni kwenye malisho, walipewa pumziko na Roho wa Bwana. Hivi ndivyo ulivyowaongoza watu wako ili kujipatia mwenyewe jina tukufu.
Kama ng'ombe anayeshuka chini kwenye bonde, Roho ya Yahwe imewapa punziko. Hivyo umewaongoza watu wako, kufanya wewe mwenyewe jina la kusifu.
15 Tazama chini kutoka mbinguni ukaone kutoka kiti chako cha enzi kilichoinuliwa juu, kitakatifu na kitukufu. Uko wapi wivu wako na uweza wako? Umetuzuilia wema wako na huruma zako.
Tazama chini kutoka mbinguni na pata taarifa kutoka kwenye makao ya utukufu wako. Iko wapi bidii yenu na matendo makuu? Uruatendo yako ya uruma yamezuiliwaa kutoka kwetu.
16 Lakini wewe ni Baba yetu, ingawa Abrahamu hatufahamu sisi wala Israeli hatutambui; wewe, Ee Bwana, ndiwe Baba yetu, Mkombozi wetu tangu zamani za kale ndilo jina lako.
Maana wewe n baba yetu, Japokuwa Ibrahimu hatujui sisi, na Israeli haitutambui sisi, wewe, Yahwe, wewe ni baba yetu. Mkombozi wetu limekuwa jina lako kutoka nyakati za kale.
17 Ee Bwana, kwa nini unatuacha twende mbali na njia zako, na kuifanya mioyo yetu migumu hata hatukukuheshimu? Rudi kwa ajili ya watumishi wako, yale makabila ambayo ni urithi wako.
Yahwe, kwa nini unatufanya tangetange na kuifanya mioyo yetu kuwa migumu, hivyo hatukukuheshimu wewe? Rudi kwa niaba ya watumishi wako, kabila la urithi wako.
18 Kwa maana kwa muda mfupi watu wako walimiliki mahali pako patakatifu, lakini sasa adui zetu wamepakanyaga mahali patakatifu pako.
Watu wako walirithi mahali patakatifu kwa mda mfupi, halafu maadui zetu waliwakanyaga.
19 Sisi tumekuwa kama wale ambao hujawatawala kamwe, kama wale ambao hawajaitwa kwa jina lako.
Tumekuwa kama juu ya wale ambao hawajawai kuongoza, kama wale ambao hawajaitwa kwa jina lako.

< Isaya 63 >