< Isaya 50 >

1 Hili ndilo asemalo Bwana: “Iko wapi hati ya talaka ya mama yako ambayo kwayo niliachana naye? Au nimewauza ninyi kwa nani miongoni mwa watu wanaonidai? Kwa ajili ya dhambi zenu mliuzwa, kwa sababu ya makosa, mama yenu aliachwa.
Yahwe asema hivi, ''Kiko wapi cheti cha talaka ambacho nimempa tataka mama yako? na kwa nani niliowauza mimi? Tazama, umewauza kwa sababu ya dhambi zako, na kwa sababu ya uasi wako, na mama yako amepelekwa mbali.
2 Nilipokuja, kwa nini hakuwepo hata mmoja? Nilipoita, kwa nini hakuwepo hata mmoja wa kujibu? Je, mkono wangu ni mfupi mno hata nisiweze kuwakomboa? Je, mimi sina nguvu za kukuokoa? Kwa kukemea tu naikausha bahari, naigeuza mito ya maji kuwa jangwa; samaki wake wanaoza kwa kukosa maji na kufa kwa ajili ya kiu.
Kwa nini nimekuja maana hakuna mtu pale? Kwa nini nimeita lakini hakuna aliyejibu? Je mkono wangu ni mfupi kukufidia wewe? Je hakuna nguvu katika ukombozi wngu kwako? Tazama, maonyo yangu, nimeikausha bahari; nimeufanya mto kuwa jangwa; samaki wake wamekufa na kuoza kwa kukosa maji.
3 Ninalivika anga weusi na kufanya nguo ya gunia kuwa kifuniko chake.”
Nimelivisha giza; na ku kwa ngfunika nguo za magunia.''
4 Bwana Mwenyezi amenipa ulimi uliofundishwa, ili kujua neno limtegemezalo aliyechoka. Huniamsha asubuhi kwa asubuhi, huamsha sikio langu lisikie kama mtu afundishwaye.
Bwana Yahwe amenipa mimi lugha kama wale wanayofundishwa, ili kwamba nizungumze maneno ya kudumisha kwa yeye aliyechoka; huniamsha mimi asubuhi kwa asubuhi; huyaamsha masikio yangu kama wale wanofundisha.
5 Bwana Mwenyezi amezibua masikio yangu, nami sikuwa mwasi, wala sikurudi nyuma.
Bwana Yahwe amefungua sikio langu, na sikuaasi, wala kurudi nyuma.
6 Niliwapa mgongo wangu wale wanipigao, mashavu yangu wale wangʼoao ndevu zangu; sikuuficha uso wangu kutokana na fedheha na kutemewa mate.
Niliwapa mgongo wangu wale wanaonipiga mimi, na shavu langu kwa wale wanaopokonya nje ndevu zangu; Sitouficha uso wangu kutokana na matendo ya aibu na kutema mate.
7 Kwa sababu Bwana Mwenyezi ananisaidia, sitatahayarika. Kwa hiyo nimekaza uso wangu kama jiwe la gumegume, nami ninajua sitaaibika.
Maana Bwana Yahwe atanisaidia mimi; hivyo basi sitapatwa na aibu; hivyo nimeufanya uso wangu kama jiwe, maana ninajua kwamba sitaabishwa.
8 Yeye anipatiaye haki yangu yu karibu. Ni nani basi atakayeleta mashtaka dhidi yangu? Tukabiliane uso kwa uso! Mshtaki wangu ni nani? Ni nani aliye mshtaki wangu?
Yeye aliye nitakasa mimi yu karibu. Ni nani atakayenipinga mimi? Basi na tusimame tufarijiane mmoja mmoja. Nani aliye mshitaki? Muache aje karibu na mimi.
9 Ni Bwana Mwenyezi anisaidiaye mimi. Ni nani huyo atakayenihukumu? Wote watachakaa kama vazi, nondo watawala wawamalize.
Tazama, Bwana Yahwe atanisaidia mimi. Nani atakayetangaza kuwa mimi ni mwenye hatia? Tazama, watavaa nje kama vazi; mdomo utawala wao juu.
10 Ni nani miongoni mwenu amchaye Bwana, na kulitii neno la mtumishi wake? Yeye atembeaye gizani, yeye asiye na nuru, na alitumainie jina la Bwana, na amtegemee Mungu wake.
Ni nani miongoni mwenu anayemuogopa Yahwe? Ni nani anayehieshimu sauti ya Yahwe? Ni nani atakayetembea kwenye giza nene pasipo mwanga?
11 Lakini sasa, ninyi nyote mnaowasha mioto, na kupeana mienge iwakayo ninyi kwa ninyi, nendeni, tembeeni katika nuru ya moto wenu na ya mienge mliyoiwasha. Hili ndilo mtakalolipokea kutoka mkononi mwangu: Mtalala chini kwa mateso makali.
Tazama, ninyi nyote mnaowasha, ni nani aliyewapa wenyewe kwa tochi: tembeni katika mwanga wa moto wenu na katika moto mliouwasha. Hili ndilo mlilopokea kutoka kwangu: utalala chini katika mahali pachungu.

< Isaya 50 >