< Isaya 53 >
1 Ni nani aliyeamini ujumbe wetu, na mkono wa Bwana umefunuliwa kwa nani?
Ni nani angeweza kuamini tuliyasikia? Na mkono wa Yahwe, kwake uliojidhihirisha?
2 Alikua mbele yake kama mche mwororo na kama mzizi katika nchi kavu. Hakuwa na uzuri wala utukufu wa kutuvutia kwake, hakuwa na chochote katika sura yake cha kutufanya tumtamani.
Maana amekuwa mbele za Yahwe kama sampuli, na kama chipukizikatika aridhi kavu; hakuna maajabu yalionekana au mapambo; tulipo muona yeye, hapakuwa na uzuri kutuvutia sisi.
3 Alidharauliwa na kukataliwa na wanadamu, mtu wa huzuni nyingi, ajuaye mateso. Kama mtu ambaye watu humficha nyuso zao, alidharauliwa, wala hatukumhesabu kuwa kitu.
Alidharauliwa na kukataliwa na watu; mtu wa huzuni, na mwenye maumivu. Kama mmoja aliyetoka kwa watu wafichao nyuso zao, alidharauliwa; na kujfikiria kuwa asiye na faida.
4 Hakika alichukua udhaifu wetu na akajitwika huzuni zetu, hata hivyo tulidhania kuwa amepigwa na Mungu, akapigwa sana naye, na kuteswa.
Lakini hakika amezaliwa ugonjwa wetu na kubeba huzuni yetu; tulidhani aliadhibiwa na Mungu, amepigwa na Mungu, na kutaabishwa.
5 Lakini alitobolewa kwa ajili ya makosa yetu, alichubuliwa kwa ajili ya maovu yetu; adhabu iliyotuletea sisi amani ilikuwa juu yake, na kwa majeraha yake sisi tumepona.
Lakini alichomwa kwa sababu ya uaasi wa matendo yetu; aliangamizwa kwa sababu ya dhambi zetu. Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, na kwa majeraha yake sisi tumepona.
6 Sisi sote, kama kondoo, tumepotea, kila mmoja wetu amegeukia njia yake mwenyewe, naye Bwana aliweka juu yake maovu yetu sisi sote.
Sisi ni kama kondoo tumepotoka; kila mmoja amejeuka katika njia yake, na Yahwe amemueka juu yake maovu kwetu sisi sote.
7 Alionewa na kuteswa, hata hivyo hakufungua kinywa chake; aliongozwa kama mwana-kondoo apelekwaye machinjoni, kama vile kondoo anyamazavyo mbele ya wao wamkataye manyoya, hivyo hakufungua kinywa chake.
Aliteswa; lakini alinyenyekea mwenyewe, hakufungua mdomo wake; kama kondooendae kuchinjwa, na kama kondoo mbele ya mtu anayemkata mnyoa yake taratibu, hivyo hakufungua mdomo wake.
8 Kwa kuonewa na kuhukumiwa aliondolewa. Nani awezaye kueleza kuhusu kizazi chake? Kwa maana alikatiliwa mbali na nchi ya walio hai, alipigwa kwa ajili ya makosa ya watu wangu.
Kwa kutumia nguvu na hukumu yeye aliyelaaniwa; ni katika kizazi hicho atafikiria zaidi kuhusu yeye? Lakini aliondolewa katika aridhi ya walio hai; kwa sababu ya makosa ya watu wangu na adhabu ilikuwa juu yake.
9 Wakamfanyia kaburi pamoja na waovu, pamoja na matajiri katika kifo chake, ingawa hakutenda jeuri, wala hapakuwa na hila kinywani mwake.
Wameliweka kaburi lake pamoja nawahalifu, kwa utajiri wa mtu katika kifo chake ingawa hakuwa na vurugu wala udanganyifu wowote katika mdomo wake.
10 Lakini yalikuwa ni mapenzi ya Bwana kumchubua na kumsababisha ateseke. Ingawa Bwana amefanya maisha yake kuwa sadaka ya hatia, ataona uzao wake na kuishi siku nyingi, nayo mapenzi ya Bwana yatafanikiwa mkononi mwake.
Lakini yalikuwa ni mapenzi ya Yahwe kumponda yeye na kumfanya yeye apone. Alipoyafanya maisha yake kuwa sadaka kwa ajili ya dhambi, ataona watoto wake, ataongeza siku zao, na mapenzi ya Yahwe yatatimizwa kupitia yeye.
11 Baada ya maumivu ya nafsi yake, ataona nuru ya uzima na kuridhika; kwa maarifa yake, mtumishi wangu mwenye haki atawafanya wengi kuwa wenye haki, naye atayachukua maovu yao.
Baada ya mateso ya maisha yake, ataona mwanga na ataridhika kwa maarifa yake.
12 Kwa hiyo nitamgawia sehemu miongoni mwa wakuu, naye atagawana nyara pamoja na wenye nguvu, kwa sababu aliyamimina maisha yake hadi mauti, naye alihesabiwa pamoja na wakosaji. Kwa kuwa alichukua dhambi za wengi, na kuwaombea wakosaji.
Hivyo basi Je ninaweza kumpa yeye sehemu yake miongoni mwa wengi, naye atatawnya mateka kwa wengi, kwa sabubu amejionyesha yeye mwenye kwenye kifo na amehesabiwa na wahalifu. Amezaa dhambi za wengi na kufanya maombolezo kwa wahalifu.