< Isaya 63 >
1 Ni nani huyu anayekuja kutoka Edomu, kutoka Bosra, mwenye mavazi yaliyotiwa madoa mekundu? Ni nani huyu, aliyevikwa joho la kifahari, anayetembea kwa ukuu wa nguvu zake? “Mimi ndimi, nisemaye katika haki, mwenye nguvu wa kuokoa.”
¿Quién es este que viene de Edom, con prendas teñidas de Bozrah? ¿Quién es este que es glorioso en su ropa, marchando en la grandeza de su fuerza? “Soy yo quien habla con justicia, poderoso para salvar”.
2 Kwa nini mavazi yako ni mekundu, kama ya yule akanyagaye shinikizo la zabibu?
Por qué su ropa es roja, y tus vestidos como el que pisa la cuba de vino?
3 “Nimekanyaga shinikizo la zabibu peke yangu; kutoka mataifa hakuna mtu aliyekuwa pamoja nami. Nimewaponda kwa miguu katika hasira yangu na kuwakanyaga chini katika ghadhabu yangu; damu yao ilitia matone kwenye mavazi yangu, na kutia madoa nguo zangu zote.
“He pisado el lagar solo. De los pueblos, nadie estaba conmigo. Sí, los pisé en mi ira y los pisoteé en mi ira. Su sangre vital está rociada en mis prendas, y he manchado toda mi ropa.
4 Kwa kuwa siku ya kisasi ilikuwa moyoni mwangu, mwaka wa ukombozi wangu umefika.
Porque el día de la venganza estaba en mi corazón, y el año de mi redención ha llegado.
5 Nilitazama, lakini hakuwepo yeyote wa kunisaidia, nilishangaa kwa kuwa hakuwepo yeyote aliyetoa msaada; hivyo mkono wangu wenyewe ndio ulionifanyia wokovu, na ghadhabu yangu mwenyewe ndiyo iliyonitegemeza.
Miré, y no había nadie para ayudar; y me pregunté si no había nadie que lo defendiera. Por lo tanto, mi propio brazo me trajo la salvación. Mi propia ira me sostuvo.
6 Nilikanyaga mataifa kwa miguu katika hasira yangu, katika ghadhabu yangu niliwalewesha, na kumwaga damu yao juu ya ardhi.”
Yo pisoteé a los pueblos en mi cólera y los emborraché en mi ira. Derramé su sangre vital sobre la tierra”.
7 Nitasimulia juu ya wema wa Bwana, kwa matendo ambayo apaswa kusifiwa, sawasawa na yote ambayo Bwana ametenda kwa ajili yetu: naam, mambo mengi mema aliyoyatenda kwa ajili ya nyumba ya Israeli, sawasawa na huruma zake na wema wake mwingi.
Voy a contar las bondades de Yahvé y las alabanzas de Yahvé, según todo lo que Yahvé nos ha dado, y la gran bondad hacia la casa de Israel, que les ha dado según sus misericordias, y según la multitud de sus amorosas bondades.
8 Alisema, “Hakika wao ni watu wangu, wana ambao hawatanidanganya”; hivyo akawa Mwokozi wao.
Porque dijo: “Ciertamente, ellos son mi pueblo, niños que no traten con falsedad”. por lo que se convirtió en su Salvador.
9 Katika taabu zao zote naye alitaabika, na malaika wa uso wake akawaokoa. Katika upendo wake na rehema zake aliwakomboa, akawainua na kuwachukua siku zote zilizopita.
En toda la aflicción de ellos fue afligido, y el ángel de su presencia los salvó. En su amor y en su piedad los redimió. Él los soportó, y los llevó todos los días de antaño.
10 Lakini waliasi, na kumhuzunisha Roho Mtakatifu wake. Hivyo aligeuka na kuwa adui yao, na yeye mwenyewe akapigana dhidi yao.
Pero se rebelaron y entristeció a su Espíritu Santo. Por eso se volvió y se convirtió en su enemigo, y él mismo luchó contra ellos.
11 Ndipo watu wake wakazikumbuka siku zilizopita, siku za Mose na watu wake: yuko wapi yeye aliyewaleta kupitia katikati ya bahari, pamoja na wachungaji wa kundi lake? Yuko wapi yule aliyeweka Roho wake Mtakatifu katikati yao,
Entonces se acordó de los días de antaño, Moisés y su pueblo, diciendo, “¿Dónde está el que los sacó del mar con los pastores de su rebaño? ¿Dónde está el que puso su Espíritu Santo entre ellos?”
12 aliyetuma mkono wake uliotukuka wenye nguvu kuwa katika mkono wa kuume wa Mose, aliyegawa maji ya bahari mbele yao, ili kujipatia jina milele,
¿Quién hizo que su brazo glorioso estuviera a la derecha de Moisés? ¿Quién dividió las aguas ante ellos, para hacerse un nombre eterno?
13 aliyewaongoza kupitia kwenye vilindi? Kama farasi katika nchi iliyo wazi, wao hawakujikwaa,
Que los condujo a través de las profundidades, como un caballo en el desierto, ¿para que no tropezaran?
14 kama ngʼombe washukao bondeni kwenye malisho, walipewa pumziko na Roho wa Bwana. Hivi ndivyo ulivyowaongoza watu wako ili kujipatia mwenyewe jina tukufu.
Como el ganado que baja al valle, El Espíritu de Yahvé les hizo descansar. Así que dirigiste a tu pueblo para hacerte un nombre glorioso.
15 Tazama chini kutoka mbinguni ukaone kutoka kiti chako cha enzi kilichoinuliwa juu, kitakatifu na kitukufu. Uko wapi wivu wako na uweza wako? Umetuzuilia wema wako na huruma zako.
Mira desde el cielo, y ver desde la morada de tu santidad y de tu gloria. ¿Dónde están tu celo y tus actos de poder? El anhelo de tu corazón y tu compasión se contienen hacia mí.
16 Lakini wewe ni Baba yetu, ingawa Abrahamu hatufahamu sisi wala Israeli hatutambui; wewe, Ee Bwana, ndiwe Baba yetu, Mkombozi wetu tangu zamani za kale ndilo jina lako.
Porque tú eres nuestro Padre, aunque Abraham no nos conoce, e Israel no nos reconoce. Tú, Yahvé, eres nuestro Padre. Nuestro Redentor desde siempre es tu nombre.
17 Ee Bwana, kwa nini unatuacha twende mbali na njia zako, na kuifanya mioyo yetu migumu hata hatukukuheshimu? Rudi kwa ajili ya watumishi wako, yale makabila ambayo ni urithi wako.
Oh, Yahvé, ¿por qué nos haces desviarnos de tus caminos? y endurecer nuestro corazón por tu miedo? Regresa por el bien de tus sirvientes, las tribus de su herencia.
18 Kwa maana kwa muda mfupi watu wako walimiliki mahali pako patakatifu, lakini sasa adui zetu wamepakanyaga mahali patakatifu pako.
Tu pueblo santo lo poseyó sólo por un tiempo. Nuestros adversarios han pisoteado tu santuario.
19 Sisi tumekuwa kama wale ambao hujawatawala kamwe, kama wale ambao hawajaitwa kwa jina lako.
Nosotros, nos hemos vuelto como aquellos sobre los que nunca has gobernado, como los que no fueron llamados por su nombre.