< Isaya 55 >

1 “Njooni, ninyi nyote wenye kiu, njooni kwenye maji; nanyi ambao hamna fedha, njooni, nunueni na mle! Njooni, nunueni divai na maziwa bila fedha na bila gharama.
''Njooni, kila aliye na kiu, njooni kwenye maji! na ewe usio na pesa, njoo, ununua na ule! Njoo, nunua mvinyo na maziwa pasipo pesa na pasipo gharama.
2 Kwa nini kutumia fedha kwa kitu ambacho si chakula, na kutaabikia kitu kisichoshibisha? Sikilizeni, nisikilizeni mimi na mle kilicho kizuri, nazo nafsi zenu zitafurahia utajiri wa unono.
Kwa nini tunapima fedha kwa kitu ambacho sio mkate? na kufanya kazi isiyoridhisha? Nisikilizeni mimi kwa makini na ule kilicho kizuri, na kujifurahisha mwenyewe kwa unono.
3 Tegeni sikio mje kwangu, nisikieni mimi, ili nafsi zenu zipate kuishi. Nitafanya agano la milele nanyi, pendo la uaminifu nililomwahidi Daudi.
Jeuzeni masikio yenu, na mje kwangu! Sikiliza, iliuweze kuishi! Nitafanya agano ya milele na ninyi; pendo langu la kuaminika nililomuhaidi Daudi.
4 Tazama, nimemfanya kuwa shahidi wa mataifa, kiongozi na jemadari wa mataifa.
Tazama, nimwemuweka yeye kama shahidi kwa mataifa, kama kiiongozi na kamanda wa watu.
5 Hakika utaita mataifa usiyoyajua, nayo mataifa yale yasiyokujua yataharakisha kukujia, kwa sababu ya Bwana Mungu wako, yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli, kwa maana amekutukuza.”
Tazama, utaliita taifa ambalo haulijui; na taifa ambalo halikujui wewe litakukimbilia wewe kwa sababu wewe ni Yahwe Mungu wao, Mtakatifu wa Israeli, yeye aliyekutukuza wewe.
6 Mtafuteni Bwana maadamu anapatikana; mwiteni maadamu yu karibu.
Mtafuteni Yahwe maana anapatikana; muiteni yeye maana yu karibu.
7 Mtu mwovu na aiache njia yake, na mtu mbaya na ayaache mawazo yake. Yeye na amrudie Bwana, naye atamrehemu, arudi kwa Mungu wetu, kwa kuwa atamsamehe bure kabisa.
Tuwaache waovu waziache njia zao, na mtu mwenye dhambi mawazo yake. Muache yeye arudi kwa Yahwe, na atamuhurumia yeye, na kwa Mungu wetu, yeye ambaye atamsamehe huyo kwa wingi.
8 “Kwa kuwa mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu,” asema Bwana.
Maana mawazo yangu sio mawazo yenu, wala njia zangu sio njia zenu- Hili ni tamko la Yahwe-
9 “Kama vile mbingu zilivyo juu kuliko dunia, ndivyo njia zangu zilivyo juu kuliko njia zenu na mawazo yangu kuliko mawazo yenu.
maana kama vile mbingu zilivyo juu kuliko nchi, hivyo ndivyo njia zangu zilivyo juu kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu.
10 Kama vile mvua na theluji ishukavyo kutoka mbinguni, nayo hairudi tena huko bila kunywesha dunia na kuichipusha na kuistawisha, hivyo hutoa mbegu kwa mpanzi na mkate kwa mlaji,
Maana kama mvua na theluji zishukavyo chini kutoka mbinguni na hazirudi tena pale isipokuwa kueneza nchi na kufanya uzalishaji na chipukizi na kutoa mbegu kwa wakulima waliopanda na mkate kwa walaji,
11 ndivyo lilivyo neno langu lile litokalo kinywani mwangu: Halitanirudia tupu, bali litatimiliza lile nililokusudia na litafanikiwa katika kusudi lile nililolituma.
hivyo neno langu litakuwa linalotoka kwenye mdomo wangu: halitanirudia tena mimi bure, Lakini itatimiza lilie nililokusudia, na litatimiza lile nililolituma.
12 Mtatoka nje kwa furaha na kuongozwa kwa amani; milima na vilima vitapaza sauti kwa nyimbo mbele yenu, nayo miti yote ya shambani itapiga makofi.
Maana utakwenda nje katika furaha na utaongozwa kwa amani; Milima na vilima vitapaza sauti kwa furaha mbele yako, na miti yote shambani itapiga makofi.
13 Badala ya kichaka cha miiba itaota miti ya misunobari, na badala ya michongoma utaota mhadasi. Hili litakuwa jambo la kumpatia Bwana jina, kwa ajili ya ishara ya milele, ambayo haitaharibiwa.”
Badala ya miiba ya porini, misonobari itakuwa; na badala ya mbigiri, mihadasi inaota, na itakuwa kwa Yahwe, maana jina lake, ni kama alama ya milele ambayo haiwezi kuondolewa.''

< Isaya 55 >