< Isaya 56 >

1 Hili ndilo asemalo Bwana: “Dumisheni haki na mkatende lile lililo sawa, kwa maana wokovu wangu u karibu na haki yangu itafunuliwa upesi.
Yahwe asema hivi, ''Fanyeni yaliyo sahihi, fanyeni yaliyo ya haki; maana wakovu wangu u karibu, na haki yangu inakaribia kujidhihirisha.
2 Amebarikiwa mtu yule atendaye hili, mtu yule alishikaye kwa uthabiti, yeye ashikaye Sabato bila kuinajisi, auzuiaye mkono wake usifanye uovu wowote.”
Abarikiwe mtu yule ataendae haya, anayeyashika sana. Anaifuata sabato, na haitii unajisi, azuiaye mkono wake usitende maovu.''
3 Usimwache mgeni aambatanaye na Bwana aseme, “Hakika Bwana atanitenga na watu wake.” Usimwache towashi yeyote alalamike akisema, “Mimi ni mti mkavu tu.”
Usimuache mgeni yeyote aliyekuwa mfuasi wa Yahwe aseme, ''Yahwe atahakikisha ananiondoa kwa watu wake.'' Toashi ataweza kusema, ''tazama, mimi ni mti mkavu.''
4 Kwa kuwa hili ndilo asemalo Bwana: “Kwa matowashi washikao Sabato zangu, ambao huchagua kile kinachonipendeza na kulishika sana agano langu:
Yahwe asema hivi, kwa matoashi wanaoitimiza sabato yangu huchagua mambo yanayonipendeza mimi, na hushika kwanza agano langu,
5 hao nitawapa ndani ya Hekalu langu na kuta zake kumbukumbu na jina bora kuliko kuwa na watoto wa kiume na wa kike: nitawapa jina lidumulo milele, ambalo halitakatiliwa mbali.
kwao nitaiweka nyumba yangu na ndani ya kuta zangu kumbukumbu ambayo ni kubwa kuliko kuwa na vijana na mabinti. Nitawapa kumbumbu ya milele ambalo halitaondolewa.
6 Wageni wanaoambatana na Bwana ili kumtumikia, kulipenda jina la Bwana, na kumwabudu yeye, wote washikao Sabato bila kuinajisi na ambao hushika sana agano langu:
Pia wageni ambao wataungana wenyewe kwa Yahwe- kwa ajili ya kumtumikia yeye, na yeye alipendae jina la Yahwe, kumuabudu yeye, na kila anayeheshimu sabato na wale wanoitunza isitiwe najisi, na wale walishikao agano langu
7 hawa nitawaleta kwenye mlima wangu mtakatifu na kuwapa furaha ndani ya nyumba yangu ya sala. Sadaka zao za kuteketeza na dhabihu zao zitakubalika juu ya madhabahu yangu; kwa maana nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala kwa mataifa yote.”
nitawaleta katika mlima wangu mtakatifu na kuwafaya muwe na furaha katika nyumba yangu ya maombi; matoleo na sadaka zenu zitakubalika katika mathebau yangu. Maana nyumba yangu itaitwa nyumba ya maombi kwa mataifa yote.
8 Bwana Mwenyezi asema, yeye awakusanyaye Waisraeli waliohamishwa: “Bado nitawakusanya wengine kwao zaidi ya hao ambao wamekusanywa tayari.”
Hili ni tamko la Yahwe, anayewakusanya watu wenye ukiwa katika Israeli- nitaendelea kuwakusanya wenginwe ili kuwaongeza wao.''
9 Njooni, enyi wanyama wote wa kondeni, njooni mle, ninyi wanyama wote wa mwituni!
Enyi nyote wanyama pori mlioko porini, njooni na mle, enyi wanyama mlioko msituni, Walinzi wao wote ni vipofu, hawaelewi.
10 Walinzi wa Israeli ni vipofu, wote wamepungukiwa na maarifa; wote ni mbwa walio bubu, hawawezi kubweka; hulala na kuota ndoto, hupenda kulala.
Wote ni mbwa wapole ambao hawawezi kubweka. Wanaota, na wanalala chini maana wanapenda kulala.
11 Ni mbwa wenye tamaa kubwa, kamwe hawatosheki. Wao ni wachungaji waliopungukiwa na ufahamu; wote wamegeukia njia yao wenyewe, kila mmoja hutafuta faida yake mwenyewe.
Mbwa wanahamu kubwa; hawajawahi kuridhika; wachungaji wao hawawatambui; wamejeuka katika njia zao wenyewe, kila mmoja ana tamaa kupata faida isiyo yaa haki.
12 Kila mmoja hulia, “Njooni, tupate mvinyo! Tunywe kileo sana! Kesho itakuwa kama leo, au hata bora zaidi.”
''Njooni, ''Tunywe mvinyo na pombe. Kesho itakuwa kama leo, siku kubwa zaidi ya kipimo.''

< Isaya 56 >