< Isaya 57 >

1 Mwenye haki hupotea, wala hakuna hata mmoja awazaye hilo moyoni mwake; watu wanaomcha Mungu huondolewa, wala hakuna hata mmoja anayeelewa kuwa wenye haki wameondolewa ili wasipatikane na maovu.
Wenye waki watatoweka, lakini hakuna mtu atakayelitia maanani, na watu wa agano la kuaminika wamekusanyika mbali, lakini hakuna mtu anayefahamu kuwa wenye haki wamekusanyika mbali na maovu,
2 Wale waendao kwa unyofu huwa na amani; hupata pumziko walalapo mautini.
Wameingia katika amani; wamepumzika katika vitanda vyao, wale wanotembea katika haki.
3 “Lakini ninyi: Njooni hapa, ninyi wana wa wachawi, ninyi wazao wa wazinzi na makahaba!
Lakini njooni hapa, enyi watoto wa wachawi, watoto wa wazinifu na mwanamke anayefanya ukahaba.
4 Mnamdhihaki nani? Ni nani mnayemcheka kwa dharau, na kumtolea ndimi zenu? Je, ninyi si watoto wa waasi, uzao wa waongo?
Ni nani mnayemfanyia mzaha? dhidi ya wale wanofungua midomo yao na kutoa nje ndimi zao? Je ninyi sio watoto wa uaasi, watoto wa uongo?
5 Mnawaka tamaa katikati ya mialoni na chini ya kila mti uliotanda matawi; mnawatoa kafara watoto wenu kwenye mabonde na chini ya majabali yenye mianya.
Enyi unaowasha wenywe kwa kulala pamoja chini ya mualoni, kila chini ya mti mbichi, ewe unaeua watoto wako katika mabonde yaliyokauka, chini ya miamba inayoning'inia.
6 “Sanamu zilizo katikati ya mawe laini ya mabondeni ndizo fungu lenu; hizo ndizo sehemu yenu. Naam, kwa hizo mmemimina sadaka za vinywaji, na kutoa sadaka za nafaka. Katika haya yote, niendelee kuona huruma?
Miongoni mwa vitu vilaini katika bonde la mto ni mambo uliyopewa uyafanyie kazi. Ni vitu vya ibada yako. Umemwaga nje kinywaji chako kwao na kutoa sadaka ya mazao. Katika haya mambo Je ninaweza kuwa radhi na mambo haya?
7 Umeweka kitanda chako juu kwenye kilima kirefu kilichoinuka, huko ulikwenda kutoa dhabihu zako.
Umeandaa kitanda chako juu ya mlima mrefu; pia umeeda pale juu kutoa sadaka.
8 Nyuma ya milango yako na miimo yako umeweka alama zako za kipagani. Kwa kuniacha mimi, ulifunua kitanda chako, umepanda juu yake na kukipanua sana; ulifanya patano na wale ambao unapenda vitanda vyao, nawe uliangalia uchi wao.
Nyuma ya mlango na mihimili ya milango umeweka ishara zako; umeniweka mimi furagha, umejifunua wewe mwenywe, na kwenda juu; umekifanya kitanda changu kuwa kikubwa. Umefanya agano na wao; ulipenda vitanda vyao; uliona sehemu zao za siri.
9 Ulikwenda kwa Moleki ukiwa na mafuta ya zeituni, na ukaongeza manukato yako. Ukawatuma wajumbe wako mbali sana, ukashuka kwenye kaburi lenyewe! (Sheol h7585)
Ulienda kwa Moleki pamoja na mafuta; umeongeza marashi. Ulimtuma balozi wako mbali sana; Alikwenda chini kuzimu. (Sheol h7585)
10 Ulikuwa umechoshwa na njia zako zote, lakini hukusema, ‘Hakuna tumaini.’ Ulipata uhuisho wa nguvu zako, kwa sababu hiyo hukuzimia.
Ulichoka kwa safari yako ndefu, lakini haukusema, ''Haina matumaini.'' Umeyatafuta maisha katika mkono wako; Hivyo basi haukudhoofika.
11 “Ni nani uliyemhofu hivyo na kumwogopa hata ukawa mwongo kwangu, wala hukunikumbuka au kutafakari hili moyoni mwako? Si ni kwa sababu nimekuwa kimya muda mrefu hata huniogopi?
Ni uliyemuogopa? Ni nani uliye muhofia zaidi ambaye aliyekufanya wewe kutenda udanganyifu, kwa wingi namna hiyo ambapo hauwezi kunikumbuka mimi au kufikiria kuhusu mimi? Maana nilikuwa kimya kwa mda mrefu, hauniogopi mimi tena.
12 Nitaifunua haki yako na matendo yako, nayo hayatakufaidi.
Nitatangaza matendo haki yako na nitawaambia kila kitu ulichokifanya, lakini hawatakusaidia.
13 Utakapolia kwa kuhitaji msaada, sanamu zako ulizojikusanyia na zikuokoe! Upepo utazipeperusha zote, pumzi peke yake itazipeperusha, Lakini mtu atakayenifanya kimbilio lake, atairithi nchi na kuumiliki mlima wangu mtakatifu.”
Utakapolia nje, wacha sanamu ulizozikusnya zikusaidie wewe. Badala yake upepo utavipeperusha vyote, punzi itavipeperusha mbali. Lakini yeye anayenikimbilia mimi atairithi aridhi na atachukua umiliki katika mlima wangu mtakatifu.
14 Tena itasemwa: “Jengeni, jengeni, itengenezeni njia! Ondoeni vikwazo katika njia ya watu wangu.”
Atasema, 'Jenga, jenga! safisha njia! ondoeni vizuizi vyote katika njia ya watu wangu!''
15 Kwa maana hili ndilo asemalo Aliye juu, yeye aliyeinuliwa sana, yeye aishiye milele, ambaye jina lake ni Mtakatifu: “Ninaishi mimi mahali palipoinuka na patakatifu, lakini pia pamoja na yeye aliye na roho iliyotubu na mwenye roho ya unyenyekevu, ili kuzihuisha roho za wanyenyekevu na kuihuisha mioyo yao waliotubu.
Maana yeye allye juu palipoinuka, anayeishi katika uzima wa milele, ambaye jina lake ni mtakatifu, asema hivi, ''Ninaishi mahali pa juu na mahali patakatifu pamoja na yeye pia aliyemnyenyekevu na moyo uliopondeka, ili kuzifufua roho za wanyenyekevu na kufufua mioyo ya wanaojutia.
16 Sitaendelea kulaumu milele, wala sitakasirika siku zote, kwa kuwa roho ya mwanadamu ingezimia mbele zangu: yaani pumzi ya mwanadamu niliyemuumba.
Maana sitawahukumu milele, wala sitakuwa na hasira milele, Kisha roho ya mtu itazimia mbele yangu, maisha niliyowafanyia.
17 Nilighadhibika na tamaa yake ya dhambi; nilimwadhibu, nikauficha uso wangu kwa hasira, na bado aliendelea katika njia zake za tamaa.
Kwa sababu ya dhambi ya mapato ya vurugu zake, Nilipatwa na hasira, na nikamuadhibu yeye; niliuficha uso wangu, nilikuwa na hasira, lakini alirudi nyuma katika njia za moyo wake mwenyewe.
18 Nimeziona njia zake, lakini nitamponya, nitamwongoza na kumrudishia upya faraja,
Nimeziona njia zake, lakini nitamoponya yeye. Nitamuongoza yeye na kumfariji na kuwashauri wale wanomliliia yeye,
19 nikiumba sifa midomoni ya waombolezaji katika Israeli. Amani, amani, kwa wale walio mbali na kwa wale walio karibu,” asema Bwana. “Nami nitawaponya.”
na natengeneza tunda la midomo. Amani, amani, kwa wale walio mbali sana na wale walio karibu-asema Yahwe nitawaponya ninyi.
20 Bali waovu ni kama bahari ichafukayo, ambayo haiwezi kutulia, mawimbi yake hutupa takataka na matope.
Lakini waovu ni kama bahari iliyochafuka, haiwezi kutulia, na maji yake yametanda juu ya matope.
21 Mungu wangu asema, “Hakuna amani kwa waovu.”
Hakuna amani kwa wakosaji asema Mungu.''

< Isaya 57 >